Njoo, Unifuate
Machi 18–24 Mathayo 13; Luka 8; 13: ‘Mwenye Masikio Asikie’


“Machi 18–24 Mathayo 13; Luka 8:13: ‘Mwenye Masikio Asikie’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Machi 18–24. Mathayo 13; Luka 8; 13” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili; 2019

Picha
ngano tayari kwa kuvunwa

Machi 18–24

Mathayo 13; Luka 813

“Mwenye Masikio Asikie”

Unaposoma, fikiria maswali washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa nayo wanapojaribu kuelewa ujumbe wa mafumbo. Nini kinaweza kuwa kigumu kuelewa? Kujifunza kwako kunawezaje kukuandaa kujibu maswali yao?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Rejea pamoja na darasa “Mawazo ya Kuendeleza Kujifunza Maandiko Kwako Binafsi” katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waalike washiriki wa darasa kushiriki njia walizotumia kujifunza Mathayo 13 na Luka 813

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 13:1–23

Mioyo yetu lazima itaandaliwe kupokea neno la Mungu.

  • Ili kuwasaidia wale unaowafundisha kupata taswira ya jumbe za fumbo la mpanzi, unaweza kuleta mbegu kiasi, chungu cha udongo, na chungu cha mawe madogo madogo darasani. Mwombe mshiriki wa darasa apande mbegu moja katika udongo na moja katika mawe. Mbegu gani itakua vizuri, na kwa nini? Ni kwa jinsi gani hili somo la vielezo linahusiana na fumbo katika Mathayo13:1–23? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuiandaa mioyo yetu kupokea neno la Mungu?

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia fumbo la mpanzi kuwatia moyo washiriki wa darasa lako kuandaa mioyo yao kupokea neno la Mungu? Unaweza kuandika Wafuasi na Wengine ubaoni. Waalike washiriki wa darasa kusoma Mathayo 13:10–17 na kutafuta jinsi Mwokozi alivyoelezea tofauti kati ya wafuasi Wake na wengine waliosikia mafumbo Yake. Kisha waombe washiriki wa darasa wapekue aya 18–23, wakitafuta nini kinaweza kusababisha masikio yetu kuwa “mazito kusikia” au macho yetu kufunga kwa vitu vya kiroho. Mwelekeo gani tunaoupokea katika siku zetu kutoka kwa Mungu na watumishi Wake? Ni kwa njia gani tunalima “ardhi mzuri”? (aya 23).

  • Unaweza kuwaalika washiriki wachache wa darasa kila mmoja aje amejiandaa kufundisha kifungu kutoka kwenye ujumbe wa Mzee Dallin H. Oaks “Fumbo la Mpanzi” (Ensign au Liahona, Mei 2015, 32–35). Ni nini ujumbe huu unaongeza kwa uelewa wetu wa fumbo?

Mathayo 13:24–35, 44–53

Mafumbo ya Yesu yanatusaidia kuelewa ukuaji, majaliwa, na thamani ya Kanisa Lake.

  • Utawasaidia vipi washiriki wa darasa lako kuelewa kweli kuhusu Kanisa ambazo zilifundishwa katika mafumbo ya Yesu katika Mathayo 13? Unaweza kuorodhesha mafumbo machache ubaoni (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia na Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith, 293–303). Omba vikundi vidogo vya washiriki wa darasa kujifunza kila fumbo na kutafuta kile wanajifunza kuhusu ukuaji na majaliwa ya Kanisa. Njia moja ya kukusanya mawazo yote kutoka kila kikundi ni kuchora duara kubwa ubaoni na kuweka kitambulisho Kanisa la Kristo (“ufalme wa mbinguni”). Wakati kila kikundi kinaposhiriki wanaweza kuandika kitu fulani ndani ya duara ambacho walijifunza kuhusu ukuaji na majaliwa ya Kanisa.

    Picha
    mtu akivua kwa wavu

    Ufalme wa mbinguni ni kama wavu wa mvuvi.

  • Tunajifunza nini kuhusu thamani ya kustahili kuwa katika Kanisa kutoka kwa mafumbo ya hazina katika shamba na lulu ya thamani kuu, yanayopatikana katika Mathayo 13:44–46? Baadhi ya washiriki wa darasa lako (au watu wanaowajua) wamefanya dhabihu—iwe ni kubwa au ndogo—ili kuwa waumini wa Kanisa. Waalike washiriki wa darasa kushiriki dhabihu walizofanya au kuona wengine wakifanya ili wastahili kuwa katika Kanisa. Ni baraka gani zimekuja kama matokeo? Fikiria kushiriki hadithi ya Rais Gordon B. Hinckley kuhusu ofisa wa jeshi la majini katika “Nyenzo za Ziada.” Waalike washiriki wa darasa kutafakari nini wanahisi kushawishika kutoa dhabihu kwa ajili ya Kanisa.

Mathayo 13:24–30, 37–43

Hapo mwisho wa ulimwengu, Bwana atawakusanya wenye haki na kuwaangamiza waovu.

  • Ni kwa jinsi gani utaweza kusaidia darasa lako kujifunza masomo kutoka fumbo la ngano na magugu ambayo yatawasaidia kubaki Watakatifu wa Siku za Mwisho waaminifu? Anza kwa kumwalika mshiriki wa darasa kufupisha fumbo na ufafanuzi wake. Inaweza pia kuwa msaada kuonyesha picha ya ngano na magugu kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Ni yapi baadhi masomo katika fumbo hili ni kwa ajili ya siku zetu? Kwa nini ni muhimu kujua kwamba Bwana anaruhusu Watakatifu Wake “kukua pamoja” (Mathayo 13:30) na waovu mpaka muda wa mavuno? Tunawezaje kuimarisha imani yetu katika mazingira haya, wakati uovu umetuzunguka ? Mafundisho na Maagano 86 yanatoa umaizi wa ziada kwa matumizi ya fumbo hili kwa siku za mwisho.

  • Kauli ya Mzee L. Tom Perry katika “Nyenzo za Ziada” inapendekeza kwamba magugu yangewakilisha “uovu na njia za kidunia” ambazo zinapenyeza maishani mwetu. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari jinsi wanavyoweza kutambua aina hii ya gugu la kiroho, andika katika vipande vya karatasi kweli kadha za injili na uongo kadha, mawazo ya kiulimwengu au desturi. Weka vipande hivyo vya karatasi katika chombo. Kisha waombe washiriki wa darasa kuchagua chache na kujadili zipi ni kweli na zipi ni uongo. (Nyingi za kweli hizi na uongo zimetambuliwa katika hotuba za mkutano mkuu, unaweza kutafuta hapo kwa ajili ya mawazo.) Tunawezaje kufuata ushauri wa Mzee Perry “kurutubisha kile ambacho ni kizuri” katika maisha yetu?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Unaweza kusema kwamba somo la wiki ijayo linaelezea watu waliomfuata Yesu lakini kisha “wasiandamane naye tena” (Yohana 6:66). Waambie washiriki wa darasa wanaweza kupata umaizi unaoweza kuwasaidia wao na wengine kubaki na imani katika Mwokozi.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mathayo 13; Luka 813

“Ni kweli, au la?”

Rais Gordon B. Hinckley alishiriki uzoefu aliokuwa nao na ofisa wa jeshi la majini kutoka Asia ambaye alikuwa amejiunga na Kanisa hivi karibuni.

“Alitambulishwa kwangu tu kabla ya kurudi kwenye inchi yake ya asili. Tulizungumza juu ya [kweli za injili], na kisha nilisema: ‘Watu wako sio Wakristo. Nini kitatokea utakaporudi nyumbani Mkristo na, hasa Mkristo Mormoni?

‘Uso wake uliingiwa na hofu, na alijibu, ‘Familia yangu itasikitika. ‘Wanaweza kunifukuza na kunifikiria kama nimekufa. Na maisha yangu ya baadaye, na kazi yangu, fursa zangu zinaweza kufungwa dhidi yangu.’

“Nilimwuliza, uko tayari kulipa kiasi kikubwa cha gharama namna hiyo kwa ajili ya injili?.

“Macho yake meusi, yaliyoloweshwa na machozi, yalin’gara … alipojibu, ‘Ni kweli, au la?’

“Kwa aibu kwa kuuliza swali, nilijibu, ‘Ndio, ni kweli.’

“Ambapo alijibu, ‘Kisha nini kingine cha kujali?” Ni Kweli, Au La?” Ensign, Julai, 1993, 2)

Tunapaswa kurutubisha kilicho bora.

Mzee L. Tom Perry alifunza: “Yule adui wa mwanadamu amepata mbinu nyingi kadiri awezavyo kufikiria ili kutawanya magugu mbali. Amepata njia ya kuyafanya yapenyeze katika hata utakatifu wa nyumba zetu wenyewe. Njia za uovu na mambo ya kidunia yamesambaa huko na kuonekana kama hakuna njia ya kuyaondoa kabisa. Yanakuja kwa njia ya televisheni, redio na tovuti, vyombo ambavyo vimeanzishwa kwa lengo la kuelimisha na kutuburudisha. Ngano na magugu vyote vimekua kwa pamoja. Mtu atunzaye shamba lazima, kwa nguvu zake zote, lazima akirutubishe kilicho bora na kukifanya kiwe imara na cha kupendeza ili magugu yasiwe na mvuto kwa macho au masikio.’ (Kupata Amani Isiyo na Kikomo na Kujenga Familia za Milele.” Ensign au Liahona, Nov. 2014, 44).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Lenga ufundishaji wako katika mafundisho. Hakikisha majadiliano yako na darasa yanalenga kwenye mafundisho ya kimsingi katika maandiko. Unaweza kufanya hivi kwa kuwaomba wanafunzi wasome maandiko mapema, ukilenga majadiliano ya darasa kwenye maandiko, na kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki ushuhuda wao wa mafundisho ya kweli. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 20–21.)

Chapisha