Njoo, Unifuate
Machi 4–10. Mathayo 8–9; Marko 2–5: ‘Imani Yako Imekuponya’


“Machi 4–10 Mathayo 8–9; Marko 2–5: ‘Imani Yako Imekuponya’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shuie ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Machi 4–10 Mathayo 8–9; Marko 2–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Yesu akimponya mtu mlemavu

Kuponya katika Mabawa Yake, na John McNaughton

Machi 4–10.

Mathayo 8–9; Marko 2–5

“Imani Yako Imekuponya”

Maandalizi yako ya kufundisha yanaanza unapojifunza kwa maombi Mathayo 8–9 na Marko 2–5. Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia inaweza kuboresha kujifunza kwako na kuchochea mawazo ya kufundisha zaidi ya yale yaliyowasilishwa hapa.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya ushiriki

Himiza Kushiriki

Unaweza kuleta picha kadha zikionyesha matukio kutoka Mathayo 8–9 na Marko 2–5 (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, namba 4041, au LDS.org) au orodhesha matukio haya ubaoni. Waombe washiriki wa darasa kushiriki kile wanachojua kuhusu kila muujiza. Je, ni jumbe gani wanazoziona katika miujiza hii?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 8–9; Marko 25

Miujiza inatokea kulingana na mapenzi ya Mungu na imani yetu katika Yesu Kristo.

  • Washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa wamepata umaizi wenye nguvu wakati wa kujifunza binafsi juu ya miujiza katika sura hizi (ona orodha ya uponyaji katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki umaizi wao na mwenza au na darasa zima.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa uhusiano kati ya imani na miujiza, unaweza kusoma uponyaji wa kimiujiza mara kadha kutoka Mathayo 8–9 na Marko 25, wakitafuta imani ya mtu aliyeponywa au imani za wengine. (Kama huna muda wa kujadili miujiza yote, waombe washiriki wa darasa ni ipi ilikuwa ya maana sana kwao.) Baadhi ya miujiza hii ingeweza kuboresha majadiliano yenu: Mormoni 9:15–21; Etheri 12:12–16; Moroni 7:27–37; na Mafundisho na Maagano 35:8. Ni nini uponyaji wa Mwokozi na maandiko haya yanafundisha kuhusu imani na miujiza? Ona pia Kamusi ya Biblia, “Miujiza.”

  • Kunaweza kuwa na watu katika darasa lako ambao wana imani na wanatafuta muujiza, lakini muujiza haujatokea katika njia wanayotamani. Maandiko na viongozi wetu wa Kanisa wanafundisha nini kuhusu hili? Katika makala yenye kichwa “Accepting the Lord’s Will and Timing,” Mzee David A. Bednar alieleza kuhusu jinsi alivyowashauri wanandoa katika hali kama hii (Ensign, Aug, 2016, 31–35; pia ona 2 Wakorintho 12:7–10; M&M 42:43–52). Je, washiriki wa darasa wamewahi kuona baraka zikija katika maisha yao au maisha ya wengine wakati miujiza iliyotamaniwa haikutokea?

  • Wakati wa kusoma kuhusu miujiza katika Mathayo 8–9 na Marko 25, baadhi ya watu wanaweza kushangaa kama vitu kama hivi vinawezekana leo. Moroni alielezea siku yetu kama muda ambao “itasemekana kwamba miujiza imeondolewa,” lakini pia aliahidi kwamba Mungu bado ni Mungu wa miujiza, kwani Mungu ni “Kiumbe kisichobadilika” (Mormoni 8–26; 9:8–21; ona pia Moroni 7:27–29). Je, unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuongeza imani yao katika uwezo wa Mungu kubariki maisha yao? Unaweza kuwauliza kushiriki mifano ya miujiza waliyoishuhudia. Unaweza pia kufikiria kushiriki matukio ya miujiza kutoka historia ya Kanisa (ona “Nyenzo za Ziada”).

Picha
mwanamke akigusa pindo la vazi la Yesu

Mwamini Bwana, na Liz Lemon Swindle

Mathayo 8:23–27; Marko 4:35–41

Yesu Kristo ana uwezo wa kuleta amani katikati ya dhoruba za maisha.

  • Unaweza kufahamu baadhi ya changamoto washiriki wa darasa lako wanakabiliana nazo. Kwa sababu sisi wote tunakuwa na majaribu wakati fulani katika maisha yetu, kurejea matukio katika Marko 4:35–41 kunaweza kujenga imani ya washiriki wa darasa kwamba Mwokozi anaweza kuwaletea amani. Mpe kila mtu kipande cha karatasi, na waombe waandike kwenye upande mmoja wa karatasi majaribu walilopitia. Upande mwingine, waombe waandike kitu fulani kutoka Marko 4:35–41 kile kinachowavutia kumgeukia Mwokozi wakati wa majaribu. Wahimize washiriki wa darasa kushiriki kile walichoandika, ikiwa watahisi sawa kufanya hivyo.

  • Wimbo “Master, the Tempest Is Raging,” Nyimbo, na. 105, msingi wake ni hadithi katika Mathayo 8:23–27 na Marko 4:35–41. Labda washiriki wa darasa wanaweza kutafuta maneno katika wimbo ambayo yanahusiana na virai katika maandiko. Unaweza pia kuonyesha picha inayoonyesha mandhari (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 40) na jadili ni muda gani msanii anauonesha. Ni njia gani zingine unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa maana na uwezo wa muujiza huu?

Marko 2:1–12

Kuwaokoa wale ambao wamepotea kunahitaji kuunganisha juhudi zetu.

  • Matukio ya muujiza huu yanafundisha faida ya kufanya kazi pamoja kwa umoja kumsaidia Mwokozi katika kuwaokoa wale wenye mahitaji ya kiroho na kimwili. Ujumbe wa Mzee Chi Hong (Sam) Wong “Okoa Katika Umoja” (Ensign au Liahona, Nov. 2014, 14–16) unaweza kuongezwa kwenye majadiliano kuhusu ukweli huu. Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kuja wakiwa wamejiandaa kurejea matukio kutoka katika maandiko na kisha kushiriki kile Mzee Wong alifundisha. Tunajifunza nini kutoka Marko 2:1–12 kuhusu faida ya kufanya kazi pamoja kuwaokoa wenye mahitaji? (ona pia Marko 3:24–25).

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma Mathayo 10–12; Marko 2; na Luka 711 wakati wa wiki ijayo, waambie kwamba wataona katika sura hizi baadhi ya ushauri ambao unaweza kuwasaidia kutekeleza wito wao na wajibu katika Kanisa.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mathayo 8–9; Marko 2–5

Nabii Joseph Smith aliwaponya wagonjwa.

Mnamo Julai 1839 idadi kubwa ya Watakatifu walikuwa wamefukuzwa kutoka Missouri walikuwa wanaishi katika magari ya kukokotwa, katika mahema, na aridhini karibu na Commerce, Illinois. Wengi walikuwa wagonjwa sana, na Joseph na Emma Smith walikuwa wamechoka kabisa kwa kujaribu kuwasaidia. Wilford Woodruff alieleza kile kilitokea Julai 22: “Ilikuwa siku ya nguvu za Mungu. Kulikuwa na wagonjwa wengi miongoni mwa Watakatifu sehemu zote mbili za Mto [Mississippi, na Joseph alikwenda akipita katikati yao, akiwainua kwa mikono na katika sauti kubwa kuwaamuru katika jina la Yesu Kristo kuinuka kutoka vitandani mwao na wafanywe wazima, na waliruka kutoka kwenye vitanda vyao wamefanywa wazima kwa nguvu za Mungu. … Ilikuwa kwa kweli wakati wa kushangilia” (Wilford Woodruff, Shajara, Julai 22, 1839 Maktaba ya Historia ya Kanisa).

Mzee Franklin D. Richards alituliza dhoruba.

Mzee LeGrand Richards, mshiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alisimulia tukio kutoka maisha ya babu yake, Mzee Franklin D. Richards, ambaye mwaka wa 1848 alikuwa kiongozi wa kikundi cha Watakatifu wa Kiingereza waliokuwa wanavuka Bahari ya Atlantiki kwenda Marekani: “Mashua ambayo [Mzee Richards] aliyokuwa ameabiri ilikuwa katika hatari kubwa [kutokana na dhoruba kali], kiasi kwamba nahodha wa mashua alimwendea na kumsihi atoe sala ya kuomba kwa Bwana kwa niaba ya mashua na abiria wake; na Babu, akikumbuka kwamba ameahidiwa kwamba atakuwa na uwezo juu ya vitu vya asili, alitoka juu ya sitaha ya mashua na kuinua mikono yake juu mbinguni na akakemea bahari na mawimbi, na mara moja yalitulia” (katika Taarifa ya Mkutano Mkuu, Apr. 1941, 84).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa ushuhuda kila mara. Ushuhuda wako rahisi, wa dhati kuhusu kweli za kiroho unaweza kuwa na ushawishi wenye nguvu kwa wale unaowafundisha. Ushahidi wako hauhitaji kuwa wa ufasaha au mrefu. Unaweza, kwa mfano, kuwa ushuhuda rahisi wa muujiza wa kuwa na injili katika maisha yako.

Chapisha