“Juni 3–9. Yohana 13–17: ‘Kaeni Katika Pendo Langu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019.)
“Juni 3–9. Yohana 13–17 “ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019
Juni 3–9
Yohana 13–17
“Kaeni Katika Pendo Langu”
Wakati unapojifunza kwa maombi Yohana 13-17, tafakari jinsi unavyoweza kuonyesha vyema upendo kwa wale unaowafundisha. Roho Mtakatifu ataleta mawazo katika akili yako unapojifunza maandiko, Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, na muhtasari huu.
Andika Misukumo Yako
Himiza Kushiriki
Andika nambari 13 mpaka 17 ubaoni, zikiwakilisha sura katika Yohana ambazo washiriki wa darasa walizisoma wiki hii. Waalike washiriki wachache wa darasa kuandika, karibu na kila nambari ya sura, marejeo kwa aya wanayopata kuwa yana maana na wangependa kuijadili kama darasa.
Fundisha Mafundisho
Mwokozi ni mfano wetu wa kuhudumia wengine kwa unyenyekevu.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kutafakari umuhimu wa Yesu akiwaosha miguu wanafunzi wake, unaweza kumwita mshiriki wa darasa mbeleni kuigiza wajibu wa Petro katika maelezo haya na kusailiwa na washiriki wa darasa wengine. Wahimize washiriki wa darasa kupekua Yohana 13:1–17 na wafikirie maswali yenye maana wangemwuliza Petro. Tunajifunza nini kutoka maelezo haya ambayo yanaweza kuathiri jinsi tunavyowahudumia wengine?
Upendo ni ufafanuzi wa tabia ya wanafunzi wa Yesu Kristo.
-
Nini kinaweza kuwatia moyo washiriki wa darasa wawe wenye kupenda zaidi? Pengine unaweza kuwauliza jinsi wanavyoweza kujua kwamba mtu fulani waliyekutana naye ni mfuasi wa Kristo. Ni tabia gani wanazoziona kuhusu mtu yule? Unaweza kuwaalika wapekue Yohana 13:34–35 ili kujifunza jinsi wafuasi wa kweli wa Kristo wanaweza kutambuliwa. Tunaweza kufanya nini kuufanya upendo tabia ya ufafanuzi wa ufuasi wetu? Mafundisho haya yanaathiri vipi njia tunayowatendea wengine, ikijumuisha kwenye vyombo vya habari vya jamii?
-
Kama darasa, mmejifunza mengi kuhusu maisha ya Mwokozi mwaka huu, ikijumuisha mifano mingi ya jinsi Alivyoonyesha upendo Wake kwa wengine. Njia mojawapo ya kuwasidia washiriki wa darasa kutafakari amri katika Yohana 13–34 inaweza kuwa kuandika Kama nilivyo wapenda ubaoni na kuwataka washiriki wa darasa kuorodhesha mifano wanayokumbuka kutoka Agano Jipya ambayo inaonyesha upendo wa Yesu. Unaweza kuandika Mpendane ubaoni na waulize washiriki wa darasa kuorodhesha njia tunayoweza kufuata mfano Wake wa upendo. Kuimba au kusikiliza wimbo “Love One Another,” Nyimbo, na. 308: au kutazama mojawapo ya video katika “Nyenzo za Ziada” itakuwa nyongeza mzuri kwenye shughuli hii.
-
Kama hatujisikii hasa kuwa wenye upendo kwa wengine, tunaweza kufanya nini kutafuta karama ya upendo? Ni nini ushauri kwenye Moroni 7:48; 8:26 unaongeza kwenye uelewa wetu wa karama hii? Nani tunamjua ambaye anahitaji kuhisi upendo wetu?
Yohana 14:16–27; 15:26; 16:7–15
Roho Mtakatifu hutuwezesha kukamilisha azma zetu kama wafuasi wa Yesu Kristo.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza majukumu tofauti ya Roho Mtakatifu, fikiria kuwagawa katika vikundi na kukipa kila kikundi mojawapo ya vifungu vifuatavyo: Yohana 14:16–27; 16:26; na 16:7–15. Omba kila kundi liandike ubaoni kile walichojifunza kuhusu Roho Mtakatifu kutoka kwenye vifungu hivi. Washiriki wa darasa wanaweza kuongeza umaizi mwingine wanaoupata wanapochunguza maandiko yaliyoorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada.” Ni wakati gani tumehisi ushawishi wa Roho Mtakatifu? Vitu gani au vielelezo unavyoweza kuvileta darasani ambavyo vitawasaidia washiriki wa darasa kuelewa majukumu ya Roho Mtakatifu?
-
Fikiria kuwaalika washiriki wachache wa darasa kabla ya muda kujifunza mojawapo ya hotuba za mkutano mkuu zilizopendekezwa katika “Nyenzo za Ziada” (au hotuba zingine za mkutano mkuu wanazozijua) kuhusu Roho Mtakatifu. Waruhusu kushiriki kwa muda mfupi kile walichojifunza pamoja na darasa. Hizi jumbe zinaongeza nini kwenye kile tulichojifunza kuhusu Roho Mtakatifu kutoka Yohana 14–16?
Tunapokaa katika Mwokozi, tutakuwa wenye kuzaa matunda na kuwa na furaha.
-
Washiriki wa darasa wamejifunza nini wiki hii kutokana na fumbo la Mwokozi la mzabibu na matawi? Fikiria kuleta mche mdogo darasani na kuutumia kuwasaidia washiriki wa darasa kupata sura ya fumbo la Mwokozi. Baada ya kusoma Yohana 15:1–12 kama darasa, mnaweza kujadili ina maana gani “kukaa katika [Kristo]” (Yohana 15:4). Unaweza kuwataka washiriki wachache wa darasa kushiriki jinsi walivyopata Yohana 15:5–5 kuwa kweli. (Ona pia kauli kutoka kwa Mzee Jeffrey R. Holland katika “Nyenzo za Ziada.”) Video “The Will of God” (LDS.org) ingeweza pia kuwa msaada katika mjadala huu.
Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wameungana kikamilifu, na wanataka na sisi tuungane pia.
-
Pengine huwezi kufundisha kweli zote muhimu zinazopatikana katika Yohana 17 katika majadiliano ya darasa moja, bali hapa kuna njia ya kusaidia darasa kuchunguza baadhi yake. Orodhesha ubaoni mawazo kutoka Yohana 17, kama haya:
-
Uhusiano wetu na Yesu Kristo
-
Uhusiano wa Yesu Kristo na Baba Yake
-
Uhusiano wetu na ulimwengu wote
-
Uhusiano wetu sisi kwa sisi kama wafuasi Wake
Muombe kila mshiriki wa darasa kuchagua mojawapo ya mawazo haya na kusoma Yohana 17, kupekua aya ambazo zinahusiana nayo. Waombe baadhi ya washiriki wa darasa kushiriki kile wanachojifunza.
-
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wahimize washiriki wa darasa wasome Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; na Yohana 18 wiki ijayo, unaweza kuwaambia kwamba katika sura hizi watasoma kuhusu nyakati za maana sana katika mpango mkuu wa wokovu wa Mungu.
Nyenzo za Ziada
Video katika LDS.org kihusu upendo.
-
“Mpendane”
-
“Dhabihu ya Familia, Toa, na Upendo”
-
“Matayarisho ya Thomas S. Monson: Alijifunza Huruma katika Ujana Wake”
Roho Mtakatifu.
-
Matendo ya Mitume 2:37–38; Wagalatia 5:22–23; 1 Nefi 10:17–19; 2 Nefi 32:3–5; Mosia 3:19; 3 Nefi 27:20; Moroni 8:26; 10:4–5; Mafundisho na Maagano 8:2–3; 42:17
-
Robert D. Hales, ”Roho Mtakatifu.” Ensign au Liahona, Mei 2016, 105-7
-
Henry B. Eyring, ”Roho Mtakatifu kama Mwenza Wako.” Ensign au Liahona, Nov. 2015,104-7.
-
David A. Bednar, “Mpokee Roho Mtakatifu” Ensign au Liahona, Nov. 2010, 94-97
Kukaa katika Kristo.
Akifahamu kwamba neno kaa lina maana matilaba ya kudumu na kujitolea, Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:
“Upambanuzi wa [neno] hili basi ni “ishi—bali ishi milele.’ Huu ndio mwito wa ujumbe wa injili. … Njoo, lakini njoo ubakie. Njoo kwa imani na uvumilivu …
“Yesu alisema, ‘Pasipo mimi ninyi hamuwezi kufanya lolote’ [Yohana 15:5]. Ninashuhudia kwamba huo ni ukweli wa Mungu. Kristo ni kila kitu kwetu na tunatakiwa ‘takae’ katika Yeye kwa kudumu, bila kukubali kushindwa, kimathubuti, milele. Ili tunda la injili listawi na kubariki maisha yetu, ni sharti tujishikize Kwake kwa uthabiti, Mwokozi wetu wote, na kwa Kanisa hili, lililo na jina lake takatifu. Yeye ni mzabibu ambao ni chanzo chetu cha kweli cha nguvu na chanzo pekee cha uzima wa milele. Katika Yeye hatutavumilia tu bali pia tutashinda na kushangilia katika kusudi hili takatifu ambalo kamwe halitatufanya tushindwe” (“Abide in Me.” Ensign au Liahona, Mei 2004, 32).