Njoo, Unifuate
Novemba 4–10. Waebrania 1–6: ‘Yesu Kristo, ‘Sababu ya Wokovu wa Milele’’


Novemba 4–10. Waebrania 1–6: ‘Yesu Kristo, ‘Sababu ya Wokovu wa Milele’’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

Novemba 4–10. Waebrania 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Kristo amesimama na msichana mdogo na mwanaume

Siku ya Pentekoste, na Sidney King

Novemba 4–10.

Waebrania 1–6

Yesu Kristo, “Sababu ya Wokovu wa Milele”

Fikiria kushiriki na washiriki wa darasa lako baadhi ya misukumo ambayo umepokea kutoka kwa Roho Mtakatifu kuhusu Waebrania 1–6. Kwa kufanya hivyo unaweza kuwahimiza kutafuta misukumo yao wenyewe wakati wakijifunza maandiko.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Baadhi ya washiriki wa darasa ambao hawashiriki mara nyingi katika darasa, wanaweza kuhitaji mwaliko maalum na muda kidogo ili kujiandaa. Ungeweza kuwasiliana na wachache kati yao siku moja au mbili kabla na kuwaomba waje wakiwa wamejiandaa kushiriki mstari kutoka Waebrania 1–6 ambao ni wa maana kwao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Waebrania 1–5

Yesu Kristo ni “sababu ya wokovu wa milele.”

  • Ni kwa namna gani unaweza kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki maandiko yenye maana kwao kuhusu Yesu Kristo ambayo waliyapata katika kujifunza kwako binafsi na katika familia wiki hii? Fikiria kutengeneza safu tano kwenye ubao zikiwakilisha sura tano za kwanza za Waebrania. Waalike washiriki wa darasa kuandika katika safu husika virai kutoka kwenye sura hizi ambavyo viliwafundisha kuhusu Yesu Kristo na mstari ambapo kirai hicho kinapatikana. Ni kwa namna gani kujua vitu hivi kuhusu Mwokozi kunaathiri imani yetu Kwake na utayari wa Kumfuata?

  • Waebrania 1–5 hutumia taswira mbali mbali kumwelezea Mwokozi. Labda ungeweza kutumia taswira hizi kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kwa kina kuhusu kazi Yake. Kwa mfano, ungeweza kuwasiliana na baadhi ya washiriki siku chache kabla na kuwaomba waje darasani na kitu kinachowakilisha moja kati ya maelezo ya Yesu Kristo au Kazi yake kutoka Waebrania 1–5 (ona hasa Waebrania 1:3; 2:10; 3:1, 6; 5:9). Wangeweza kulielezea darasa nini vitu vyao vinafundisha kuhusu Yesu Kristo na kusoma mstari unaoendana kutoka Waebrania. Ni kwa namna gani kujua kweli hizi kuhusu Mwokozi huathiri maisha yetu?

Waebrania 2:9–18; 4:12–16; 5:7–8

Yesu Kristo aliteseka kwa yote ili kwamba Aweze kuelewa na kuwasaidia wale wanaoteseka.

  • Kunaweza kuwa na washiriki wa darasa lako ambao wanateseka kwa majaribu na wakati mwingine wanahisi kusahaulika au kutokuwa na tumaini. Labda mjadala wa Waebrania 2:9–18; 4:12–16; 5:7–8 ungeweza kujenga imani yao kwamba wanaweza kumgeukia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kwa ajili ya msaada. Njia mojawapo ya kuanzisha mjadala huo ni kwa kuwaalika washiriki wa darasa kumfikiria mtu fulani ambaye wanamjua anateseka na anayeweza kupoteza tumaini. Ni kweli zipi wanazozipata katika mistari hii ambazo wangeweza kushiriki na mtu huyo? Washiriki wa darasa pia wangeweza kushiriki ni kwa namna gani Mwokozi amewafariji na kuwasaidia. Fikiria kushiriki nukuu toka kwa Rais John Taylor katika “Nyenzo za Ziada” kama sehemu ya mjadala.

  • Waebrania 2:9–18; 4:12–16 inaweza pia kusaidia watu ambao wanayaona masumbuko ya dunia na kujiuliza kama Mungu anayaona au hata kujali. Labda washiriki wa darasa wangeweza kuchunguza mistari hii ili kupata kweli ambazo zingeweza kusaidia katika maswali kama hayo. Mistari hii inafundisha nini kuhusu jinsi Mwokozi anavyoitikia katika mateso ya binadamu? Inaweza pia kusaidia kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki mifano kutoka maandiko ambapo watu walisaidiwa na Yesu Kristo katika masumbuko yao (ona “Nyenzo za Ziada”) au onyesha video “Milima ya Kupanda” (LDS.org). Jadilini kwa pamoja nini tunajifunza kuhusu jinsi Mwokozi anaweza kutusaidia wakati tukikumbana na changamoto ngumu.

Waebrania 3:7–4:2

Baraka za Mungu zinapatikana kwa wote ambao “hawashupazi mioyo [yao].”

  • Waebrania 3 na 4 zina ombi kwa Watakatifu la kutoshupaza mioyo yao na hivyo kukataa baraka ambazo Mungu alitaka kuwapa. Wakati wewe na darasa lako mkisoma Waebrania 3:7–4:2, jadilini njia ambazo uzoefu wa Waisraeli wa zamani ungeweza kutumika kwetu leo, kama zilivyotumika kwa Waebrania katika Kanisa la mwanzo (fikiria kurejea nyenzo za kujifunza kuhusu mistari hii katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia). Nini husababisha watu kushupaza mioyo yao katika siku zetu? Tunaweza kufanya nini ili kuweka mioyo yetu kuwa laini na ya kuitikia mapenzi ya Bwana? (ona Etheri 4:15; Alma 5:14–15).

Waebrania 5:1–5

Wale wanaohudumu katika ufalme wa Mungu lazima waitwe na Mungu.

  • Si washiriki wote wa darasa lako ni watu wenye ukuhani, lakini ujumbe kutoka Waebrania 5 kuhusu wenye ukuhani kwa kuitwa na Mungu unatumika kwa wote ambao wamepokea miito Kanisani. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa nini humaanishwa kwa “kuitwa na Mungu kama Haruni,” fikiria kuwaalika kurejea tukio la Haruni akipokea wito wake katika Kutoka 4:10–16, 27–31; 28:1. Ni umaizi gani kutoka kwenye maelezo haya hutusaidia kuelewa Waebrania 5:1–5? Ni lini washiriki wa darasa, ikijumuisha viongozi wa kata, walipokea uthibitisho kwamba mtu fulani aliitwa na Mungu kutimiza wito maalum? Ni kwa namna gani uthibitisho huo unawasaidia kumkubali zaidi mtu fulani katika wito wake? (Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kutotoa taarifa nyeti.) Kunaweza pia kuwa na washiriki wa darasa ambao wangeweza kushuhudia kwamba Mungu aliwapa msukumo walipokuwa wakitimiza miito yao.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Je, washiriki wa darasa lako wamewahi kuhisi kuwa “wageni na wasafiri juu ya nchi” (Waebrania 11:13) kwa sababu imani zao zilikuwa tofauti na za wale wanaowazunguka? Waambie kwamba wanaposoma Waebrania 7–13, watapata mifano ya watu ambao kwa uaminifu walipokea na kukumbatia ahadi za Mungu japokuwa wengi wa waliowazunguka hawakuwa na imani.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Waebrania 1–6

Yesu Kristo anajua ni jinsi gani kupitia mateso kulivyo.

Rais John Taylor alifundisha: “Ilikuwa wakati Mwokozi alipokuwa duniani, kwamba lazima ajaribiwe katika kila kitu kama sisi,’ na ‘aguswe na hisia za udhaifu wetu,’ [ona Waebrania 4:15] ili kuweza kuelewa udhaifu na nguvu; ukamilifu na mapungufu ya asili dhaifu ya mwanadamu aliyeanguka; na baada ya kukamilisha hiki kitu alichokuja duniani kukifanya, baada ya kukabiliana na unafiki, uovu, udhaifu, na upumbavu wa mwanadamu—baada ya kukutana na jaribu katika mwonekano wake wote, na kushinda, amekuwa Kuhani mkuu mwaminifu [ona Waebrania 2:17] kufanya njia kwa ajili yetu katika ufalme usio na mwisho wa Baba. Anajua jinsi ya kukadiria, na kuweka thamani halisi ya asili ya binadamu, kwake, kwa kuwekwa katika sehemu sawa na sisi, anajua jinsi ya kuchukulia udhaifu wetu na mapungufu, na anaweza kuelewa kikamilifu kina, nguvu na uwezo wa mateso na majaribu ambayo wanadamu wanatakiwa kukabiliana nayo katika dunia hii, na hivyo kwa uelewa na kwa uzoefu, anaweza kuyachukulia kama baba na kaka mkubwa” (Teachings of Presidents of the Church: John Taylor [2001], 204–5).

Mifano ya maandiko ya watu waliofarijiwa na Yesu Kristo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tengeneza mazingira ya kiroho. Wakati ukiendeleza mazingira tulivu, ya upendo katika darasa lako, Roho anaweza kiurahisi kugusa mioyo ya wale unaowafundisha. Unaweza kufanya nini ili kualika ushawishi wa Roho katika darasa lako? Je, ungeweza kupanga viti au maandiko au muziki ili kumwalika Roho? (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 15.)

Chapisha