“Juni 24–30. Mathayo 28; Marko 16, Luka 24; Yohana 20–20: ‘Amefufuka’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)
“Juni 24–30. Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–20,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili; 2019
Juni 24–30
Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21
“Amefufuka”
Kabla ya kuchunguza mawazo ya kufundisha katika muhtasari huu, soma Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20–21, na utafakari jinsi sura hizi zinaweza kutumika kuimarisha imani ya wale unaowafundisha.
Andika Misukumo Yako
Himiza Kushiriki
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki kile walijifundisha katika kujifunza kwao binafsi na familia, waombe waandike ukweli kutoka katika somo lililopangwa wiki hii ambao wanahisi unapaswa kushirikishwa kwa “ulimwengu wote” (ona Marko 16:15). Mwisho wa darasa, waulize kama walipata kweli zozote za nyongeza wangependa kushiriki.
Fundisha Mafundisho
Mathayo 28; Marko 16; Luka 24; Yohana 20
Kwa sababu Yesu alifufuka, sisi pia tutafufuliwa.
-
Kuwapa nafasi watu wengi kadri inavyowezekana kushiriki kile walichojifunza kuhusu Ufufuo, unaweza kuwapa washiriki wa darasa dakika chache kurejea somo lililopangwa wiki hii na “Ufufuo” katika Kamusi ya Biblia na uandike kweli walizojifunza kuhusu Ufufuo. Waache washiriki kile walichoandika, na wahimize wainue mikono yao wakati wanaposikia mtu fulani akishiriki ukweli ambao unafanana na ule walioandika. Kwa nini kweli hizi ni muhimu kwetu? Ni kwa jinsi gani kujua kwamba tutafufuliwa kunaathiri hisia zetu kuhusu Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo? Kuonyesha video ya muziki “He Is Risen” (LDS.org) kunaweza kusaidia kumwalika Roho kwenye mazungumzo haya.
Tunaweza kumwalika Mwokozi “kukaa pamoja nasi.”
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuona uhusiano kati ya uzoefu wao na uzoefu wa wafuasi waliokuwa njiani kwenda Emau, chora njia ubaoni, na waulize washiriki wa darasa waandike kila kitu kutoka kwenye maelezo katika Luka 24:13–35 upande mmoja wa njia. Kisha, upande mwingine wa njia, wanaweza kuandika milinganisho wanayoona kwenye uzoefu wao wenyewe kama wafuasi wa Yesu Kristo. Kwa mfano, wanaweza kuandika Macho yao yalifumbwa (Luka 24:16) upande mmoja wa njia na Wakati mwingine hatutambui ushawishi wa Bwana katika maisha yetu upande mwingine.
-
Kuna nyimbo mbili zenye msingi kwenye Luka 24:13–35; “Abide With Me:’Tis Eventide” na Abide With Me!” Nyimbo, na. 165, 166. Unawezaje kutumia nyimbo hizi kuwasaidia washiriki wa darasa kupata maana ya kina zaidi katika maelezo ya kimaandiko?
Mathayo 28:16–20; Marko 16:14–20; Luka 24:44–53
Tumeamriwa kuhubiri injili ulimwenguni kote.
-
Amri ambayo Mwokozi aliyefufuka aliwapa Mitume Wake kuhubiri injili Yake inaweza pia kutumika kwetu leo. Jinsi gani unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuona wajibu wao katika kuhubiri injili? Pengine unaweza kuwaalika wafikirie kwamba walikuwa wanatoa ushauri fulani kwa mwanafamilia au rafiki ambaye yuko karibu kuondoka kwenda kwenye misheni. Nini tunaweza kushiriki kutoka kwenye maneno ya Mwokozi kwa Mitume Wake? Tunawezaje kutumia maneno haya haya katika juhudi zetu kushiriki injili na wengine?
“Heri wale wasioona, wakasadiki.”
-
Unaweza kuwa na washiriki wa darasa wanaomhurumia Tomaso, ambaye alitamani kumwona Bwana mfufuka kabla kuamini. Darasa la Shule ya Jumapili lako linaweza kuwa mahali pa washiriki wa darasa kuimarishana imani zao katika vitu ambavyo hawavioni. Pengine unaweza kuanza kwa kumuomba mtu fulani kufanya muhtasari wa uzoefu wa Tomaso katika Yohana 20:19–28. Unaweza pia kuonyesha video “Blessed Are They That Have Not Seen, and Yet Have Believed” (LDS.org). Washiriki wa darasa wanaweza kuorodhesha ubaoni baadhi ya vitu Mungu anatutaka sisi tuamini bila kuviona. Kisha unaweza kuwaomba washiriki uzoefu ambao umeimarisha shuhuda zao za vitu hivi. Baraka gani zimewajia washiriki wa darasa walipotumia imani?
Mwokozi anatualika tuwalishe Kondoo Wake.
-
Nini kinaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kukubali mwaliko wa Mwokozi “kuwalisha kondoo [Wake]”? Unaweza kuanza kwa kuwaalika wasome Yohana 21:15–17 kimyakimya, wakibadilisha jina la Simioni na kuweka majina yao na “kondoo wangu” na majina ya watu wanaohisi Bwana anawataka wawahudumie—kwa mfano, watu wanaowafundisha nyumbani au kuwatembelea, majirani, au watu wanaowafahamu kazini au shuleni. Baada ya dakika chache, washiriki wa darasa wanaweza kushiriki misukumo waliopata. Inamaanisha nini kuwalisha wanakondoo na kondoo wa Mwokozi? Kauli za Rais Russell M. Nelson na Mzee Marvin J. Ashton katika “Nyenzo za Ziada” zinaweza kusaidia kujibu swali hili.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma Matendo ya Mitume 1–5 wiki hii, waombe wasikilize kwa makini jinsi mvuvi asiyeelimika alivyokuwa kiongozi mwenye nguvu wa Kanisa la Kristo lilipokuwa likisambaa ulimwenguni kote. Wanapojifunza sura hizi, wataona jinsi mabadiliko haya yalivyotokea.
Nyenzo za Ziada
Inamaanisha nini kulisha kondoo wa Mwokozi?
Rais Russell M. Nelson alishiriki umaizi huu kutoka matini ya zamani ya Kiyunani ya Yohana 21:
“Katika [Yohana 21:15], neno Lisha linatokana na neno la Kiyunani bosko ambalo linamaanisha ‘kulisha au malisho.’ Neno mwanakondoo linatokana na neno dogo sana arnion, maana yake ‘mwanakondoo mdogo.’ …
“Katika [Yohana 21:16], neno lisha linatokana na neno tofauti, poimaino, ambalo linamaanisha ‘kuchunga kondoo, kuchunga, au kutunza.’ Neno Kondoo linatokana na neno Probaton, maana yake ‘kondoo iliyepevuka.’ …
“Katika [Yohana 21:17], neno Lisha tena linatokana na la Kiyunani bosko kurejea chakula. Neno Kondoo lilitafsiriwa tena kutoka neno la Kiyunani probaton, kurejea Kondoo mkubwa.
“Aya hizi tatu, ambazo zinaonekana kufanana mno katika lugha ya Kiingereza, kwa kweli zina taarifa tatu tofauti katika Kiyunani:
-
Wanakondoo wadogo wanahitaji kulishwa ili wakue;
-
Kondoo wanahitaji kuchungwa;
-
Kondoo wanahitaji kulishwa” (“Shepherds, Lambs, and Home Teachers,” Ensign, Aug.1994, 16).
Tunawezaje “kulisha kondoo [Wake]”?
Mzee Marvin J. Ashton alielezea jinsi tunavyoweza kutimiza amri ya Bwana ya kulisha kondoo Wake:
“Yesu alisema, ‘Lisha kondoo wangu.’ (Yohana 21:16.) Huwezi kuwalisha kama hujui pale walipo. Huwezi kuwalisha kama unawapa sababu za kukataa. Huwezi kuwalisha kama huna chakula. Huwezi kuwalisha kama huna hisani. Huwezi kuwalisha kama hauko tayari kufanya kazi na kushiriki. …
“Wale wanaohitaji msaada wanakuja katika marika yote. Baadhi ya kondoo Wake ni wachanga, wapweke, na wamepotea. Baadhi ni wachovu, walioteseka na wamechoka kiumri. Baadhi wako kwenye familia zetu, majirani zetu, au katika pembe za mbali za ulimwengu ambako tunaweza kuwasaidia kwa matoleo ya mfungo. Baadhi wanahitaji sana chakula. Baadhi wanahitaji sana upendo na kujaliwa.
“Kama tutawapa kondoo Wake sababu za kutukataa sisi, mchakato wa kulisha unakuwa mgumu, kama si kutowezekana. Hakuna anayeweza kufundisha au kusaidia kwa dhihaka na kejeli. Udikteta au ‘Mimi ni sahihi na wewe umekosea’ utakosesha juhudi zote za kulisha kondoo wanaotangatanga. Ukuta wa upinzani utajengwa, na hakuna atakayenufaika. …
“Kwa matendo yetu tunaonyesha upendo wetu. Hisia za upendo ni bure kama matendo hayalingani. Kondoo Wake wote wanahitaji mguso wa mchungaji anayejali” (“Give With Wisdom That they May Receive with Dignity.” Ensign, Nov.1981, 91).