Njoo, Unifuate
Juni 17–23. Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19: ‘Imekwisha’


“Juni 17–23. Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19: ‘Imekwisha’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Juni 17-23. Mathayo 27; Marko ; 15: Luka23; Yohana 19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Kristo mbele ya Pilato

Ecce Homo, na Antonio Ciseri

Juni 17-23

Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19

“Imekwisha”

Anza matayarisho yako ya kufundisha kwa kusoma kwa maombi Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; na Yohana 19. Kumbuka kwamba utaweza kutoa ushahidi wa nguvu wa Mwokozi na Upatanisho Wake unapoishi maisha ya kumstahili Roho.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Inaweza kusaidia kuandika ubaoni baadhi ya maneno na virai kuwakumbusha washiriki wa darasa matukio ambayo yalielezwa katika sura wiki hii. Waombe washiriki wa darasa kuandika ubaoni baadhi ya maneno ambayo yanaeleza jinsi walivyojihisi waliposoma kuhusu matukio haya. Kwa nini walijihisi namna hii?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19

Utayari wa Yesu Kristo kuteseka unaonyesha upendo Wake kwa ajili ya Baba na kwa sisi wote.

  • Ili kusaidia darasa kuelewa jinsi maelezo ya kifo cha Mwokozi yanavyoonyesha upendo Wake, jaribu shughuli kama hii: Mpe kila mshiriki wa darasa karatasi ya upendo, na waalike waandike kwenye mioyo yao kirai kutoka 1 Wakorintho 13:4–7 ambacho kinaelezea hisani. Kisha waombe wapekue Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; au Yohana 19 na waandike upande mwingine wa mioyo yao aya chache ambazo zinaonyesha jinsi Mwokozi alivyoonyesha upendo ulioelezwa katika kirai walichochagua. Waache washiriki kile walichokipata. Uzoefu gani umewasaidia washiriki wa darasa kuelewa upendo wa Mwokozi?

    taji ya miiba

    Askari “wakasokota taji ya miiba, wakamvika kichwani” (Marko 15:17).

  • Unaweza kufanya nini kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki ushuhuda wao wa kile walichojifunza wiki hii? Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kutafuta wimbo ambao unaelezea matukio waliyosoma kuhusu au hasia zao kuhusu mateso ya Mwokozi na Kusulubiwa. Fikiria kuimba mmoja au zaidi ya hizi kama darasa. Jinsi gani kujifunza kuhusu saa za mwisho za Mwokozi kunaweza kutupa mwongozo kumwamini na kumfuata Yeye?

  • Sanaa inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata taswira ya baadhi ya matukio wanayoyasoma kuyahusu wiki hii (ona “Nyenzo za Ziada” kwa picha zilizopendekezwa). Pengine ungeligawa darasa katika vikundi na kutoa picha kwa kila kikundi. Vikundi vinaweza kusoma pamoja aya ambazo zinaeleza nini kimeonyeshwa kimchoro katika picha yao. Wanaweza kujadili maana ya aya na kushiriki jinsi picha inavyowasaidia kuelewa aya vjema. Kila kikundi kinaweza kushiriki mawazo yake pamoja na darasa. Unaweza pia kufikiria kuonyesha video “Jesus Is Condemned before Pilate” and “Jesus Is Scourged and Crucified” (LDS.org).

  • Hutaweza kujadili utondoti wote kuhusu saa za mwisho za Mwokozi kama darasa, lakini hii hapa ni shughuli ambayo inaweza kukusaidia kujadili kila kitu chenye maana sana kwa watu unaowafundisha. Alika kila mshiriki wa darasa kuchagua sura kutoka masomo ya wiki hii na kutumia dakika chache kuikagua, kutafuta neno, kirai, au utondoti unaowafundisha kitu chenye maana kuhusu Mwokozi na huduma Yake. Wape nafasi za kushiriki kile walichopata na kuelezea nini kina maana kwao.

Mathayo 27:14–60

Manabii wa zamani walijua yajayo kuhusu kuteseka kwa Mwokozi na Kusulubiwa.

  • Inaweza kuimarisha imani ya wale unaowafundisha kujua kwamba manabii wa zamani walieleza kabla mengi ya matukio katika saa za mwisho za Mwokozi. Njia moja ya kuwasaidia washiriki wa darasa kurejea unabii huu na kuona jinsi ulivyotimizwa itakuwa ni kumpa kila mtu andiko moja au zaidi katika “Nyenzo za Ziada” na waombe watafute aya katika Mathayo 27 ambayo inaonyesha jinsi maandiko yalivyotimizwa. Unaweza kutengeneza chati ambayo inalingana na unabii pamoja na utimilifu wake. Unaweza kupendekeza kwamba washiriki wa darasa waandike aya zilizo na unabii katika pambizo za maandiko yao katika Mathayo 27. Tunaweza kujifunza nini kutoka unabii huu? Jinsi gani unabii huu unaimarisha imani yetu katika Yesu Kristo?

Mathayo 27:27–49; Marko 15:16–32; Luka 23:11, 35–39; Yohana 19:1–5

Upinzani hauwezi kusitisha kazi ya Mungu.

  • Baadhi ya washiriki wako wa darasa wamewahi kukabiliana na upinzani—kama vile kuhukumiwa au kudhihakiwa—wakati wameonyesha imani yao au kujaribu kuishi imani yao. Fikiria kuanzisha darasa lako kwa kuwaomba baadhi ya washiriki wa darasa kushiriki uzoefu wakati hii ilipotokea. Walijibu vipi? Waalike washiriki wa darasa wasome aya hizi kutoka Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19 zikielezea mateso Mwokozi aliyokabiliana nayo. Ni aina gani za upinzani kazi ya Mungu inakabiliana nao leo? Tunaweza kujifunza nini kutokana na majibu ya Mwokozi ambayo yanaweza kutusaidia kukabiliana na upinzani katika siku zetu? Maandiko mengine ambayo yanaweza kutusaidia tunapokabiliana na upinzani inajumuisha Mathayo 5:10; Warumi 12:14; 2 Timotheo 3:10–12; Alma 1:19–28; 3 Nefi 12:10–12. Tunajifunza nini kutoka kwenye aya hizi?

Luka 11:34–43

Mwokozi anatupa matumaini na msamaha.

  • Je, itawasaidia washiriki wako wa darasa kusoma maelezo ya Mwokozi akimwomba Baba awasamehe askari na matumaini ya ahadi kwa mwizi msalabani? Fikiria kuligawa darasa katika vikundi viwili na kupangia kikundi kimoja kusoma Luka 23:34–38 (ikijumuisha aya 34, tanbihi c, ambayo inatoa umaizi kutoka kwenye Tafsiri ya Joseph Smith) na kikundi kingine kisome Luka 23:39–43. Washiriki wa kila kikundi wajadili kile wanajifunza kuhusu Mwokozi kutoka kwenye aya hizi na kisha washiriki mawazo yao na darasa zima. Tunawezaje kufuata mfano wa Mwokozi?

  • Kumsaidia yoyote katika darasa lako anayeweza kuwa na matatizo ya kuwasamehe wengine kama Yesu alivyofanya, fikiria kushiriki kauli ya Mzee Jeffrey R. Holland katika “Nyenzo za Ziada.”

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; an Yohana 20–21 muda wote wa wiki ijayo, waombe wafikirie kuhusu kile watakachosema kwa mtu fulani aliyesema, “Nahitaji kuona ili niamini.” Waambie kwamba somo la wiki ijayo litawasaidia kujibu tatizo lao.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19

Picha za mateso, kusumbuliwa, na kifo cha Yesu.

Unabii wa kale kuhusu mashtaka na kifo cha Yesu Kristo.

Mfano wa Mwokozi wa msamaha

Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

“Wajibu wetu wa karibu wa kutubu ni ukarimu wa kuacha wengine wafanye vilevile—tunapaswa kusamehe hata kama tunavyosamehewa. Katika hili tunashiriki katika kiini cha Upatanisho wa Yesu Kristo. Kwa hakika muda mfupi hasa wa utukufu wa majaliwa Ijumaa ile, wakati ulimwengu ulisukwasukwa na pazia la hekalu lilipasuka, ulikuwa wakati ule mfupi usiosemeka wa huruma wakati Kristo aliposema, ‘Baba, wasamehe; kwani hawajui wafanyalo.’Kama muombezi wetu kwa Baba, bado anafanya ombi lilelile leo—kwa niaba yako na yangu.

“Hapa, kama katika vitu vyote, Yesu aliweka kiwango kwetu sisi kufuata. Maisha ni mafupi sana kutumika katika kulea chuki. … Hatutaki Mungu akumbuke dhambi zetu, kwa hiyo kuna kitu fulani cha msingi kilicho na makosa katika kujaribu kwetu bila kukoma kuzikumbuka zile za wengine” (“The Peaceable Things of the Kingdom.” Ensign, Nov.1996, 83).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuvuta nguvu kutoka kwa Kristo. Katika juhudi zako kuishi na kufundisha zaidi kama Mwokozi, hautaepuka kukosea wakati mwingine. Usikate tamaa; bali, wacha makosa na upungufu wako ukuelekeze kwa Baba wa Mbinguni na Mwokozi” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 14).