Njoo, Unifuate
Aprili 15–21. Pasaka: ‘Ku Wapi, Ewe Mauti, Kushinda Kwako?’


“Aprili 15–21. Pasaka: ‘Ku Wapi, Ewe Mauti, Kushinda Kwako?’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Aprili 15–21. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Kaburi la Bustani.

Aprili 15–21.

Pasaka

“Ku Wapi, Ewe Mauti, Kushinda Kwako?”

Unapojiandaa kufundisha wiki hii, fikiria jinsi majadiliano ya darasa lako kuhusu Jumapili ya Pasaka yavyoweza kujenga imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Waulize washiriki wa darasa jinsi watakavyojibu maswali kama “Upatanisho wa Yesu Kristo ni nini?” na “Ninawezaje kupokea baraka za Upatanisho wa Kristo? Je, walisoma maandiko yoyote wiki hii ambayo yanasaidia kujibu maswali haya?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Yesu Kristo anatuokoa kutoka kwenye dhambi na kifo, anatuimarisha katika udhaifu wetu, na anatufariji katika majaribu yetu.

  • Je, washiriki wa darasa lako wanaelewa kwamba zaidi ya kushinda dhambi na kifo, Yesu Kristo anaweza pia kutufariji katika majaribu yetu na kutuimarisha katika udhaifu wetu? Njia mojawapo ya kuwasaidia kugundua kanuni hizi ingeweza kuwa kuandika maneno haya ubaoni: Dhambi, Kifo, Udhaifu. Muombe kila mshiriki wa darasa kusoma mojawapo ya maandiko yaliyoorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada” na kutakafari jinsi Mwokozi anavyotusaidia kushinda au kuvumilia vitu hivi. Washiriki wa darasa wanaweza kuandika kile walichojifunza kutoka katika maandiko haya chini ya kila kichwa cha habari na kushiriki ushuhuda wao wa Mwokozi na Upatanisho Wake.

  • Maandiko yanafundisha nini kuhusu gharama Yesu Kristo alilipa kwa ajili ya wokozi wetu? Kwa mfano, ona Luka 22:39–44; Mosia 3:7; na Mafundisho na Maagano 19:16–19. Ni gharama gani Baba yetu wa Mbinguni alilipa? (ona Yohana 3:16).

    Picha
    Kusulibiwa kwa Kristo

    Kusulibiwa kwa Kristo, na Louise Parker

  • Kabla ya darasa, fikiria kuwaita washiriki wa darasa wachache kuleta dondoo kutoka ujumbe wa mkutano mkuu ambayo inaelezea jinsi Mwokozi anavyotubariki kupitia Upatanisho Wake (kwa baadhi ya mifano, ona “Nyenzo za Ziada”). Mafundisho ya manabii wa kisasa yanapanua uelewa wetu wa baraka za Upatanisho wa Mwokozi kwa njia gani? Yanaimarisha vipi ushuhuda wetu wa nguvu ya Upatanisho?

  • Pengine somo la kitu rahisi lingeweza kusaidia kuonyesha tofauti kati ya kusafishwa tokana na dhambi na kufanywa mkamilifu: unaweza kuandika ubaoni mistari michache kutoka Moroni 10:32, lakini jumuisha tahajia au makosa ya kisarufi. Kisha waulize washiriki wa darasa kufuta makosa. Je, hii ilitatua tatizo? Ni masomo gani tunayojifunza kutoka kwenye maandiko haya na somo hili la kitu kuhusu athari ambayo Upatanisho unaweza kuwa juu yetu. Kauli hii kutoka kwa Rais Dieter F. Uchtdorf inaweza pia kusaidia: “Kama wokovu unamaanisha kufuta makosa yetu na dhambi tu, basi wokovu—wa ajabu kama ulivyo—haukamilishi hamu ya Baba kwetu sisi. Nia yake ni ya juu zaidi: Anawataka wana na mabinti wake kuwa kama Yeye” (‘Karama ya Rehema, Ensign au Liahona, Mei 2015, 108).

  • Hadithi na anolojia inaweza kutusaidia kuelewa Upatanisho wa Kristo. Mathalani, Mzee Jeffrey R. Holland anashiriki hadithi kuhusu ndugu wawili wakipanda ukuta wa korongo kubwa katika ujumbe wake “Where Justice, Love, and Mercy Meet” (Ensign au Liahona, mei 2015, 104–6). Kuna pia video yenye kichwa cha habari kama hicho kwenye LDS.org. Au mnaweza kuangalia pamoja “Handel’s Messiah: Debtor’s Prison” (LDS.org; ona maelezo katika “Nyenzo za Ziada”) na kujadiliana jinsi Upatanisho wa Yesu Kristo unavyotuweka huru kutoka magereza yetu.

Mashahidi katika Agano Jipya walitoa ushuhuda kwamba Yesu Kristo alishinda kifo.

  • Fikiria kurejea maelezo ya kimaandiko ya Pasaka ya kwanza—Kufufuka kwa Yesu Kristo. Unaweza kumwambia mshiriki wa darasa kueleza tena hadithi katika maneno yake mwenyewe (ona Yohana 20:1–17). Unaweza pia kuonyesha video ya Biblia, kama vile “He Is Risen” (LDS.org).

  • Labda darasa lako lingepata kwa undani zaidi uelewa wa umuhimu wa mashahidi wa Kufufuka kwa Yesu Kristo kama wanajifikiria wao ni wanasheria au waandishi wa habari wanapeleleza madai kwamba Kristo alifufuka. Waalike wao watafute watu katika maandiko ambao wangefaa kama mashahidi (ona Mathayo 28:1–10; Luka 24:13–35; Yohana 20:19–29; 1 Wakorintho 15:3–8, 55–58). Wanaweza hata kuandika muhtasari mfupi wa nini watu hawa wangeweza kusema wakati wa kushuhudia katika mahakama au wakati wakihojiwa kwa ajili ya taarifa ya habari.

  • Njia mojawapo ya kuongeza shukrani zetu kwa kina kwa ajili ya Kufufuka kwa Mwokozi ni kufikiria kuhusu jinsi tutakavyoelezea imani zetu kwa wengine. Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki vipi ushuhuda wao wa Yesu Kristo katika hali zifuatazo: mwana familia amebainika ana ugonjwa wa hatari; rafiki amempoteza mpendwa wake; jirani anauliza kwa nini mnasherehekea Pasaka. Wahimize warejee maandiko (kama hayo katika “Nyenzo za Ziada”) wanapopanga majibu yao. Waalike wanafunzi wachache kushiriki mawazo yao.

Yesu Kristo anatupa matumaini na furaha.

  • Tunaweza sote kuwa na matumaini na kufurahi kwa sababu ya Mwokozi. Unaweza kusoma Yohana 16:33 na kujadili jinsi Upatanisho wa Yesu Kristo unavyotusaidia kuwa wenye furaha licha ya majaribu yetu. Jinsi gani tulivyopokea furaha na kusaidiwa wakati wa majaribu yetu.

  • Kusoma ushuhuda wa Petro katika 1 Petro 1:3–11 kungeweza kuwapa washiriki wa darasa matumaini yaliyoongezeka katika Upatanisho wa Yesu Kristo. Wape muda kutakafari aya hizi na kufanya kazi katika majozi kutafuta maandiko mengine ambayo pia yanaelezea jinsi ya kupata matumaini katika Yesu Kristo (ona kitabu cha mwongozo, “Matumaini”). Wanaweza kutumia maandiko wanayopata kutengeneza bango la kuonyesha katika nyumba zao au kwenye mtandao (ona mifano ya picha za dondoo zenye mwongozo kwenye LDS.org). Washiriki wa darasa wangeweza kufikiria hali za wanafamila au marafiki watakaohitaji kuhisi zaidi kimatumaini.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ungewatia moyo vipi washiriki wa darasa kusoma Mathayo 18 na Luka 10? Unaweza kuwaambia kwamba sura hizi zina mafumbo mawili ya kukumbukwa ya Mwokozi, yote yanabeba masomo muhimu kuhusu jinsi tungetendeana sisi kwa sisi.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Pasaka

Maandiko kuhusu Upatanisho wa Mwokozi.

Ujumbe kuhusu Upatanisho wa Mwokozi.

Nyimbo kuhusu Upatanisho wa Mwokozi.

Washiriki wa darasa wanaweza kufurahia kuimba baadhi ya nyimbo hizi na kusoma maandiko husika yaliyotajwa chini ya ukurasa. Baadhi ya washiriki wa darasa labda wamejifunza baadhi ya nyimbo kama sehemu ya mafunzo ya maandiko ya wiki ya familia zao; wahimize washiriki uzoefu wao.

Video kuhusu Pasaka

Kila mwaka Kanisa huleta jumbe za Pasaka, ambazo zinapatikana kwenye mormon.org/easter

Yesu Kristo anatuweka huru.

Mnamo mwaka 1741, George Frideric Handel alitunga muziki simulizi kuhusu Yesu Kristo wenye jina Masiya. Handel alikusudia kwamba mapato ya maonyesho ya Masiya yatatolewa kama mchango kulipia kuwaachilia wadeni kutoka katika gereza la wadeni. Zaidi ya watu 140 waliokuwa wamefungwa kwa sababu walikuwa hawawezi kulipa madeni yao waliachiwa huru kama matokeo yake. Akitoa maoni yake juu ya tukio hili, Rais Russell M. Nelson alisema, “Bila Upatanisho wa Yesu Kristo, wote tungekuwa tunadaiwa bila matumaini, kama vile wale watu walivyokuwa katika gereza la wadeni. Mkombozi wetu, Bwana Yesu Kristo, alikuja kulipa deni ambalo hakuwa mdeni kwa sababu tulikuwa na deni ambalo tusingeweza kulipa.” Kwa video inayoonesha tukio hili, ona ‘Handel’s Messiah: Debtor’s Prison” kwenye LDS.org.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa chombo cha Roho. Lengo lako kama mwalimu sio kuwasilisha somo bali ni kuwasaidia wengine kupokea ushawishi wa Roho Mtakatifu—ambaye ni mwalimu wa kweli. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 10.)

Chapisha