“Julai 15–21. Matendo ya Mitume 10: ‘Neno la Mungu Likazidi na Kuenea’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)
“Julai 15–21. Yohana 10–15,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019
Julai 15–21
Matendo ya Mitume 10–15
“Neno la Mungu Likazidi na Kuenea”
Kujifunza kwa maombi Matendo ya Mitume 10–15 kabla ya kusoma muhtasari huu kutakusaidia kupokea misukumo kutoka kwa Bwana. Mawazo hapa chini ni mapendekezo tu.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waalike washiriki wa darasa kushiriki, na mtu ambaye wamekaa nae karibu, uzoefu wa kimisionari kutoka Matendo ya Mitume 10–15 ambao uliwavutia. Alika wachache kuelezea umaizi wao kwa darasa zima.
Fundisha Mafundisho
Matendo ya Mitume 10; 11:1–18; 15:1–25
Baba Yetu wa Mbinguni hutufundisha mstari juu ya mstari kupitia ufunuo.
-
Baadhi ya washiriki wa darasa wanaweza kuwa na mawazo yasiyo sahihi kuhusu mchakato wa kupokea ufunuo. Inaweza kuwasaidia wao kujadili jinsi gani ufunuo ulikuja kwa Petro na jinsi gani wanaweza kusonga mbele, “bila shaka yoyote” (Matendo ya Mitume 10:20), wakati ufunuo unapoonekana kutokamilika au kutoeleweka. Fikiria kuchora mstari kwenye ubao na andika kwenye mwisho wa mstari Injili ifundishwe kwa Wayunani. Kama darasa, pitieni Matendo ya Mitume 10 na 11:1–18, na kisha muongeze vipengele kwenye mstari ambavyo vinaonyesha ni kwa namna gani Bwana alimfunulia Petro hatua kwa hatua kwamba muda ulikuwa umefika wa kuhubiri injili kwa Wayunani. Kwa mfano, ungeweza kuanza na kipengele kiitwacho “Kornelio aliona ono” (Matendo ya Mitume 10:1–6) au hata kuanza na amri ya Mwokozi kwa wanafunzi Wake “mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi” katika Mathayo 28:19. Tunaweza kujifunza nini kuhusu ufunuo kupitia uzoefu wa Petro? Mafundisho ya Nefi kuhusu ufunuo katika 2 Nefi 28:30 na mafundisho kutoka kwa Mzee David A. Bednar na Mzee Dallin H. Oaks katika “Nyenzo za Ziada” huongeza nini katika majadiliano?
-
Ungewezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari kwa kina zaidi kuhusu jinsi gani wanapokea ufunuo? Unaweza kujifunza mifano kutoka kwenye maandiko ambamo ndani yake Bwana aliwafundisha watu mstari juu ya mstari. Kama nyongeza kwa uzoefu wa Petro katika Matendo ya Mitume 10, washiriki wa darasa wangeweza kurejea uzoefu wa Nefi (1 Nefi 18:1–3); Alma (Alma 7:8; 16:20); na Mormoni (3 Nefi 28:17, 36–40). Mifano gani mingine washiriki wa darasa wanafikiri ambapo watu walipokea mwongozo wa kiroho “hapa kidogo na pale kidogo”? (2 Nefi 28:30). Ni kwa nini wakati mwingine Bwana anachagua kufunua mambo katika njia hii kuliko kutupatia majibu yote kwa wakati mmoja? (Ona Mafundisho na Maagano 50:40; 98:12). Analojia kama hii inaweza kusaidia: Chukulia mtu fulani alipendekeza kuwa usome darasa la kalkulasi kabla ya kujifunza aljebra au jometri. Je, wewe ungemjibu nini? Je, ni kwa jinsi gani hii inahusiana na mpangilio wa Bwana kwa ajili ya kufunua ukweli?
-
Wakati mwingine waumini wanakuwa na tatizo kuhusu mabadiliko katika sera au programu katika Kanisa. Ingeweza kuwasaidia wao kujadili jinsi gani ufunuo wa kuanza kufundisha injili kwa Wayunani (ona Matendo ya Mitume 10) ulichukua nafasi ya maelekezo ya awali ya Bwana kwa wanafunzi wake (ona Mathayo 10:1, 5–6). Ni kwa namna gani washiriki wa darasa wangeweza kuitikia kama mmoja wa watu waliokuwepo wakati wa Petro ambaye hakukubaliana na mwongozo wa Petro kwa sababu ulipingana na tamaduni za awali? Ni kwa namna gani ufunuo katika Matendo ya Mitume 10 unatusaidia kufuata ufunuo endelevu wa Bwana kupitia manabii Wake?
-
Ingekuwa ya kupendeza kurejea majadiliano ya pamoja ambayo yalifanyika miongoni mwa Mitume, kama ilivyoelezwa katika Matendo ya Mitume 15:1–22, na barua waliyoandika kwenda kwa Watakatifu (ona mistari 23–29). Ungeweza kuonyesha video ya “The Jerusalem Conference” (LDS.org). Je, ni swali gani wanafunzi walikuwa nalo? Je, ni kwa namna gani walitafuta jibu? Kauli toka kwa Rais Gordon B. Hinckley katika “Nyenzo za Ziada” inaweza kuongeza mwanga zaidi juu ya jinsi gani Bwana huongoza Kanisa Lake kupitia ufunuo kwa mitume na manabii.
“Mungu hana upendeleo .”
-
Je, washiriki wa darasa lako wangenufaika kutokana na majadiliano kuhusu kile kinachomaanishwa na “hana upendeleo”? Unaweza kuanza kwa kualika darasa kusoma maandiko ambayo yanafundisha kwamba Mungu hana upendeleo, kama vile Warumi 2:1–11; 1 Nefi 17:34–40; 2 Nefi 26:32–33; Alma 5:33; Moroni 8:12; na Mafundisho na Maagano 1:34–35. Waombe washiriki wa darasa kuandika maana zinazowezekana za “hana upendeleo,” kulingana na kile wanachosoma, halafu waelezee kile walichoandika. Unaweza kuhitajika kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kwamba “hana upendeleo” haimaanishi kwamba Mungu humbariki kila mtu sawa sawa bila kujali matendo yetu. Yeye anataka watoto Wake wote waikubali injili, lakini utimilifu wa baraka za injili umetunzwa kwa ajili ya wale wanaofanya Naye maagano na kuyashika. Ni kwa namna gani matukio na kanuni katika Matendo ya Mitume 10:34–48 huonyesha kwamba Mungu hana upendeleo? Ni kwa namna gani mwenye haki “anakubaliwa” na “kupendelewa” na Mungu licha ya kwamba Yeye hana upendeleo? (ona Matendo ya Mitume 10:34–35; 1 Nefi 17:35).
Sala za mwenye haki zinaweza kuleta miujiza mikubwa.
-
Tukio la Petro kuokolewa kutoka gerezani katika Matendo ya Mitume 12:1–17 linaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kujenga imani katika nguvu ya sala. Labda mshiriki wa darasa angeweza kuja amejiandaa kuelezea kwa undani hadithi hii na ushuhuda wake juu ya sala. Au ungeweza kumwalika muumini mmoja au zaidi wa kata au tawi kushiriki uzoefu ambao kupitia huo walihisi au kushuhudia nguvu ya sala za pamoja za waumini. Unaweza pia kuimba wimbo kuhusu sala (kama vile “Je Uliomba?” Wimbo, namba. 140) na kujadili wimbo huu unafundisha nini kuhusu nguvu ya sala.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Alika washiriki wa darasa kutafakari sababu za sisi kushindwa wakati mwingine kushiriki injili na watu wengine. Pendekeza kwamba kujifunza Matendo ya Mitume 16–21 kunaweza kuwasaidia wao kushinda vikwazo ambavyo vinaweza kuwazuia kushiriki injili.
Nyenzo za Ziada
Kupokea ufunuo mstari juu ya mstari
Mzee David A. Bednar alifanya uchunguzi wa yafuatayo kuhusu njia ya Bwana ya ufunuo: “Wengi wetu hasa hudhani tutapokea jibu au mwongozo kutokana na sala zetu za dhati na maombi. Na pia mara nyingi tunategemea kwamba jibu au mwongozo vitakuja bila kuchelewa na kwa mara moja Hivyo, tunakuwa wenye kuamini kwamba Bwana atatupatia jibu kubwa kwa haraka na yote kwa mara moja.. Hata hivyo, mpangilio ambao umeelezewa mara kwa mara kwenye maandiko unapendekeza kwamba tupokee ‘amri juu ya amri, kanuni juu ya kanuni,’ au kwa maneno mengine majibu mengi madogo madogo kadiri ya muda. Kutambua na kuelewa mpangilio huu ni ufunguo muhimu katika kupata mwongozo wa kiungu na usaidizi kutoka kwa Roho Mtakatifu (“Mstari juu ya Mstari, Kanuni juu ya Kanuni,” New Era, Sept. 2010, 3–4).
Mzee Dallin H. Oaks alitoa ushauri huu: “Yatupasa tuchunguze mambo akilini mwetu, kwa kutumia uwezo wetu wa kufikiri tuliopewa na Muumba wetu. Kisha tunapaswa kusali kwa ajili ya mwongozo na kuufanyia kazi kama tutaupokea. Kama hatutapokea mwongozo, tunapaswa kutenda kulingana na maamuzi yetu bora.” (“Nguvu Yetu Yaweza Kuwa Anguko Letu,” Ensign, Oct. 1994, 13–14).
Rais Gordon B. Hinckley alielezea mtazamo wake wa kutumikia Kanisani katika mabaraza ya uongozi:
“Mwanzoni katika kufikiria mambo, kunaweza kuwa na utofauti katika mawazo. Haya yanategemewa. Watu hawa hutoka katika machimbuko mbalimbali. Ni watu wanaojifikiria wenyewe. …
“… Kutoka katika mchakato huu huu wa watu kuongea yaliyo akilini mwao kumetokea mawazo na dhana zilizochujwa na kupepetwa. Lakini sikuwahi kuona kutokubaliana au uadui baina ya Ndugu zangu wa Ukuhani. Bali, nimeona kitu kizuri na cha kupendeza—kuja kwa pamoja, chini ya uongozi shawishi wa Roho Mtakatifu na chini ya nguvu ya ufunuo, mitazamo mbalimbali mpaka kuwepo kwa maelewano kamili na makubaliano timilifu. Mpaka kufikia hapo ndipo utendaji kazi hufanywa. Hilo, nashuhudia, huwakilisha roho ya ufunuo iliyojidhihirisha tena na tena katika kuongoza kazi hii ya Bwana” (“Mungu yu katika usukani,” Ensign, Mei 1994, 54, 59).