Aprili 1–14 Mathayo 16–17: Marko 9: Luka 9: ‘Wewe ndiwe Kristo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili; Agano Jipya 2019 (2019)
“Aprili 1–14. Mathayo 16–17; Marko 9 ; Luka 9 Njoo, Unifuate—Kwa Aili ya Shule ya Jumapili: 2019
Aprili 1–14
Mathayo 16–17; Marko 9; Luka 9
“Wewe Ndiwe Kristo”
Kuna ujumbe gani uliosikia au kusoma kutoka mkutano mkuu wa hivi karibuni ambao unaweza kuhimili mafundisho katika sura hizi? Unapojifunza, takafari mahitaji ya washiriki wa darasa lako na andika misukumo ambayo unapokea.
Andika Misukumo Yako
Himiza Kushiriki
Njia mojawapo unaweza kuwahimiza washiriki wa darasa kujifunza maandiko kibinafsi na pamoja na famila zao ni kuwaalika kushiriki kila wiki jinsi mafunzo yao ya maandiko ni baraka katika maisha yao. Kwa mfano, jinsi gani mafunzo yao ya sura hizi yanaathiri uzoefu wao wa mkutano mkuu?
Fundisha Mafundisho
Ushuhuda wa Yesu Kristo unakuja kwa ufunuo.
-
Je, kuna mshiriki wa darasa yoyote aliyewahi kumwelezea mtu fulani jinsi wanavyojua kwamba injili ni kweli? Katika Mathayo 16:13–17, Mwokozi alifundisha nini kuhusu jinsi tunavyopokea ushuhuda? Mnaweza kushiriki jinsi Alma alivyopata ushuhuda wake (ona Alma 5:45–46) au Bwana alimfundisha nini Oliver Cowdery kuhusu ufunuo (ona M&M 6:14–15, 22–23; 8:2–3). Unafikiri ni nini Petro au Alma au Oliver Cowdery wangeweza kusema kama mtu fulani angewauliza jinsi wanavyojua kwamba injili ni kweli?
-
Kunaweza kuwa na watu katika darasa lako ambao wanaomba kwa ajili ya ufunuo binafsi lakini hawajui jinsi ya kuutambua wakati unapokuja. Mzee David A. Bednar alitumia matukio mawili ya kawaida ya mwanga kufundisha kuhusu jinsi tunavyopokea ufunuo; unaweza kutaka kushiriki umaizi wa Mzee Bednar pamoja na washiriki wa darasa (ona ”The Spirit of Revelation.” Ensign au Liahona, Mei 2011, 87–90; ona pia video “Patterns of Light: Spirit of Revelation” kwenye LDS.org). Ni mafundisho gani mengine au matukio darasa lako wanaweza kufikiria ambayo yatawasaidia watu wengine kutambua ufunuo binafsi? (Kwa mfano, ona 1 Wafalme 19:11–12; Wagalatia 5:22–23; Enoshi 1:1–8; M&M 8:2–3.)
Funguo za ukuhani ni muhimu kwa ajili ya wokovu wetu.
-
Kuanza majadiliano kuhusu funguo za ukuhani, ungeweza kuandika maswali kama yafuatayo ubaoni: Funguo za ukuhani ni nini? Funguo zinashikiliwa na nani? Funguo za ukuhani zinatolewaje? Unaweza pia kushiriki baadhi ya marejeo ya maandiko ambayo yanasaidia kujibu maswali haya, kama vile Mathayo 16:19; Mafundisho na Maagano 107:18–19; 128:8–11; 132:18–19, 59; Joseph Smith—Historia 1:72. Washiriki wa darasa wanaweza kupata msaada wa ziada kwa kurejea Kitabu cha Maelekezo 2: Kusimamia Kanisa (2010), 2.1.1; Ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Power in the Priesthood” (Ensign au Liahona, Nov. 2013, 92–95; au Kweli kwa Injili, 126–27. Waruhusu washiriki wa darasa muda wa kutafiti swali lao walilochagua. Kisha wanaweza kufundishana kile walichojifunza.
-
Majadiliano kuhusu Petro na Mitume wengine wakipokea funguo za ukuhani juu ya Mlima wa Kugeuka Sura yanaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuimarisha ushuhuda wao wa urejesho wa funguo za ukuhani katika siku za mwisho. Himiza majadiliano kama haya, ungeweza kutaka nusu ya darasa kujifunza Mathayo 17:1–9 (ona pia Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia) na nusu ingine kujifunza Mafundisho na Maagano 110. Wanaweza kisha kushiriki kile walichojifunza na kufahamu mifanano kati ya matukio hayo mawili. Video “Priesthood Keys: The Restoration of Priesthood Keys” (LDS.org) ingeweza pia kuwa na msaada.
-
Je, washiriki wa darasa lako wanaelewa jinsi funguo za ukuhani zinavyobariki maisha yao? Ili kuwasaidia, unaweza kuwaalika wachunguze Kitabu cha Maelekezo 2. 2.1.1, kwa orodha ya watu wanaoshikilia funguo. Watu hawa ni nani katika kata na kigingi chako? Labda ungeweza kuorodhesha majina yao ubaoni au waalike baadhi yao waje wazungumze na darasa. Wanatumiaje funguo za ukuhani walizopewa kuelekeza kazi ya ukuhani ndani ya miito yao? Tunabarikiwaje na huduma ya viongozi hawa wa ukuhani?
Tunapotafuta imani kuu, lazima kwanza tusimame imara kwenye imani tuliyokuwa nayo tayari.
-
Mzee Jeffrey R. Holland alitumia tukio la baba akitafuta uponyaji kwa ajili ya mwanawe kufundisha jinsi tunavyotakiwa kumkaribia Bwana tunapohisi kwamba imani yetu haitoshi (ona “Lord, I Believe.” Ensign au Liahona, Mei 2013, 93–95). Vipengele vitatu muhimu kutoka hotuba yake vimejumuishwa katika “Nyenzo za Ziada.” Labda unaweza kugawa darasa katika vikundi vinne na upangie kikundi kimoja kujadili Marko 9:14–30 na vile vikundi vingine kila kimoja kijadili mojawapo ya hoja tatu za Mzee Holland. Wanaweza kutafuta ujumbe katika tukio hili la maandiko ambalo linaweza kutusaidia kuzidisha imani yetu. Kila kikundi kinaweza kushiriki na darasa lote baadhi ya umaizi uliokuja kutoka majadiliano yao.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kujifunza nyumbani wiki hii, waambie kwamba muhtasari unaofuata katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unaweza kuwasaidia na familia zao kuwa na Pasaka yenye maana. Zaidi ya hayo, unaweza kupendekeza kwamba Jumapili ya Pasaka inaweza kuwa muda mzuri kwa ajili yao kuwaalika waumini wasioshiriki kikamilifu au marafiki wa imani nyingine kuja kanisani.
Nyenzo za Ziada
Urais saidizi unapokea mamlaka wakilishi.
“Vikundi vyote saidizi vya kata na kigingi vinatenda kazi chini ya maelekezo ya askofu au rais wa kigingi, anayeshikilia funguo za usimamizi. Marais wa vikundi saidizi na washauri wao hawapokei funguo. Wanapokea mamlaka wakilishi kufanya kazi katika miito yao” (Kitabu cha Maelekezo 2, 2.1.1).
Hoja tatu za kutusaidia kupata imani zaidi.
Baada ya kuwaambia tena tukio linalopatikana katika Marko 9:14–29, Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:
“Hoja nambari moja kulingana na tukio hili ni kwamba wakati anapokabiliana na changamoto ya imani, baba anaonyesha nguvu zake kwanza na ndipo anakubali upungufu wake. Tamko lake la mwanzo ni kukubali na bila kusita: ‘Bwana, Naamini.’ Ningesema kwa wote wanaotamani imani zaidi, mkumbukeni mtu huyu! Katika nyakati za hofu au wasiwasi au wakati wa matatizo, shikilia nafasi tayari umeshinda, hata kama nafasi yenyewe ni finyu. … Shikilia imara kwa kile unachojua tayari na simama kwa uthabiti mpaka uelewa wa ziada uje. … Kiwango cha imani yako au daraja ya elimu yako sio hoja—ni uadilifu unaonyesha kuelekea imani uliyonayo na kweli ambayo tayari unajua.
“Hoja ya pili ni tofauti na ya kwanza. Wakati matatizo yanakuja na maswali yanaibuka, usianze utafutaji wako wa imani kwa kusema kiasi gani ambacho huna , kukuongoza kama ilivyo kawaida katika ‘kutoamini’, … Sikuambii wewe ujisingizie imani usiyokuwa nayo. Mimi ninakuambia uwe mkweli kwa imani uliyonayo. … Kuwa muwazi kuhusu maswali yako kama unavyohitaji kuwa; maisha yamejaa hayo kwenye suala moja au mengine. Lakini kama wewe na familia mnataka kuponywa, msiruhusu hayo maswali kuzuia imani ikifanya miujiza yake. …
“Hoja ya mwisho: Wakati wasiwasi au ugumu unapokuja, usiogope kuomba msaada. Kama tunautaka kwa unyenyekevu na kwa uaminifu kama alivyofanya baba huyu, tunaweza kuupata. Kirai cha maandiko kama vile tamaa ya dhati kuwa ‘nia halisi’ iliyofuatiwa ‘na kusudi lililojaa la moyo, bila kuwa na unafiki na udanganyifu mbele ya Mungu’ [2 Nefi 31:13]. Ninashuhudia kwamba katika kujibu namna hiyo ya kusali sana, Mungu atatuma msaada kutoka pande zote mbili za pazia kuimarisha kuamini kwetu” (“Naamini.” Ensign au Liahona, Mei 2013, 93–94).