Njoo, Unifuate
Julai 8–14. Matendo ya Mitume 6–9: ‘Ungetaka Nifanye Nini?’


“Julai 8–14. Matendo ya Mitume 6–9: ‘Ungetaka Nifanye Nini?’“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Julai 8–14. Matendo ya Mitume 6–9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Paulo akielekea Dameski.

Na Tuishi Hivyo, na Sam Lawlor

Julai 8–14

Matendo ya Mitume 6–9

Matendo ya Mitume 6–9: “Ungetaka Nifanye Nini?”

Jifunze Matendo ya Mitume 6–9 na uandike misukumo yako. Hii itakusaidia kupokea ufunuo wa jinsi ya kuwasaidia washiriki wa darasa lako kumsogelea Kristo kupitia kujifunza kwao sura hizi.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kwenye ubao, andika majina ya baadhi ya watu waliotajwa kwenye Matendo ya Mitume 6–9, kama vile Stefano, Sauli, Filipo, Anania, Petro, na Tabitha au Dora. Waliike washiriki wachache wa darasa kuelezea kitu fulani walichojifunza kutoka kwa mmoja wa watu hawa katika kujifunza kwao wiki hii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Matendo ya Mitume 7

Kumpinga Roho Mtakatifu kunaweza kusababisha kutomkubali Mwokozi na manabii Wake.

  • Je, ni kweli zipi washiriki wa darasa walijifunza wiki hii kutokana na kusoma tukio la Stefano? Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kujifunza mafundisho ya Stefano katika Matendo ya Mitume 7:37–53, wakitafuta ni kwa namna gani viongozi wa Kiyahudi walikuwa kama Waisraeli wa kale ambao waliwakataa manabii. Unaweza kuzingatia kwenye kauli ya Stefano kuhusu viongozi hawa katika Matendo ya Mitume 7:51. Ni kwa namna gani 2 Nefi 28:3–6; 33:1–2; Mosia 2:36–37; Alma 10:5–6; na Alma 34:37–38 huwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kauli hii? Inawezekanaje sisi “kumpinga Roho Mtakatifu”? Tunaweza kufanya nini ili kuweza kutambua zaidi na kufuata ushawishi wa Roho Mtakatifu?

Matendo ya Mitume 8:9–24

Mioyo yetu inatakiwa kuwa “minyoofu mbele za Mungu.”

  • Kusoma tukio la Simoni kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutathmini sababu ya wao kuishi injili. Kusoma tukio hili kama darasa, ungeweza kuandika kwenye ubao maswali haya Je, Simoni alikuwa nani? Yeye alitaka kitu gani? na Ni kwa namna gani alijaribu kukipata? Mpangie kila mshiriki wa darasa kusoma Matendo ya Mitume 8:9–24, akitafuta majibu ya maswali haya. Tunajifunza nini kutokana na uzoefu wa Simoni?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa nini humaanisha kwa mioyo yao kuwa “minyoofu mbele za Mungu” (Matendo ya Mitume 8:21), ungeweza kuwaalika kujifunza Mafundisho na Maagano 121:41–46, wakitafuta maneno au virai ambavyo vinaelezea ni kwa namna gani mioyo yetu inatakiwa kuwa wakati tunapojitahidi kumtumikia Mungu na kupokea zawadi Zake. Washiriki wa darasa wangeweza kulinganisha utambuzi huu na tukio la Simoni, lipatikanalo katika Matendo ya Mitume 8:9–24. Ni kweli zipi ambazo Simoni alikuwa hajazielewa? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuiandaa mioyo yetu ili kupokea neno la Mungu?

  • Je, washiriki wa darasa lako waliwalinganisha Stefano na Filipo pamoja na Simoni wakati wa kujifunza kwao binafsi, kama ilivyopendekezwa katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia? Kama ndivyo, je, walijifunza nini? Ungeweza kuwaalika kutafuta uthibitisho kwenye sura hizi kwamba mioyo ya watu wengine ilikuwa minyoofu—watu kama Filipo na mtu yule wa kutoka Ethiopia (Matendo ya Mitume 8:26–40) na Sauli (Matendo ya Mitume 9:1–22).

Matendo ya Mitume 8:26–39

Roho Mtakatifu atatusaidia kuwaongoza wengine kwa Kristo.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa ni kwa namna gani wanaweza kuwaongoza wengine kwa Kristo (ona Matendo ya Mitume 8:31), ungeweza kuwaalika washiriki wawili wa darasa kukaa mkabala na kusoma mazungumzo ya Filipo na mtu yule wa kutoka Ethiopia katika Matendo ya Mitume 8:26–39. Mshiriki wa tatu wa darasa angeweza kusoma sehemu ambazo si za mazungumzo. Tunajifunza nini kutokana na mfano wa Filipo kuhusu kufundisha injili kwa wengine?

  • Kufafanua mifano ya sasa ya tukio katika Matendo ya Mitume 8:26–39, washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu waliokuwa nao katika kushiriki injili au kujiunga kwao na kanisa. Ni kwa namna gani Roho Mtakatifu aliwasaidia? Ni kwa namna gani mtu fulani alitumika kama mwongozo kwao? Waalike washiriki wa darasa kutafakari nani wanaweza kumwongoza kwenye injili.

Matendo ya Mitume 9

Tunapokubali mapenzi ya Bwana, tunaweza kuwa vyombo katika mikono yake.

  • Washiriki wa darasa wanaweza kujifunza ukweli wenye nguvu kuhusu uongofu wao kwa kujifunza kutokana na uzoefu wa Sauli, ikijumuisha ukweli kwamba kila mtu anaweza kutubu na kubadilika kama watakuwa tayari. Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kulinganisha uzoefu wa Sauli na ule wa Alma (ona Mosia 17:1–418; 26:15–21) na Lamani na Lemueli (ona 1 Nefi 3:28–31). Ni sifa zipi za Sauli na Alma zilizowasaidia kutubu na kubadilika? Ni sifa zipi ziliwafanya Lamani na Lemueli wasibadilike? Ni ushawishi gani waliokuwa nao Sauli na Alma baada ya kuwa wameongoka? Ni ujumbe gani tunaupata kwa ajili ya maisha yetu kutokana na matukio haya

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutumia uzoefu wa Sauli katika maisha yao, ungeweza kuwaalika washiriki wachache kuja wakiwa wamejiandaa kuelezea kile wanachojifunza kutoka kila sehemu ya ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf “Kusubiri katika njia iendayo Dameski” (Ensign au Liahona, Mei 2011, 70–77). Ni kwa namna gani wakati mwingine tunasubiri katika njia yetu wenyewe ya kwenda Dameski? Kulingana na Rais Uchtdorf, nini kinaweza kutusaidia zaidi kuisikia sauti ya Mungu? Unaweza pia kufikiria kuangalia video “The Road to Dameski” (LDS.org). Ili kuwatia hamasa washiriki wa darasa kufuata mfano wa Sauli na kumuliza Bwana “Ungetaka nifanye nini?” fikiria kujadili uzoefu wa Rais Thomas S. Monson upatikanao katika “Nyenzo za ziada.” Labda washiriki wa darasa wangeelezea uzoefu wao wa kutafuta na kufuata mapenzi ya Mungu.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma Matendo ya Mitume 10–15 wakati wa wiki ijayo, ungeweza kusimulia baadhi ya matukio muhimu katika sura hizi—kubomoka kwa gereza kimiujiza, wamisionari wakidhaniwa kimakosa kuwa miungu ya Kirumi, na Mtume akipigwa mawe na kuachwa afe—kisha kuhuishwa.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Matendo ya Mitume 6–9

Matendo ya Mitume 6–9: “Ungetaka Nifanye Nini?”

Wakati Rais Thomas S. Monson alipokuwa akihudhuria mkutano wa kigingi, rais wa kigingi alimuuliza kama angeweza kumtembelea msichana wa miaka 10 aliyeitwa Christal Methvin, ambaye alikuwa akishambuliwa na saratani. Familia ya msichana huyu iliishi maili 80 kutoka eneo la mkutano. Rais Monson alielezea yafuatayo:

“Niliangalia ratiba ya mikutano. … Kiufupi hakukuwa na muda wa kutosha. Pendekezo mbadala likaja akilini mwangu. Hatungeweza kumkumbuka mtoto huyu katika sala zetu za pamoja kwenye mkutano huu? …

“… [Katika moja ya mikutano] nilikuwa nikipanga muhtasari wangu, nikijiandaa kusimama kwenye mimbari, ndipo niliposikia sauti ikiongea na roho yangu. Ujumbe ulikuwa mfupi, maneno ya kueleweka: ‘Waacheni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie: kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.” (Marko 10:14.) Muhtasari wangu ukawa kama umezibwa na ukungu. Mawazo yangu yakamgeukia msichana mdogo aliyehitaji baraka. Uamuzi ukafanywa Ratiba ya mkutano ikabadilishwa. …

“… [Nyumbani kwa Methvin,] Nilimkazia macho mtoto ambaye alikuwa akiumwa sana—mdhaifu karibu ya kushindwa kuzungumza. Ugonjwa wake sasa ulimuacha ashindwe kuona. Roho ilikuwa na nguvu sana kwamba nikapiga magoti, nikauchukua mkono wake dhaifu kwa mkono wangu, na kusema kiurahisi, ‘Christal, niko hapa.’ Alifungua mdomo wake na kunong’ona, ‘Kaka Monson, Nilijua tu ungekuja’” (“Imani ya Mtoto,” Ensign, Nov. 1975, 20–22).

Miaka kadhaa baadae, Rais Dieter F. Uchtdorf alisimulia hadithi, akitualika sisi “kujitahidi kuwa kati ya wale ambao Bwana anaweza kuwategemea katika kusikia minong’ono Yake na kuiitikia, kama Sauli alivyofanya katika njia yake kuelekea Dameski, ‘Bwana, ungetaka nifanye nini?’” (“Kusubiri katika njia iendayo Dameski,” Ensign au Liahona, Mei 2011, 75).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ongoza wanafunzi wako. Kama mwalimu, unaweza kuwaongoza wale unaowafundisha kupitia maandiko, kama Filipo alivyomwongoza Muethiopia kwa kumfundisha kutoka Isaya (ona Matendo ya Mitume 8:26–37). Kufanya hivi, “lazima utafute maarifa hata kwa kujifunza na pia kwa imani” (Mafundisho na Maagano 109:7). Maarifa unayopata yanaweza kuwa kani ya nguvu katika kuwasaidia washiriki wa darasa kuwa na hamu ya kutambua ukweli wao wenyewe na kuuishi.

Chapisha