Njoo, Unifuate
Julai 1–7. Matendo ya Mitume 1–5: ‘Mtakuwa Mashahidi juu Yangu’


“Julai 1–7. Matendo ya Mitume 1–5: ‘Mtakuwa Mashahidi Juu Yangu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019.)

“Julai 1–7. Matendo ya Mitume 1–5,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

siku ya Pentekosti

Siku ya Pentekoste, na Sidney King

Julai 1–7.

Matendo ya Mitume 1–5

Matendo ya Mitume 1–5: “Mtakuwa Mashahidi juu Yangu”

Kama utasoma Matendo ya Mitume 1–5 na kutafuta mwongozo toka kwa Roho, utapokea ufunuo kuhusu kweli zipi zilizopo kwenye hizo sura ambazo zitawasaidia washiriki wa darasa lako kumtegemea zaidi Roho na kuwa mashahidi waaminifu wa Bwana Yesu Kristo.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kuna vifungu vingi muhimu na kanuni katika Matendo ya Mitume 1–5. Njia kuu mojawapo ya kugundua ni vipi vya thamani na vya muhimu kwa washiriki wa darasa lako ni kwa kuwaacha wakuambie kile kilichokuwa muhimu kwao wakati wa kujifunza kwao. Je, ni kwa namna gani unaweza kualika namna hii ya kushiriki? Ingeweza kuwa rahisi kama vile kuwapa dakika chache kutafuta na kuelezea mstari kutoka Matendo ya Mitume 1–5 ambapo walihisi sauti ya Bwana ikizungumza nao.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Matendo ya Mitume 1:1–8; 2:37–39; 4:1–16, 31–33

Yesu Kristo huongoza Kanisa Lake kupitia Roho Mtakatifu.

  • Kusoma kuhusu uzoefu wa Mitume kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuona jinsi gani wanaweza kupokea nguvu na mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu katika miito yao ya Kanisani. Njia mojawapo ya kurejea uzoefu katika Matendo ya Mitume 1–5 ingekuwa kuandika ubaoni Roho Mtakatifu anaweza kunisaidia katika wito wangu kwa: na kisha waalike washiriki wa darasa kutafuta kutoka Matendo ya Mitume 1:1–8; 2:36–39; na 4:1–16, 31–33, wakiangalia njia za kumalizia sentensi hiyo. Kwa nini Mitume walimhitaji Roho Mtakatifu.

  • Kama darasa, mnaweza kutafuta jinsi Yesu Kristo anavyoliongoza Kanisa Lake katika siku zetu kupitia Roho Mtakatifu. Ili kufanya hivi, ungeweza kuwasiliana kabla na baadhi ya washiriki wa darasa na kuwaomba kurejea matukio katika Matendo ya Mitume 1:1–8; 2:37–39; 4:1–16, 31–33 na kuja wakiwa wamejiandaa kushiriki uzoefu wao binafsi ambao ni sawa na ule wa Mitume. Kwa mfano, wangeweza kuelezea kuhusu wakati ambapo Roho Mtakatifu aliwasaidia kushuhudia kuhusu kanuni ya injili au kujibu swali la mtu fulani. Walifanya nini kutafuta mwongozo wa Roho Mtakatifu?

Matendo ya Mitume 1:15–26

Mitume wa Yesu Kristo wanaitwa na Mungu kupitia ufunuo.

  • Ingeweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kujua kuwa washiriki wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili katika kanisa la awali waliitwa kwa ufunuo, kama wanavyoitwa sasa. Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kuelezea jinsi gani makampuni ya kibiashara hupitia mchakato wa kumchagua mtu kujaza nafasi ya mtendaji, kama vile kuangalia uwezo wa kielimu, uzoefu na kadhalika. Waombe kutofautisha na jinsi gani Mtume Mathiya aliitwa katika Matendo ya Mitume 1:15–26 (ona pia 1 Samueli 16:1–13). Ni kwa namna gani nukuu toka kwa Rais Gordon B. Hinckley kwenye “nyezo za ziada” huongeza katika uelewa wa washiriki wa darasa? (Ona pia Russell M. Nelson, “Kuwakubali Manabii,” Ensign au Liahona, Nov. 2014, 74–77). Ni kwa namna gani uelewa huu unaathiri imani yetu kwa viongozi ambao Bwana amewaita? Ni kwa jinsi gani umepokea ushahidi wako juu ya mitume na manabii wa sasa?

Matendo ya Mitume 2:22–47; 3:13–26; 4:5–12

Tunapokea baraka za Upatanisho tunapoishi kanuni na ibada za kwanza za injili.

  • Ni kwa namna gani wale unaowafundisha wanaweza kupata maana na nguvu katika ukweli rahisi unaofundishwa na Petro na Yohana (Imani katika Yesu Kristo, Toba, Ubatizo, Kipawa cha Roho Mtakatifu, na Kuvumilia hadi mwisho)? Njia mojawapo inaweza kuwa kwa kutafuta umuhimu wa kanuni hizi na ibada, wakati mwingine zikiitwa kama mafundisho ya Kristo (ona 2 Nephi 31). Ungeweza kuleta mabango matano darasani na kuandika juu ya kila moja mojawapo kati ya vipengele vya mafundisho ya Kristo: Imani katika Yesu Kristo, Toba, Ubatizo, Kipawa cha Roho Mtakatifu, Kuvumilia hadi mwisho. Ligawe darasa katika makundi matano na lipe kila kundi moja ya mabango hayo. Alika makundi kurejea maana za mada katika mabango yao katika Mwongozo wa Maandiko au Hubiri Injili Yangu. Wangeweza kurejea mafundisho ya Petro katika Matendo ya Mitume 2:22–47; 3:13–26; na 4:5–12 na kuandika kwenye mabango yao mifano ya mada walizopewa kutoka kwenye maandiko. Ni kwa namna gani kanuni hizi na ibada za injili hutusaidia kupata baraka za Upatanisho wa Mwokozi? Kanuni na ibada hizi zina kazi gani katika mpango wa wokovu wa Baba Yetu wa Mbinguni?

  • Ungeweza kuwaomba baadhi ya wamisionari waliomaliza misheni hivi karibuni, au wamisionari wa kata kutumia dakika chache kuelezea jinsi gani wamefundisha wengine kuhusu mafundisho ya Kristo kwa kutumia somo la 3 katika Hubiri Injili Yangu. Ni kwa nini mafundisho ya Kristo ni ujumbe mkuu wa wamisionari wetu? Ni kwa namna gani mtu ambaye tayari amekwishabatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu anaendelea kufuata mafundisho ya Kristo?

Matendo ya Mitume 2:37–47

Roho Mtakatifu hutufunulia kutenda tunachojifunza.

  • Wakati washiriki wa darasa wanapojifunza maandiko nyumbani na kwa pamoja katika darasa kila wiki wanaweza kila mara kuhisi “kuchomwa mioyoni mwao” (Matendo ya Mitume 2:37). Unaweza kusikia mwongozo wa kiungu ili kuwasaidia kwenda hatua moja mbele kwa kuwauliza, “tunaweza kufanya nini?” Matendo ya Mitume 2:37). Soma Matendo ya Mitume 2:37–47 kwa pamoja, waalike washiriki wa darasa kutafuta mambo ambayo kundi hili la watu 3,000 lilifanya kama matokeo ya mwaliko wa Petro. Labda wangeweza pia kuelezea njia ambazo wamefuata kutokana na mwongozo wa kiungu waliopata kutokana na usomaji wao wa neno la Mungu. Kisha ungeweza kubakiza muda mwisho wa darasa kwa kila mtu kujiuliza swali “Je, mimi nitafanya nini?” Na kuandika misukumo yao.

Petro anahubiri baada ya kupigwa

Licha ya kufungwa gerezani na kupigwa, Petro kwa uthabiti alihubiri injili.

Matendo ya Mitume 3; 4:1–21; 5:12–42

Tunapojazwa na Roho Mtakatifu, tunaweza kufundisha injili kwa uthabiti.

  • Tukio la Petro na Yohana kushuhudia kwa uthabiti juu ya Yesu Kristo linaweza kushawishi darasa lako kutoogopa kile watu wengine hufikiria wakati wanapotoa ushahidi wao juu ya injili. Je, ni kitu gani kinawavutia washiriki wa darasa kuhusu uthabiti wa Petro na Yohana katika Matendo ya Mitume 3; 4:1–21; na 5:12–42? Kuna uhusiano gani kati ya kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu na uwezo wetu wa kushuhudia kwa uthabiti? Matukio ya sura hizi yameigizwa katika video “Petro Anahubiri na Anafungwa Gerezani,” “Petro na Yohana Wanahukumiwa,” na Petro na Yohana Wanaendelea Kuhubiri Injili” (LDS.org). Washiriki wa darasa yawezekana pia wakawa na uzoefu wa kusimulia ambao wao, au mtu mwingine wanayemjua, kwa uthabiti alitetea au alishuhudia juu ya injili.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waombe washiriki wa darasa kufikiria kuhusu jinsi gani wangefanya kama wangejua kuwa kuishi injili kungeweza kusababisha kupoteza maisha yao. Waambie katika Matendo ya Mitume 6–9 watasoma kuhusu mtu fulani aliyekuwa tayari kufa kwa sababu ya imani yake.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Matendo ya Mitume 1–5

Wito wa mshiriki wa Kumi na Wawili

Gordon B. Hinckley alielezea utambuzi ufuatao kuhusu mchakato wa kuitwa kwa Mtume mpya: “utaratibu ni wa kipekee kwa kanisa la Bwana. Hakuna kutafuta ofisi, hakuna kushindania nafasi, hakuna kampeni ya kunadi wema wa mtu. Njia ya Mungu ni tofauti na njia ya ulimwengu. Njia ya Mungu ni tulivu, ni njia ya amani, haina mshindo wa nderemo wala gharama za kifedha. Haina kujikweza wala malengo yasiyo na maana. Chini ya mpango wa Bwana, wale wenye majukumu ya kuchagua maofisa wanaongozwa na swali moja la muhimu: ‘Ni yupi Bwana angemtaka?’ Kuna ukimya na kushauriana kwa kina. Na kuna sala nyingi ili kupokea uthibitisho wa Roho Mtakatifu kwamba chaguo ni sahihi” (“Mungu Yu katika Usukani,” Ensign, Mei 1994, 53).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Waamini viongozi wako. Viongozi wako wa ukuhani na vikundi saidizi wanataka kukusaidia ufanikiwe. Omba ushauri wao wakati unapojitahidi kujiboresha kama mwalimu na unapotafakari mahitaji ya wale unaowafundisha” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 5).