Njoo, Unifuate
Aprili 6–12 Luka 12–17:Yohana 11: ‘Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea’


Aprili 6–12. Luka 12–17: Yohana 11: Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea ’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

Aprili 6–12. Luka 12–17; Yohana 11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
mtu akimkumbatia mwanawe

Mwana Mpotevu, na Liz Lemon Swindle

Aprili 6–12

Luka 12–17; Yohana 11

“Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea”

Anza maandalizi yako kwa kujifunza kwa maombi Luka 12–17 na Yohana 11 “Kondoo gani aliyepotea” katika darasa lako anayekuja akilini mwako? Tumia Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na muhtasari huu unapotafuta mwongozo wa Bwana juu ya njia bora ya kukidhi mahitaji ya washiriki wa darasa hata kama hawahudhurii darasa.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Matumizi ni sehemu muhimu ya kijifunza, kwa hiyo waalike washiriki wa darasa kushiriki jinsi wanavyochagua kuishi jambo fulani walilojifunza kutoka katika maandiko wiki hii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Luka 14:15–24

Hakuna sababu inayotosha kwa kuikataa injili.

  • Kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza fumbo la karamu kuu, unaweza kuwaalika kwenye sherehe ya kubuni ambayo utakuwa mwenyeji. Waruhusu washiriki baadhi ya sababu kwa nini watahudhuria au hawatahudhuria. Someni Luka 14:15–24 pamoja, na mjadili visingizio walivyovitoa watu katika fumbo walipoalikwa kwenye karamu ambayo iliwakilisha baraka za injili. Visingizio gani watu wanavitoa leo kwa kushindwa kukubali mialiko ya Mwokozi kupokea baraka za Baba wa Mbinguni? Labda washiriki wa darasa wanaweza kushiriki baraka walizozipokea wakati walipofanya dhabihu muhimu kuishi kanuni fulani za injili.

Luka 15

Tunaweza kuwatafuta wale waliopotea na kufurahi pamoja na Baba watakaporudi.

  • Unaweza kuwahimiza wale unaowafundisha kuwatafuta watu walio “potea” kwa sababu hawana baraka za injili na kuwaalika warudi? Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kufikiria kwa muda mfupi kuhusu “kondoo aliyepotea” wanayemjua na kisha kusoma Luka 15:1–7 wakiwa na mtu yule akilini. Wanahisi wamehimizwa kufanya nini kumfika mtu yule kwa usikivu na upendo? Hadithi ya Rais Thomas S. Monson katika “Nyenzo za Ziada” au hotuba ya Mzee Mervyn B. Arnold “To the Ruscue: We can Do it” (Ensign au Liahona, Mei 2016, 53–66) inaweza kusaidia kwenye majadiliano haya.

  • Je, inaweza kuwa ni msaada kwa washiriki wa darasa kuelewa njia ambazo mtu anaweza kupotea? Fikiria kupangia vikundi vya washiriki wa darasa mojawapo ya haya mafumbo matatu katika Luka 15 kujifunza. Mafumbo yanapendekeza nini kuhusu jinsi gani tunapaswa kujaribu kuwatafuta wale ambao wamepotea? Ni maneno gani katika Luka 15 yanaonyesha jinsi Baba wa Mbinguni anahisi kuhusu wale waliopotea”? Kuimba “Dear to the Heart of the Shepherd.” Nyimbo, na. 221 pamoja inaweza kuwa nyongeza ya maana kwenye mafundisho ya mafumbo haya.

  • Washiriki wako wa darasa wanaweza kunufaika kutokana na kulenga kwenye maneno na matendo ya kaka mkubwa katika fumbo la mwana mpotevu. Labda wanaweza kuandika hatima nyingine kwa fumbo ambapo msimamo wa kaka mkubwa kwa ndugu yake ni tofauti. Namna gani ushauri wa baba katika fumbo unatufundisha kuhusu jinsi tunatakiwa kuhisi kuhusu wale waliopotea na wale wanaorudi kwenye injili? (Ona pia kauli ya Mzee Jeffrey R. Holland katika “Nyenzo za Ziada.”) Au unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kufikiria kama wao ni baba katika fumbo hili. Ushauri gani wa ziada watakaompa kaka mkubwa kumsaidia kufurahia maendeleo au mafanikio ya wengine?

Yohana 11:1–46

Yesu Kristo ni Ufufuo na Uzima.

  • Walipokuwa wakisoma kuhusu kufufuliwa kwa Lazaro wiki hii, je, kuna yoyote katika washiriki wa darasa lako amepata chochote ambacho kimeimarisha imani yao kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na Masiya aliyeahidiwa? Waalike wanafunzi washiriki kile walichopata. Ni uzoefu gani mwingine umejenga imani yao katika Yesu Kristo? Kama utataka kutoa angalizo kwamba wakati wa muujiza huu, Lazaro hakufufuliwa bali alirudishwa kwenye maisha ya kufa.

    Picha
    Yesu akilia

    Yesu Alilia, na James Tissot

  • Njia moja ya kuchanganua Yohana 11:1–46 ni kuwauliza washiriki wa darasa kuchukua zamu kusoma aya na uwaalike kutua wanapopata ushahidi wa imani katika Yesu kristo. Waambie wajadili kile walichokipata. Majaribu na mateso huimarisha kwa jinsi gani imani yetu kwake Yeye?

  • Njia nyingine ya kusoma maelezo haya ni kuwapangia washiriki wachache wa darasa kufikiria uhusiano wa watu waliohusika—kama vile Mwokozi, Mitume, Martha, Mariamu, na Lazaro. Tunaweza kujifunza nini kutoka kila mmoja wao? Tunaweza kujifunza nini kuhusu Mwokozi kutoka Yohana 11:33–35? Kwa nini ni muhimu kujua kuhusu vitu hivi kumhusu Yeye?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18, unaweza kuwauliza swali kama “Jinsi gani ungehisi kama ungefanya kazi siku mzima na ukalipwa sawa na mtu fulani ambaye alifanya kazi kwa saa moja. Waambie kwamba kuna fumbo katika somo la wiki ijayo linalopendekeza jinsi hili linaweza kufikiria ni sawa.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Luka 12–17; Yohana 11

“Ulinipata mimi”

Rais Thomas S. Monson alishiriki uzoefu ufuatao alioupata akihudumu kama askofu: “Niligundua asubuhi ya Jumapili moja kwamba Richard, mmoja wa makuhani wetu aliyehudhuria mara chache, alikosekana tena kwenye mkutano wa ukuhani. Nilikabidhi akidi katika ulinzi wa mshauri na kutembelea nyumbani kwa Richard. Mama yake alisema kwamba alikuwa anafanya kazi katika banda la kutengenezea motokaa. Niliendesha gari hadi kwenye banda katika kumtafuta Richard na nikatafuta kila mahali lakini sikuweza kumpata. Ghafla, nilipata mwongozo wa kuangalia chini katika shimo zee la mafuta lililokuwa kando ya jengo. Kutoka kwenye giza niliweza kuona macho mawili yanayog’aa. Nilisikia Richard akisema, “Umenipata mimi, Askofu! Nitakuja juu.’ Mimi na Richard tulipokuwa tunazungumza, Nilimwambia jinsi sisi tulivyomkosa na tulivyomhitaji. Nilishawishi kujitolea kutoka kwake kuhudhuria mkutano huu. … [Baadaye], Richard alisema kwamba kipindi muhimu kwangu kilikuwa wakati askofu wake alimpata alipokuwa amejificha katika shimo la mafuta na kumsaidia kurudi kwenye utendaji” (“Sugar Beets and the Worth of a Soul.” Ensign, Julai 2009, 6–7).

Kujifunza kutoka mwana mpotevu mwingine.

Mzee Jeffrey R. Holland alitoa wazo kuhusu kaka mkubwa wa mwana mpotevu:

“Huyu kijana hakukasirika sana kwamba mwenzake amerudi nyumbani kama alivyokasirika kwamba wazazi wake wanafurahia hilo. Kujihisi kutothaminiwa na labda zaidi ya kujionea huruma kidogo, mwana huyu mchapakazi—na yeye ni mchapakazi wa ajabu mtiifu—anasahau kwa muda kwamba hajawahi kujua uchafu au kukata tamaa, hofu au kujichukia. Anasahau kwa muda kwamba kila ndama katika shamba la wanyama tayari ni wake na ndivyo ilivyo kwa majoho katika kabati na kila pete katika mtoto wa meza. Anasahau kwa muda kwamba uaminifu wake umekuwa na siku zote utatuzwa.

“Hapana, yeye ambaye kwa kweli ana kila kitu, na ambaye katika kufanya kazi kwake kwa bidii, njia ya ajabu amekipata, anakosa kitu kimoja kinachoweza kumfanya mtu kamili wa Bwana anayekaribia kuwa. Yeye bado hajawa na huruma, na rehema, upana wa fadhila wa kuona kwamba huyu sio mpinzani anayerudi. Ni ndugu yake. Kama baba yake alivyomsihi aone, ni yule aliyekufa na sasa yu hai. Ni yule aliyepotea na sasa amepatikana” (“ The Other Prodigal,” Ensign, Mei 2002, 63).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kumfikia yule mmoja. Kama vile mchungaji katika fumbo la Mwokozi (ona Luka 15:4), “Unaweza kuwafikia wale ambao wanakosekana darasani mwako. Nafasi zako kuwafundisha na kuwainua washiriki wa darasa na kuwasaidia kuja kwake Kristo zinaendelea nje ya darasa na zaidi ya wale wanaohudhuria masomo yako rasmi.” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 8).

Chapisha