Njoo, Unifuate
Machi 25–31. Mathayo 14–15; Marko 6–7; Yohana 5–6: ‘Msiogope’


“Machi 25–31. Mathayo 14–15: Marko 6–7: Yohana 5–6 ‘Msiogope’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Machi 25–31 Mathayo 14–15; Marko 6–7; Yohana 5–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Kristo alisha umati

Walishe, na Jorge Cocco

Machi 25–31

Mathayo 14–15; Marko 6–7; Yohana 5–6

“Msiogope”

Unapojiandaa kufundisha kutoka Mathayo 14–15; Marko 6–7; na Yohana 5–6, tafuta jumbe ambazo zinahusika na darasa lako. Unapofanya hivyo, fikiria jinsi ya kuwaunganisha washiriki wa darasa katika uzoefu wenye maana na maandiko.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Njia mojawapo ya kuanza majadiliano ya sura hizi ni kuwaalika washiriki wa darasa wachache kila mmoja kuchagua sura kutoka kwenye somo na kuja amejiandaa kushiriki kifungu kutoka sura ile ambayo ilikuwa yenye maana kwao. Wanaposhiriki, washiriki wengine wa darasa wanaweza kuuliza maswali au kuongeza umaizi.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Yohana 5:16–47

Yesu Kristo ni Mwana Mpendwa wa Baba wa Mbinguni.

  • Katika Yohana 5, Yesu alitoa umaizi kadha kuhusu Yeye Mwenyewe, Baba Yake, na uhusiano Wake kwa Baba. Ili kusaidia darasa kugundua umaizi huu, jaribu kuwagawa katika vikundi na uwape dakika chache kuorodhesha kweli nyingi kadiri wawezavyo kuzipata katika aya 16–47 kuhusu silika ya Mungu, Yesu Kristo, na uhusiano Wao. Alika vikundi kuchukua zamu kusoma kweli kutoka orodha zao mpaka kila kweli katika kila orodha imeshirikiwa. Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinatusaidia kumwelewa vyema Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe? Tunaweza kufuata mfano wa Yesu Kristo wa utii kwa Baba?

  • Shughuli katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia huwaalika wanafunzi kuandika kila wakati Yesu alipotumia neno Baba katika Yohana 5. Waalike wanafunzi wachache kushiriki kile walichojifunza walipokamilisha shughuli. Ni umaizi gani walioupata kuhusu Baba wa Mbinguni na Mwanawe Mpendwa? Injili ya urejesho inafundisha nini ambacho kinatusaidia kuelewa vyema Baba yetu ni nani na kwa nini tunamwabudu? Baadhi ya mawazo yanaweza kupatikana katika ingizo la Kamusi ya Biblia la “Mungu” na katika ingizo la ”Mungu Baba” katika Kweli kwa Injili, 74–76. Kama sehemu ya majadiliano haya, mnaweza kuimba, au kusikiliza, au kusoma “O My Father,” Nyimbo, na. 292, kama darasa.

Mathayo 2:16–21; Marko 6:33–44; Yohana 6:5–14

Mwokozi anaweza kutukuza matoleo yetu kukamilisha azma Yake.

  • Nini kinaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata maana binafsi katika miujiza ya Yesu akiwalisha wale elfu tano? Unaweza kuuliza jinsi gani kusoma kuhusu miujiza kunaongeza imani yao katika uwezo wa Mwokozi kuwabariki binafsi. Wamewahi hata kuhisi kwamba uwezo wao au vipaji havikutosha kukamilisha lengo au amri kutoka kwa Mungu? Wamewahi hata kuhisi kwamba Mwokozi alitukuza au kuzidisha juhudi zao kuwasaidia kukamilisha kitu fulani ambacho kilionekana hakiwezekani?

    mikate na samaki.

    Yesu aliwalisha watu 5000 kimiujiza kwa mikate mitano na samaki wawili.

  • Video “Tha Feeding of the 5,000” (LDS.org) inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari muujiza ulioelezwa katika vifungu hivi. Je, ni utondoti gani tunaweza kupata katika tukio hili ambao unaweza kuongeza imani yetu katika Mwokozi? Je, ni kwa njia zipi Mwokozi anaweza kutulisha kiroho? Je, ni wakati gani tumelishwa na kuhimiliwa na Yesu Kristo? Kwa mfano wa muujiza katika siku hizi ambao ni sawasawa na muujiza wa mikate na samaki, ona video “Pure and Simple Faith” (LDS.org) au Paul VanDenBerghe, “Power in Prayer.” New Era, Julai 2012, 34–36.

Mathayo 14:22–33

Yesu Kristo anatualika tuweke kando hofu zetu na wasiwasi ili kwamba tuweze kusogea kikamilifu Kwake.

  • Tukio katika Mathayo 14:22–23 linaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuongeza imani yao katika Mwokozi na hamu yao ya kumfuata. Waalike washiriki wa darasa kusoma tukio hili, wakitoa usikivu makini wa kipekee kwa maneno yaliyosemwa na Kristo, Petro, na Mitume wengine. Ni kwa jinsi gani maneno ya Yesu yangeliweza kumsaidia Petro kuwa na imani na kuacha mashua na kutembea juu ya maji? Ni kwa jinsi gani onyo la Yesu la “furahini” na “msiogope” (aya 27) linatumika kwetu leo? Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa Petro kuhusu kile inamaanisha kuwa mfuasi wa Yesu Kristo na kumwamini Yeye?

  • Mathayo 14:22–33 ina maneno na virai ambavyo vingeweza kuwaongoza washiriki wa darasa kufanya imani kubwa katika Mwokozi. Waombe wapekue maneno ya kutia moyo kama hayo na virai, waandike ubaoni, na kujadili kile walichoandika. Washiriki wa darasa wanaweza kujihusisha na uzoefu wa Petro? Unaweza kuwahimiza kufikiria kuhusu na kushiriki uzoefu ambao wao, kama Petro, walichukua hatua kumfuata Mwokozi, hata wakati matokeo yalikuwa hayana uhakika. Walijifunza nini kutokana na uzoefu huo? Ni kwa jinsi gani Yesu amekuja kuwaokoa katika wakati wao wa hofu au wasiwasi?

Yohana 6:22–71

Kama wafuasi wa Kristo, lazima tuwe tayari kuamini na kukubali ukweli hata wakati ni vigumu kufanya hivyo.

  • Matukio katika Yohana 6 yanaweza kutoa taswira ya usaidizi wakati watu wanapohoji mafundisho, historia, au sera za Kanisa la Kristo. Katika sura hii, baadhi ya wafuasi wa Kristo walikataa kukubali mafundisho Yake kwamba Alikuwa mkate wa uzima na kwamba wangeweza kuokolewa tu kupitia dhabihu Yake ya nyama na damu. Kuwasaidia washiriki wako wa darasa kutumia maelezo haya kwenye maisha yao, unaweza kuandika maswali kama yafuatayo ubaoni na uwaombe washiriki wa darasa kutafuta majibu katika aya 22–71: Nini yalikuwa matarajio ya watu? (ona aya 26). Kristo aliwapa nini badala yake? (ona aya 51). Watu hawakuelewa nini? (ona aya 41–42, 52). Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kuchagua kutembea na Kristo hata wakati tunapokuwa na maswali? Waalike watafakari swali la Mwokozi na jibu la Petro katika aya 67–69. Ni yapi baadhi ya mafundisho, ibada, au “maneno ya uzima wa milele “ mengine ambayo yanaweza kupatikana tu katika Kanisa la urejesho la Kristo? Waalike washiriki wa darasa kushiriki jinsi mafundisho na ibada zilivyowabariki wao na familia zao. Kwa umaizi kutoka Mitume wa kisasa, mwalike mshiriki wa darasa kusoma kauli ya Mzee M. Russell Ballard katika “Nyenzo za Ziada.”

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Washiriki wa darasa wanaweza kuhisi kutiwa moyo kusoma vifungu kwa darasa la wiki ijayo kama utatoa angalizo kwamba matukio wanayosoma kuyahusu yanaweza kutajirisha uzoefu wao wa kusikiliza mkutano mkuu. Wahimize kuja kwenye darasa lijalo tayari kushiriki umaizi wao.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mathayo 14–15; Marko 6–7; Yohana 5–6

“Je, ninyi nanyi mwataka kuondoka?

Baada ya kunukuu Yohana 6:68–69, Mzee M. Russell Ballard alifundisha:

“Kwa wengine, mwaliko wa Kristo wa kuamini na kubaki unaendelea kuwa mgumu—au vigumu kuukubali. Wanafunzi wengine wanapata shida kuelewa sera mahususi za Kanisa au mafundisho. Wengine hupata wasiwasi katika historia yetu au katika udhaifu wa baadhi ya waumini na viongozi, wa zamani na sasa. Bado wengine wanaona vigumu kuishi dini ambayo inahitaji zaidi. Mwisho, wengine wamekuwa ‘wachovu kufanya mema’ [M&M 64:33]. Kwa sababu hizi na zingine, baadhi ya waumini wa Kanisa huyumba katika imani zao, wakishangaa kama wanapaswa kuwafuata wale “waliorudi nyuma, wasiandamane tena” na Yesu.

“Kama kuna mmoja wenu anayegugumia katika imani yake, ninawauliza swali kama alilouliza Petro: ‘Mtakwenda kwa nani ninyi?’ …

“… Kabla hujafanya uchaguzi huo wenye hatari kiroho wa kuondoka, ninakuhimiza kuacha na ufikirie kwa makini kabla ya kukiacha kile kilichokuleta kwenye ushuhuda wako wa Kanisa la Yesu Kristo la urejesho hapo mwanzoni. Tua na ufikirie kuhusu ulivyohisi hapa na kwa nini ulihisi hivyo. Fikiria kuhusu wakati ambao Roho Mtakatifu ametoa ushahidi kwako wa ukweli wa milele” (“Twende kwa nani?” Ensign au Liahona, Nov. 2016, 90–91).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Sikiliza. Kusikiliza ni kitendo cha upendo. … Muombe Baba wa Mbinguni akusaidie kuelewa kile washiriki wa darasa lako wanasema. Unapotoa usikivu wa makini kwa jumbe zao zilizosemwa na zisizosemwa, utakuja kuelewa vyema mahitaji yao, mashaka yao, na matamanio yao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 34).