Njoo, Unifuate
Juni 10–16. Mathayo 26; Marko 14; Luka 22: Yohana 18: “Si Kama Nitakavyo Mimi Bali Utakavyo Wewe”


“Juni 10-16 Mathayo 26: Marko 14; Luka 22; Yohana 18: ‘Si kama Nitakavyo Mimi Bali Utakavyo Wewe’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

“Juni 10-16 Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; Yohana 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Karamu ya Mwisho

Na Ilikuwa Usiku, na Benjamin McPherson

Juni 10–16

Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; Yohana 18

“Si kama Nitakavyo Mimi, Bali kama Utakavyo Wewe”

Soma Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; na Yohana 18, na utafakari mawazo na misukumo ambavyo inakuja akilini mwako. Nini jumbe gani washiriki wako wa darasa wanahitaji kujifunza?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Himiza Kushiriki

Waalike washiriki wa darasa washiriki kitu fulani walichojifunza wiki hii ambacho kiliwasaidia kupata maana zaidi katika sakramenti. Walifanya nini na iliathiri vipi uzoefu wao kushiriki sakramenti?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 26:26–29; Luka 10:19–20

Sakramenti ni fursa ya daima kumkumbuka Mwokozi.

  • Kwa nini Mwokozi alianzisha sakramenti? Kwa nini tunapokea sakramenti kila wiki? Ni majibu gani wanayoweza kupata washiriki wa darasa katika Mathayo 26:26–29; Luka 22:7–20; Mafundisho na Maagano 20:75–79; na Kweli kwa Imani, 147–49? Kwa mfano, Kweli kwa Imani inafundisha kwamba sakramenti inadhimisha dhabihu ya Kristo, ambayo ilikamilisha sheria ya Musa. Mnaweza pia kutaka kusoma sala za sakramenti kama darasa na waombe washiriki wa darasa kutambua maagano tunayofanya kama sehemu ya ibada hii. Tunaweza kumsaidia vipi mtu mwingine aelewe nini maana ya masharti haya? Jinsi gani ushiriki wetu katika sakramenti unaathiri chaguzi tunazofanya wiki nzima.

    Picha
    Msichana akipokea sakramenti

    Tunapopokea sakramenti, tunafanya upya tena maagano yetu.

  • Washiriki wa darasa wana uwezekano wa kunufaika kwa kusikiliza mawazo ya kila mmoja wao kuhusu jinsi ya kumkumbuka Mwokozi wakati wa sakramenti na wiki nzima (ona Mafundisho na Maagano 6:36–37). Labda ungewaalika washiriki kile kinachowasaidia wao na familia zao kumkumbuka Mwokozi na kuyashika maagano yao. Ni aya gani kutoka kwenye somo la wiki hii zimepanua staha yetu kwa ajili ya sakramenti? Kwa mawazo mengine kuhusu jinsi ya kumkumbuka Mwokozi, ona Gerrit W. Gong, “Daima Kumkumbuka.” Ensing au Liahona, Mei, 2016, 108–11).

  • Majadiliano yanaweza kuwa nafasi mzuri kuchunguza pamoja na washiriki wa darasa ishara za sakramenti. Jinsi gani ishara hizi zinatusaidia kulenga kwa Mwokozi wakati wa ibada? Ishara hizi zinatufundisha nini kumhusu Yeye na uhusiano wetu na Yeye.

  • Mwishoni mwa majadiliano yenu kuhusu sakramenti, unaweza kuwapa washiriki wa darasa muda mfupi kutafakari na kuandika nini wanahisi wamepata mwongozo wa kufanya ili kujitayarisha kwa sakramenti wiki ijayo. Kuongeza kwenye uzoefu huu wa kiroho, fikiria kucheza wimbo wa sakramenti wakati washiriki wa darasa wanatafakari.

Mathayo 26:36–46

Tunakuwa zaidi kama Kristo tunapochagua kutoa mapenzi yetu kwa yale ya Baba.

  • Mfano wa Mwokozi wa kujitoa kwa mapenzi ya Baba unaweza kuwasaidia washiriki wako wa darasa wakati wanahitaji kufanya hivyo hivyo. Kuanzisha majadiliano, unaweza kumwalika kila mshiriki wa darasa kushiriki wakati alipojitoa mwenyewe kwa kitu fulani alichojua Mungu alitaka afanye. Nini kilichowahamasisha kufanya vitu hivyo? Alika darasa lisome Mathayo 26:36–42 na litafakari kwa nini Mwokozi alikuwa tayari kutoa mapenzi Yake kwa yale ya Baba yake. Jinsi gani kutoa mapenzi yetu kwa Mungu hatimaye kunatubariki?

  • Kuichunguza kanuni ya kujitoa kwa Mungu, unaweza kuomba nusu ya darasa isome Mosia 3:19 na nusu ingine isome 3 Nefi 9:20. Aya hizi zinafundisha nini kuhusu kile inamaanisha kujitoa kwa Mungu? Jinsi gani tunavyojitoa? Washiriki wa darasa watatafakari jinsi wanavyoweza kutoa mapenzi yao kwa Mungu katika wiki ijayo. Maelezo kutoka Mzee Neal A. Maxwell katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza pia kuongezea kwenye majadiliano yetu.

Mathayo 26:20–22, 31–35

Lazima tuyachunguze maisha yetu wenyewe kuamua jinsi maneno ya Bwana yanavyotumika kwetu.

  • Tunasikia hadithi nyingi za injili katika maisha yetu, lakini wakati mwingine inashawishi kusadiki masomo hayo yanatumika sanasana kwa watu wengine. Majadiliano kuhusu Mathayo 26 yanatusaidia kushinda mwenendo huu. Kuanzisha mazungumzo haya, unaweza kugawa darasa katika majozi na kumuomba mmoja katika kila jozi kusoma Mathayo 26:20–22 na yule mwingine akisoma aya 31–35. Waalike walinganishe mijibizo ya wafuasi katika hizi simulizi mbili. Ni masomo gani tunayoweza kujifunza kutokana na jinsi wafuasi walitumia maneno ya Mwokozi kwao wenyewe? Kujifunza zaidi, ona marejeo ya Rais Dieter F. Uchtdorf kwa Mathayo 26:21–22 katika ujumbe wake “Ni Mimi, Bwana?” (Ensign au Liahona, Nov. 2014, 56-59).

Mathayo 26:36–46

Yesu Kristo alifanya Upatanisho usio na mwisho kwa ajili yetu.

  • Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki umaizi walioupata kuhusu Upatanisho wa Yesu Kristo katika kujifunza binafsi au familia.

  • Mathayo 26 inaelezea nini kilitokea Gethsemane, lakini washiriki wa darasa lako wanaelewa umuhimu wake katika maisha yao? Ili kuwasaidia, labda unaweza kuandika ubaoni maswali kama Nini kilitokea Gethsemane? na Kwa nini ni muhimu kwangu? Washiriki wa darasa wanaweza kufanya kazi kibinafsi au katika vikundi vidogo kupata majibu katika Mathayo 26:36–46; Alma 7:11–13; na Mafundisho na Maagano 19:16–19. Wanaweza pia kupata majibu katika ujumbe wa Mzee C. Scott Grow “ The Miracle of the Atonement” (Ensign au Liahona, Mei, 2011, 108-10).

  • Katika Kitabu cha Mormoni, Yakobo anauita Upatanisho wa Yesu Kristo “upatanisho usio na mwisho” (2 Nefi 9:7). Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kile hii inamaanisha, unaweza kushiriki mafundisho ya Rais Russell M. Nelson katika “Nyenzo za Ziada” na waombe washiriki wa darasa kuorodhesha njia ambazo athari za dhabihu ya Mwokozi inaweza kufikiriwa hazina kikomo. Wanaweza pia kusoma maandiko yafuatayo na kuongeza kwenye orodha yao: Waebrania 10:10; Alma 34:10–14; Mafundisho na Maagano; na Musa 1:33. Tunawezaje kuonyesha shukrani zetu kwa kile Mwokozi amefanya kwa ajili yetu?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kuendelea kusoma, unaweza kuwauliza kama wanajua ni vitu gani saba Yesu alivisema wakati akiwa msalabani. Waambie kwamba watagundua nini Mwokozi alisema kwa kusoma Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; na Yohana 19.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mathayo 26; Marko 14; Luka 22; Yohana 18

Bible videos (LDS.org).

“Karamu ya Mwisho,” “Mwokozi Anateseka Gethsemane”

Kutoa mapenzi yetu kwa Baba.”

Mzee Neal A. Maxwell alifundisha: “Unapotoa mapenzi yako kwa Mungu, unampa Yeye kitu pekee unacho weza kwa kweli kumpa Yeye ambacho ni chako halisi kumpa. Usingoje muda mrefu kupata madhabahu au kuanza kuweka zawadi ya mapenzi yako juu yake” (“Remember How Merciful the Lord Hath Been,” Ensign au Liahona, Mei 2004, 46).

Upatanisho usio na kikomo.

Rais Russell  M. Nelson alifundisha:

“Upatanisho wa [Yesu Kristo] hauna kikomo—hauna mwisho. Ulikuwa pia hauna kikomo kwa vile wanadamu wataokolewa kutoka kwenye kifo kisicho kuwa na mwisho. Ulikuwa hauna mwisho kwa hali ya mateso Yake makali. Ulikuwa hauna mwisho katika wakati, ukikomesha mfano wa kale wa sadaka ya wanyama. Ulikuwa hauna mwisho katika mawanda—ulikuwa ufanyike mara moja kwa ajili ya wote. Na rehema ya Upatanisho imepanuliwa siyo tu kwa idadi ya watu isiyo na kikomo, bali pia kwa idadi kubwa dunia zisizo na kikomo zilizoumbwa Naye. Ulikuwa hauna mwisho hata kuzidi kiwango chochote cha upimaji au uelewa wa uelewa wa binadamu.

“Yesu alikuwa ndio mtu pekee aliyeweza kutoa upatanisho huu usio na mwisho, kwa vile alizaliwa na mama mwenye mwili unaokufa na baba mwenye mwili usiokufa. Kwa sababu ya haki hiyo ya kipekee ya kuzaliwa, Yesu alikuwa kiumbe kikamilifu” (“The Atonement” Ensign, Nov. 1996, 35).

Rais Heber J. Grant alifundisha: “Sio tu Yesu alikuja kama zawadi ya wote, Alikuja kama toleo binafsi. … Kwa ajili kila mmoja wetu Yeye alikufa Kalvari na damu Yake itatuokoa sisi kwa masharti. Sio kama mataifa, jamii, vikundi, bali kama watu binafsi” (“A Marvelous Growth,” Juvenile Instructor, Dec.1929, 697).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tazama kupitia Macho ya Mungu. Jitahidi kuwaona washiriki wa darasa lako kama Mungu anavyowaona, na Roho atakuonyesha thamani yao tukufu na uwezo wao. Utakapofanya hivi, utaongozwa katika juhudi zako za kuwasaidia wao (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 6).

Chapisha