Njoo, Unifuate
Mei 27–Juni 2. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; Luka 21: ‘Mwana wa Adamu Atakuja’


“Mei 27–Juni 2. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; Luka 21: ‘Mwana wa Adamu Atakuja’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Mei 27 –Juni 2. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; Luka 21” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili; 2019

Picha
Ujio wa Pili

Ujio wa Pili, na Harry Anderson

Mei 27–June 2

Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Marko 12–13; Luka 21

“Mwana wa Adamu Atakuja”

Kumbuka kuanza matayarisho yako ya kufundisha kwa kusoma kwa maombi Joseph—Smith 1; Mathayo 25; Marko 12–13; na Luka 21. Tafuta mwongozo wewe mwenyewe, na kisha urejee muhtasari huu kwa mawazo ya ziada.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Tengeneza orodha ya mafumbo ya Mwokozi ubaoni yaliyopatikana katika masomo ya wiki hii, kama vile mti wa mtini, mtu mzuri na mwizi na watumishi wazuri na waovu, mabikira kumi, talanta, na kondoo na mbuzi. Waombe washiriki wa darasa washiriki ukweli waliojifunza kutoka mafumbo haya ambayo yanaweza kuwasaidia kujitayarisha kwa Ujio wa Pili wa Bwana. Wanafanya nini kutumia ukweli huu katika maisha yao?

Picha
ikoni ya kufundishia.

Fundisha Mafundisho

Joseph Smith—Mathayo 1:21–37

Unabii kuhusu Ujio wa Pili wa Mwokozi unaweza kutusaidia kukabiliana na wakati ujao kwa imani.

  • Ishara za Ujio wa Pili zinaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya washiriki wa darasa kuzielewa. Inaweza kuwasaidia kufanya kazi kwa makundi na kuzitambua ishara wanazozipata katika Joseph Smith—Mathayo 1:21–37. Inaweza pia kuwasaidia kuelewa vyema umuhimu wa ishara hizi kama watazifananisha na alama za barabarani. Kwa nini alama za barabarani ni muhimu? Hii inapendekeza nini kuhusu ishara za Ujio wa Pili? Unaweza hata ukawapa kila kikundi vipande vya karatasi vyenye umbo la ishara za barabarani na kuwaalika waandike kila karatasi ishara ambayo itatangulia Ujio wa Pili. Waache washiriki kile walichopata, na alika darasa lijadili ushahidi wa ishara hizi ulimwenguni leo.

  • Katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, Washiriki wa darasa walitakiwa kutafuta ushauri katika aya hizi kuhusu jinsi tunaweza “kutosumbiliwa” wakati wa matukio kuelekea Ujio wa Pili (ona pia kauli ya Rais Thomas S. Monson katika “Nyenzo za Ziada”). Onyesha picha inayoonyesha Ujio wa Pili (ona Ujio wa Pili, Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 66), na waalike washiriki wa darasa kushiriki aya walizoziona katika mafunzo yao binafsi. Kwa nini ni baraka kujua kuhusu matokeo kuelekea kwenye Ujio wa Pili wa Mwokozi?

Joseph Smith—Mathayo 1:26–27, 38–55; Mathayo 25:1–13

Ni lazima daima tuwe tayari kwa Ujio wa Pili wa Mwokozi.

  • Hata ingawa Mwokozi ametuomba siku zote tuwe tayari kwa Ujio Wake wa Pili, ni rahisi kujishughulisha sana katika maisha ya kila siku na kutofikiri kuhusu hilo. Mafumbo katika Joseph Smith—Mathayo 1:26–27, 38–55 na Mathayo 25:1–13 yanaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutambua umuhimu wa kujitayarisha kwa Ujio wa Pili. Waalike washiriki wa darasa kutafuta mafumbo haya na milingano na kushiriki kile yanachofundisha kuhusu kujitayarisha kwa Ujio wa Pili. Labda mshiriki mmoja au wawili wa darasa wanaweza kuja kama wamejitayarisha na onyesho la ubunifu juu ya mafumbo haya.

  • Fumbo la mabikira kumi linaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari matayarisho yao ya kiroho kukutana na Mwokozi. Mzee David A. Bednar alitoa tafsiri moja ya fumbo ambayo inaweza kusaidia (ona “Nyenzo za Ziada”). Washiriki wa darasa wanaweza kujadili nini tunaweza kufanya katika maisha yetu ya kila siku ili kuwa tumeongoka kikamilifu katika injili. Kwa nini lazima kila mmoja wetu apitie uongofu kwa ajili yetu wenyewe? Ni nini Mafundisho na Maagano 45:56–57) yanaoongeza kwenye uelewa wetu wa fumbo hili?

  • Mnaweza kuimba pamoja nyimbo kuhusu Ujio wa Pili na kujadili jumbe zinazofundisha (ona “Nyenzo za Ziada”).

Mathayo 25:14–46

Kwenye Hukumu ya Mwisho, tutampa Bwana maelezo ya maisha yetu.

  • Fumbo la talanta na fumbo la kondoo na mbuzi yanaweza kututia moyo kufikiri kuhusu maelezo ya maisha yetu tutakayotoa kwa Bwana kwenye Hukumu ya Mwisho. Mnaweza kuyasoma mafumbo pamoja na kumtaka kila mshiriki wa darasa ashiriki swali moja Mwokozi anaweza kuuliza wakati tutakapotoa maelezo ya maisha yetu. Toa muda kwa washiriki wa darasa kupanga njia watakazofanya kwa misukumo waliyopokea wakati wa majadiliano.

    Picha
    kondoo na mbuzi

    Kristo aliwatumia kondoo na mbuzi kufundisha kuhusu Hukumu ya Mwisho (ona Mathayo 25:31–33).

  • Unaweza kutaka kurejea pamoja na washiriki wa darasa ufafanuzi wa Hukumu ya Mwisho unaopatikana katika Mwongozo wa Maandiko, “Judgment, The Last,” scriptures.lds.org. Kisha unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kurejea baadhi ya maandiko kuhusu namna Hukumu ya Mwisho itakavyokuwa, kama vile Alma 5:17–25. Ni nini maandiko haya yanatupa mwongozo kufanya ili kujiandaa kwa siku ile?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupata maana ya kibinafsi katika fumbo la talanta (ona Mathayo 25:14–30), shiriki baadhi ya mawazo au tumia shughuli kutoka “The Parable of the Talents,” na Mzee Ronald A. Rasband,(Ensign, Aug. 2003, 32–35).

  • Kutoa mwongozo kuhusu Mathayo 25:34-40, unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki mifano ya watu walioonyesha huruma iliyoelezwa katika aya hizi. Wape muda kutafakari nani anaweza kuhitaji huduma yao. Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kuwalisha wenye njaa, kuwavika walio uchi, na kuwatembelea wagonjwa?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma Yohana 13:17 wakati wa wiki ijayo, waombe wafikirie kuhusu nini watakachosema kwa mwana au binti kabla tu hajaondoka kwenda misheni. Katika Yohana 13–17, tutasoma maelekezo ya mwisho ambayo Mwokozi aliyowapa wafuasi wake kabla ya Kusulubiwa Kwake.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 25; Mark 12–13; Luka 21

Nyimbo kuhusu Ujio wa Pili.

Mafuta ya uongofu.

Mzee David A. Bednar alitoa ushauri wa uwezekano wa ufafanuzi wa fumbo hili la mabikira kumi:

Fikiria mafuta kuwa mafuta ya uongofu [ona Mathayo 25:4–9]. …

“Mabikira watano wenye busara walikuwa wachoyo na hawakuwa tayari kugawana, au walikuwa wanaonyesha kwa usahihi kwamba mafuta ya ongofu hayaweze kuazimwa? “Je, nguvu ya kiroho inayotokana na utiifu wa kila mara wa amri inaweza kupewa mtu mwingine?” Elimu iliyopatikana kupitia kujifunza kwa bidii na kutafakari maandiko inaweza kupelekwa kwa anayehitaji? Amani injili inayoleta kwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho mwaminifu inaweza kuhamishiwa kwa mtu anayepata shida na changamoto kubwa? Jibu la wazi kwa kila moja ya maswali haya ni la.

“Kama walivyosisitiza vizuri mabikira wenye busara, kila mmoja wetu lazima’ ajinunulie mwenyewe.’ Wanawake hawa wenye mwongozo hawakuwa wakielezea mapatano ya kibiashara, bali, walikuwa wanasisitiza wajibu wetu binafsi kuweka taa yetu ya ushuhuda ikiwaka na kupata muda wa kutosha kwa mafuta ya wongofu. Mafuta haya ya thamani yanapatikana tone moja kwa wakati—amri juu ya amri [na] kanuni juu ya kanuni’ (2 Nefi 28:30), kwa subira na kwa kushikilia” (“Converted unto the Lord,” Ensign au Liahona Nov. 2012, 109).

 Usiogope

Rais Thomas S. Monson alisema:

“Japokuwa mawingu ya dhoruba yatatanda, japokuwa mvua itatunyeshea, elimu yetu ya injili na upendo wa Baba yetu wa Mbinguni na wa Mwokozi utatufariji na kutuimarisha na kutuletea shangwe katika mioyo yetu tunapotembea wima na kushika amri. …

“Ndugu na dada zangu wapendwa, msiogope. Jipeni moyo. Siku za baadaye ni za furaha kama imani zenu” (“Be of Good Cheer,” Ensign au Liahona, Mei 2009 92).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Hakikisha kwamba unafundisha mafundisho ya kweli. “Kila mara jiulize, ‘Ni kwa jinsi gani kile ninachofundisha kitawasaidia washiriki wa darasa langu kujenga imani katika Kristo, kutubu, kufanya na kushika maagano ya Mungu, na kupokea Roho Mtakatifu?’” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 20).

Chapisha