Njoo, Unifuate
Machi 11–17. Mathayo 10–12; Marko 2; Luka 7; 11: ‘Hawa Kumi na Wawili Yesu Aliwatuma’


“Machi 11–17. Mathayo 10–12; Marko 2; Luka 7; 11: ‘Hawa Kumi na Wawili Yesu Aliwatuma’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Machi 11–17. Mathayo 10–12; Marko 2; Luka 7; 11 Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Yesu akimtawaza Petro

Machi 11–17

Mathayo 10–12; Marko 2; Luka 711

“Hawa Kumi na Wawili Yesu Aliwatuma”

Kusoma Mathayo 10-12; Marko 2; na Luka 711 ukiwa unawafikiria wanafunzi wako kutakusaidia kupokea mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu kuhusu nini wanahitaji. Andika misukumo ya kiroho unayopata, na usome muhtasari huu kutafuta umaizi wa ziada na mawazo ya kufundishia.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Waalike washiriki wa darasa wachache kuja wamejiandaa kushiriki maswali yoyote waliyokuwa nayo kuhusu Mathayo 11:28–30. (Kwa baadhi ya mifano ya maswali, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.) Majibu gani walipata?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 10

Bwana anawapa watumishi Wake uwezo wa kufanya kazi Yake.

  • Agizo la Mwokozi kwa Mitume Wake linaweza kutusaidia katika wajibu wetu binafsi. Washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa wamepata umaizi katika mada hii kupitia mafunzo yao binafsi; kwa mfano, kuna shughuli kwenye mada hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waalike wao washiriki kile walichojifunza au wafanye kazi katika vikundi vidogo kukamilisha shughuli katika darasa. Waalike washiriki wa darasa kushiriki uzoefu wakati walipohisi uwezo wa Mwokozi walipotimiza miito yao.

  • Njia nyingine kwa washiriki wa darasa kurejea Mathayo 10 ni kupekua sura hii kwa kitu fulani Mwokozi aliwaomba Mitume kufanya na wachore picha kuwakilisha kitu hicho. Wanaweza kushiriki michoro yao na kile walijifunza kuhusu agizo la Mitume Kumi na Wawili.

  • Ni kwa jinsi gani kujifunza agizo Kristo alilowapa Mitume Wake katika Mathayo 10 kunawasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa wajibu wa manabii na mitume wa kisasa? Inaweza kuwa msaada kufananisha agizo la Mwokozi kwa wale Kumi na Wawili na agizo linalotolewa kwa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili ya kwanza katika kipindi hiki, linalopatikana katika “Nyenzo za Ziada.” Ni kwa jinsi gani washiriki wa darasa wameshawishika na huduma ya Mitume wanaoishi? Toa ushuhuda wako wa wito mtukufu wa manabii na mitume wanaoishi, na waalike washiriki wa darasa watoe wao.

  • Kueleza kwa mfano ukweli kwamba kila mwenye ukuhani anaweza kufuatilia mamlaka yake nyuma mpaka wakati Yesu alipowatawaza Mitume Wake, mwalike mmoja mwenye ukuhani kushiriki mstari wake wa mamlaka.

Picha
Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

Mitume Kumi na Wawili wanafanya kazi ya Bwana leo.

Mathayo 10:17–20

Tunapokuwa katika huduma ya Bwana, atatupa mwongozo na maneno ya kusema.

  • Watu wakati mwingine wanahisi woga wanapofundisha au kuzungumza na wengine kuhusu injili. Lakini Bwana aliwaahidi wafuasi kwamba angewasaidia kujua nini cha kusema. Tunahitaji kufanya nini kupokea msaada Bwana alioahidi kwa ajili yetu? Waalike washiriki wa darasa kusoma Mathayo 10:19–20; Mafundisho na Maagano 84:85; na Mafundisho na Maagano 100:5–8 kupata majibu ya swali hili. Ni wakati gani Roho Mtakatifu alikusaidia kujua nini cha kusema? Unaweza kushiriki uzoefu wako na uwaalike washiriki wa darasa kushiriki uzoefu wao.

Mathayo 12:1–13; Marko 2:23–28

Sabato ni siku ya kufanya mambo mazuri.

  • Ili kusaidia kuishika siku ya Sabato kitakatifu, Mafarisayo walitekeleza sheria kali na desturi za binadamu, ambazo hatimaye ilitia giza uelewa wao wa kusudi la kweli la Sabato. Je, wale unaowafundisha wanaweza kufaidika kutokana na majadiliano ya kwa nini Bwana alitupa siku ya Sabato? Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kurejea maelezo katika Mathayo 12:1–13 na Marko 2:23–28 na kushiriki kile Mwokozi alifundisha kuhusu siku ya Sabato (ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, Marko 2:26–27 [katika kiambatisho cha Biblia). Ni umaizi gani wa ziada kuhusu Sabato tunaoupata katika Kutoka 31:16–17; Isaya 58:13–14; na Mafundisho na Maagano 59:9–13? Ni desturi au sheria gani zinaweza kutuvuruga kutoka kwa kusudi halisi la Sabato?

  • Wakati Mafarisayo walisisitiza sheria nyingi za kila kitu kuhusu Sabato, Mwokozi alifundisha kanuni rahisi: “Ni halali kutenda mema siku ya Sabato” (Mathayo 12:12). Wale wanaoishi kwa kanuni hii mara nyingi wanayo matatizo madogo kuishika siku ya Sabato kwa utakatifu. Ni kanuni gani zingine zinazowasaidia washiriki wa darasa kuishika siku ya Sabato kwa utakatifu? Kwa nini kufundisha kanuni kunafaa zaidi kuliko kuweka sheria katika kukuza kujitegemea kiroho? (ona kauli ya Nabii Joseph Smith katika “Nyenzo za Ziada”). Je, kuna kanuni zingine tunazoweza kufikiria ambazo zitatusaidia kutii amri za Mungu? Kwa mfano, kanuni gani ingeweza kuwasaidia wazazi kuwatia moyo watoto wao kutii neno la hekima au kufanya utafiti wa historia ya familia?

  • Ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “The Sabbath Is a Delight” (Ensign au Liahona, Mei 2015, 129–32) na video pamoja na ushauri wa Mzee Jeffrey R. Holland katika “Nyenzo za Ziada” vinaweza kuongezwa kwenye majadiliano kuhusu siku ya Sabato.

  • Inaweza kuwa msaada kwa washiriki wa darasa kurejea “Kuadhimisha Siku ya Sabato” katika Kwa Nguvu ya Vijana. Wanaweza kuigiza jinsi wanavyoweza kuelezea kwa mtu fulani ambaye sio wa imani yetu kwa nini wanaishika siku ya Sabato kwa utakatifu.

Luka 7:36–50

Tunaposamehewa dhambi zetu, upendo wetu kwa Mwokozi unazidi.

  • Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa mwanamke na mafundisho ya Mwokozi katika Luka 7:36–50 tunapotafuta msamaha wa dhambi zetu? Ni kwa jinsi gani toba inaimarisha mahusiano yetu na Kristo? Tungewezaje kutumia tukio hili kumfundisha mtu fulani kile inamaanisha kutafuta msamaha?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Unaweza kuwapa changamoto washiriki wa darasa kusoma miujiza katika Mathayo 13 na Luka 813 na kujiandaa kushiriki katika darasa la wiki ijayo umaizi wa kanuni za injili walizopata kutoka kwa mojawapo ya miujiza.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mathayo 10–12; Marko 2; Luka 711

Baraka za kuadhimisha siku ya Sabato.

Katika mfululizo wa video tatu, Mzee Jeffrey R. Holland anafundisha kuhusu baraka za kuadhimisha siku ya Sabato: “Siku Yangu Takatifu—Kumkaribia Mungu,” “Siku Yangu Takatifu—Kuheshimu Sabato,” na “Siku Yangu Takatifu—Mapumziko na Urejesho Mpya” (LDS.org).

Agizo kwa Mitume wa siku za mwisho.

Wakati baadhi ya washiriki wa kwanza wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili katika kipindi hiki walipoitwa, Oliver Cowdery aliwapa agizo sawa na lile Yesu Kristo alilotoa katika Mathayo 10. Alisema:

“Mtatakiwa kupambana na maoni ya mataifa yote. … Kwa hiyo, ninawaonya mjenge unyenyekevu mkubwa, kwani najua kiburi cha moyo wa binadamu. Angalieni, ili msije kuinuliwa juu na wajipendekezao wa ulimwengu. Angalieni ili kupenda kwenu kusivutiwe na vitu vya kidunia. Wacheni huduma yenu iwe ya kwanza, … [Ni] muhimu kwamba mnapokea ushuhuda kutoka Mbinguni kwa ajili yenu wenyewe, ili kwamba muweze kuwa na ushuhuda kwa ukweli. …

“‘… Mnatakiwa kupeleka ujumbe huu kwa wale wanaojifikiria wenyewe kuwa wenye busara. Na kwa hiyo wanaoweza kuwatesa; wanaweza kutafuta uzima wenu. Adui siku zote ametaka uzima wa watumishi wa Mungu. Nyinyi, kwa hiyo, mjiandae wakati wote kufanya dhabihu ya uzima wenu, ikiwa Mungu atauhitaji katika uendelezi na ujenzi wa kusudi Lake. …

“Kisha aliwachukuwa mmoja mmoja kwa mkono na alisema, ‘Kwa azma yako yote ya moyo kushiriki huduma hii, kuitangaza injili kwa bidii yako yote pamoja na ndugu hawa, kulingana na utaratibu na nia ya madaraka uliyoyapokea?’ Kila mmoja wapo alijibu kwa kukubali” (katika Joseph Smith Papers, Nyaraka, Juzuu 4: Aprili 1834–Septemba 1835, ed. Matthew C. Godfrey na wengine [2016], 243–44, 247; tahajia na kutenga maneno kumesanifiwa).

Kufundisha kanuni sahihi.

Mtu fulani alimwuliza Nabii Joseph Smith jinsi alivyoweza kuwatawala watu wengi vile katika Nauvoo kwa ufanisi. Nabii akaeleza, “Ninawafundisha kanuni sahihi, na wanajitawala wenyewe” (ona Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Joseph Smith [2007], 284).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Baraka zilizoahidiwa. Unapotoa mialiko ya kutenda, shuhudia kwa mwanafunzi wako kwamba watapokea baraka Mungu alizoahidi wanapotenda kwa imani juu ya mafundisho Yake. Baraka zisiwe msingi wetu wa motisha kwa utii, bali Baba wa Mbinguni anataka sana kuwabariki watoto Wake wote. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 35.)

Chapisha