Njoo, Unifuate
Novemba 11–17. Waebrania 7–13: ‘Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo’


Novemba 11–17. Yohana 7-13 ‘Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019.)

Novemba 11–17. Waebrania 7–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Melkizedeki akimpa baraka Abram

Melkizedeki akimbariki Abram, na Walter Rane

Novemba 11–17 .

Waebrania 7–13

“Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo”

Unaposoma Webrania 7–13, tafakari ni ujumbe gani wa Bwana ulikuwa kwa ajili ya Waebrania Watakatifu. Pia angalia ujumbe Wake kwako na kwa watu unaowafundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kabla ya kuanza darasa, alika washiriki wachache kuja wakiwa wamejiandaa kushiriki mistari kutoka Waebrania 7–13 ambayo iliwasaidia “kusonga karibu na [Mungu] kwa moyo wa kweli kwa utiifu wa imani”

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Waebrania 7:1–22

Kuishi kwa kustahiki maagano na baraka za Ukuhani wa Melkizedeki hupelekea katika kuinuliwa.

  • Njia mojawapo ya kuchunguza sura hii ni kwa kuwaalika washiriki wa darasa kuandika kwenye ubao baadhi ya kauli za kweli kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki (kwa mawazo, wangeweza kusoma “Ukuhani wa Melchizedeki ” katika Kweli kati Injili, 101–2). Kisha wangeweza kutafuta kutoka Waebrania 7:1–22 kwa ajili ya virai kusaidia kauli zilizopo ubaoni. Wangeweza pia kutumia Mwongozo wa Mada au Mwongozo wa Maaandiko ili kupata maandiko saidizi.

  • Katika Waebrania 7:11 Paulo aliuliza, “kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?” Kwa maneno mengine, kwa nini tunahitaji Ukuhani wa Melkizedeki kwa nyongeza kwenye Ukuhani wa Haruni? Labda washiriki wa darasa wangeweza kutafuta majibu katika Kweli kwa Injili, “Ukuhani wa Haruni” na “Ukuhani wa Melkidezeki.” Ungeweza pia kuwaalika kufikiria baraka ambazo tunazo kwa sababu ya kuhani hizi mbili (ona pia nukuu toka kwa Dada Sheri L. Dew katika “Nyenzo za Ziada”). Ni kwa namna gani washiriki wa darasa wamepata uzoefu wa baraka hizi?

Waebrania 8–10

Ibada za kale na za sasa huelekeza kwa Yesu Kristo.

  • Japokuwa hatutoi sadaka za mnyama wa kuteketeza, tunashiriki katika ibada leo, ambazo, katika njia sawa na hiyo, zinaelekeza nafsi zetu kwa Kristo na kutoa njia iliyoruhusiwa ambayo kupitia kwayo baraka na nguvu za mbinguni hupita kufika katika maisha yetu binafsi” (David A. Bednar, “Daima Tunza Ondoleo la Dhambi Zako,” Ensign au Liahona, Mei 2016, 60). Labda mngeweza kuchunguza kwa pamoja baadhi ya maelezo kuhusu ibada za kale zilizoelezewa katika Waebrania 8–10 na maana zake kiishara. Kwa mfano, je, damu ya ngombe dume na mbuzi huwakilisha nini? (ona Waebrania 9:13–14). Kuhani mkuu humwakilisha nani? (ona Waebrania 9:24–26). Video “Dhabihu na Sakramenti” (LDS.org) ingeweza kusaidia. Ni kwa namna gani ibada za sasa zimetubariki na kutuelekeza kwa Yesu Kristo? Tunaweza kufanya nini ili kuweza kuzifanya ibada hizi kuwa na maana zaidi na kuzingatia kwa Mwokozi?

Waebrania10:34–3811.

Imani huitaji kuamini katika ahadi za Mungu.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa mafundisho ya Paulo kuhusu imani, ungeweza kuanza kwa kuwaomba wafikirie kuhusu jinsi gani wanaweza kuielezea imani katika sentensi moja. Kisha soma na mjadili kama darasa maana iliyotolewa katika Waebrania 11:1. Kisha ungeweza kugawanya darasa katika makundi madogo na kuwapa kazi kila kundi ya kujifunza juu ya mtu mmoja kati ya walioorodheshwa katika Waebrania 11. Washiriki wa darasa wangeweza kutumia muhtasari au Mwongozo wa Maandiko kurejea uzoefu wa watu katika Agano la Kale, na kisha mwakilishi toka kila kundi angeweza kushiriki na darasa kile ambacho kundi lilipata. Ni kwa namna gani watu hao walionyesha kuhisi “uhakika wa mambo yatarajiwayo”? (Tafsiri ya Joseph Smith, Waebrania 11:1 [katika Waebrania 11:1, muhtasari b]). Ni mifano gani mingine ya watu waaminifu ambao washiriki wa darasa wanaweza kushiriki? Ni wakati gani tulitumia imani katika ahadi ambazo bado hazijatimizwa?

  • Ingekuwa ya kufurahisha kutengeneza mchezo kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza kuhusu imani kutoka Waebrania 11. Kwa mfano, ungeweza kugawanya darasa katika timu mbili na kuuliza maswali kuhusu imani ambayo yanajibiwa katika Waebrania 11 (ona “Nyenzo za Ziada” kwa mifano). Timu ya kwanza kupata jibu likisaidiwa na maandiko inapata alama. Waombe washiriki wa darasa kujadili walichojifunza kutoka kwenye mistari hii ambacho kilitawasaidia kuelewa imani vizuri zaidi.

  • Baada ya kujifunza mafundisho ya Paulo juu ya imani katika Waebrania 10:34–3811, je, washiriki wa darasa wangenufaika na kujifunza kuhusu imani kutoka kwenye nyenzo zingine? Ungeweza kuwapa kazi baadhi ya washiriki wa darasa kabla ya muda kuchunguza swali kuhusu imani kama lifuatalo: Imani ni nini? Ni kwa namna gani tunakuza imani? Ni katika njia zipi tunabarikiwa tunapotumia imani? Nini hutokea tunapochagua kutotumia imani? Kisha, katika darasa, wangeweza kushiriki walichojifunza. Au ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kufanya kazi kwa pamoja katika makundi kupata majibu. Baadhi ya nyenzo ambazo wangeweza kutumia zinajumuisha Alma 32:21–43; Etheri 12; “Imani Katika Yesu Kristo,” Mada za Injili, topics.lds.org; na Kamusi ya Biblia, “Imani.” Baada ya washiriki wa darasa kushiriki walichoijifunza, waombe kufikiria nini wangeweza kufanya kuimarisha imani zao. Waalike wanafunzi wachache kushiriki mawazo yao.

  • Ushauri kwa Watakatifu Waebrania ambao walikuwa wakijaribiwa ili “waanguke” kutoka imani yao unaweza kuwa wa thamani kwa washiriki wa darasa ambao wanaweza kuwa wanasumbuka na shuhuda zao. Ili kugundua ushauri huu, washiriki wa darasa wangeweza kusoma Waebrania 10:34–38 na kauli ya Mzee Jeffrey R. Holland katika “Nyenzo za Ziada.” Ni kwa nini watu duniani leo wanatupilia mbali kujiamini kwao (ona Waebrania 10:35) katika Bwana na injili Yake? Nini tunaweza kufanya ili kujenga na kuendeleza imani na kujiamini ili “kupokea [ahadi za Mungu]”? Waebrania 10:38. Video “Vitu Vizuri Vijavyo” na “Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo” (LDS.org) zingeweza kuusindikiza mjadala huu

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Washiriki wa darasa wanaweza kuwa wanajua kuhusu uzoefu wa Joseph Smith wa kusoma Yakobo 1:5, ambao ulipelekea Ono la Kwanza. Waalike kutafuta umaizi mpya kuhusu Yakobo 1:5 wakati wakisoma wiki hii katika muktadha mpana wa ujumbe wa Yakobo.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Waebrania 7–13

Maswali kuhusu imani kutoka Waebrania 11.

Baraka za Ukuhani wa Melkizedeki zinapatikana kwa wote.

Dada Sheri L. Dew, aliyekuwa mshauri katika Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa akina Mama, alisema: “baraka za ukuhani zinapatikana kwa kila mwanaume na mwanamke mtakatifu. Wote tunaweza kupokea Roho Mtakatifu, kupata ufunuo binafsi, na kupata endaumenti hekaluni, ambako tunainuka ‘tukilindwa’ na nguvu. Nguvu ya ukuhani huponya, hulinda, na huwalinda wema wote dhidi ya nguvu za giza” (“Si Vema Mwanamume au Mwanamke Awe Pke yake,” Ensign, Nov. 2001, 13).

“Kwa hivyo usitupe kujiamini kwako.”

“Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

“Hakika ni vigumu—kabla hujajiunga na Kanisa, wakati unajaribu kujiunga, na baada ya kujiunga. Hivyo ndivyo mara zote ilivyokuwa, Paulo alisema, lakini usikate tamaa. Usihangaike na kurudi nyuma. Usipoteze kujiamini kwako. Usisahau ulivyohisi hapo awali. Usiache kuamini uzoefu uliowahi kuwa nao. …

Katika kila chaguzi muhimu kuna onyo na mambo ya kufikiria, lakini awali kunapokuwa na mwangaza, kuwa makini na majaribu ya kukurudisha nyuma kutoka kwenye vitu vizuri. Kama ilikuwa sahihi ulipoomba na kuamini na kuishi kwa hilo, ni sahihi hata sasa. Usikate tamaa wakati shinikizo linapokuwa kubwa. … Kabiliana na shaka zako. Shida woga wako. ‘Kwa hivyo, usitupe kujiamini kwako.’ Baki katika njia na uone uzuri wa maisha ukifunuliwa kwako” (Kwa hivyo Usitupe Ujasiri Wako,” Ensign, Machi. 2000, 6–11).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Nenda kwenye Maandiko kwanza. Maandiko lazima yawe chanzo cha msingi cha maandalizi na kujifunza kwako. Maneno ya manabii wa sasa yanaweza kujaliza maandiko kwenye vitabu vitakatifu (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 17).

Chapisha