“Novemba 18–24. Yakobo: ‘Iweni Watendaji wa Neno, Wala Si Wasikiaji Tu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)
“Novemba 18–24. Yakobo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019
Novemba 18–24 .
Yakobo
“Iweni Watendaji wa Neno, Wala Si Wasikiaji Tu”
Kabla ya kusoma muhtasari huu, soma waraka wa Yakobo na kuwa makini na ushawishi unaopata. Je, ni kanuni gani unazipata ambazo zingebariki na kuwainua washiriki wa darasa lako? Rejea muhtasari huu kwa ajili ya mawazo ya kufundisha ya ziada.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waalike washiriki wa darasa kushiriki mistari kutoka Yakobo ambayo imewapa msukumo wa kuwa “watendaji wa neno” (Yakobo 1:22). Kama si ya kibinafsi sana, wangeweza kushiriki kile wanachohisi wanahitaji kufanyia kazi, kibinafsi au kama familia.
Fundisha Mafundisho
Tunapoomba kwa imani, Mungu hutupatia kwa ukarimu.
-
Kanuni zilizofundishwa katika Yakobo 1:5–6 zilimuongoza Joseph Smith katika tukio lililomletea badiliko la kiroho, na zinaweza kutubariki kila mmoja wetu katika njia fulani. Labda ungeweza kuandika maswali kama yafuatayo kwenye ubao na kuwaomba washiriki wa darasa kuyatafakari kimoyomoyo: ni ushawishi gani Yakobo 1:5–6 imekuwa nayo katika maisha yako? Uzoefu wa Joseph Smith kwenye mistari hii ulikufundisha nini kuhusu kutafuta hekima kuhusu maswali yako binafsi? (Ona Joseph Smith—Historia ya 1:10–17. Ni uzoefu gani umekufundisha kwamba “ushuhuda wa Yakobo [ni] wa kweli”? (Joseph Smith—Historia ya 1:26). Waalike washiriki wa darasa kushiriki mawazo waliyonayo baada ya kutafakari maswali haya.
-
Labda washiriki wa darasa wangeweza kuiweka Yakobo 1:5–6 katika maneno yao wenyewe. Ni kwa namna gani hii inawasaidia kuelewa mistari hii vizuri zaidi?
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kukumbuka kwamba Mungu ameahidi kutoa kwa ukarimu kwa watoto Wake wakati wanapomsogelea Yeye katika sala, waombe washiriki wa darasa kusimulia matukio ambapo ahadi katika Yakobo 1:5–6 ilitimizwa katika maisha yao. Je, wamejifunza nini wakati walipomwuliza Baba wa Mbinguni kuthibitisha juu ya maswali kuhusu ukweli wa injili?
Subira ya uvumilivu hatimaye huleta ukamilifu.
-
Ili kuanza mjadala juu ya mafundisho ya Yakobo kuhusu uvumilivu katika mistari hii, ungeweza kualika mshiriki wa darasa kusimulia juu ya tukio ambapo walitakiwa kuwa wavumilivu na walijifunza nini kutokana na tukio hilo. Kisha wangeweza kutafuta toka Yakobo 1:2–4; 5:7–11 kwa ajili ya kanuni ambazo wanaweza kuzitumia kwenye uzoefu wao. Wangeweza pia kupata kanuni za kutumia katika video “Continue in Patience” (LDS.org) ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf “Endelea Katika Uvumilivu” (Ensign au Liahona, Mei 2010, 56–59). Kwa nini uvumilivu ni muhimu tunapojitahidi kuelekea kwenye ukamilifu? Je, ni kitu gani kimewasaidia washiriki wa darasa kuendeleza subira katika maisha yao?
“Imani pasipo matendo imekufa.”
-
Njia mojawapo ya kujadili mafundisho ya Yakobo kuhusu imani na matendo ingeweza kuwa kwa kuligawanya darasa lako katika makundi mawili—moja kuchunguza kwa nini imani inahitaji matendo na lingine kwa nini matendo yanahitaji imani. Kufanya hivi, wangeweza kusoma Mathayo 7:21–23; Yakobo 1:6–8, 21–25; 2:14–26; and Joseph Smith—Historia ya 1:19. Kisha kila kundi lingeweza kushiriki walichopata na kujadili kwa nini vyote imani na matendo ni muhimu.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari kwa kina zaidi kirai kikumbukwacho “Imani pasipo matendo imekufa” (Yakobo 2:26), ungeweza kuandika sentensi ifuatayo kwenye ubao: Imani bila matendo ni kama bila . Waalike washiriki wa darasa kufikiria njia za ubunifu ili kukamilisha sentensi, na waache waandike mawazo yao kwenye ubao. Pia wangeweza kunufaika kwa kufanya shughuli hii katika jozi au katika vikundi vidogo. Hadithi iliyosimuliwa na Rais Dieter F. Uchtdorf katika “Nyenzo za Zaida” ingeweza kuongezea uelewa wao wa kanuni hii. Tunaweza kufanya nini ili kuendelea kutumia imani katika Yesu Kristo?
Kama wafuasi wa Yesu Kristo, hatuna budi kuwapenda watu wote, bila kujali hali zao.
-
Ili kuwahamasisha washiriki wa darasa kuonyesha upendo kama wa Kristo kumpenda mtu bila kujali hali za wengine au mwonekano wao wa nje, ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kuchukua zamu kusoma mistari kutoka Yakobo1:9–11; 2:1–10; 5:1–6. Jadili maswali kama yafuatayo: Je, inamaanisha nini kuwa na “heshima kwa watu”? (Yakobo 2:9). Je, ni kwa nini wakati mwingine tunawatendea wale wenye fedha, umashuhuri, au uwezo tofauti na wale ambao hawana? Je, ni kwa namna gani tunaweza kuepuka kuwatendea wengine tofauti kulingana na hali walizo nazo? Ni kwa njia gani mfuasi wa kweli wa Mwokozi ni tajiri wa kweli kuliko wote? (ona Yakobo 2:5).
Maneno tunayoyatumia yana nguvu ya kuwaumiza wengine au kuwabariki.
-
Taswira ya nguvu ambayo Yakobo aliitumia inatoa kumbusho la msaada na hamasa ya kutumia maneno—yote kwa kuongea na kuandika—katika kuwainua wengine. Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kupitia Yakobo 3 wakitafuta taswira ambayo inaelezea kwa jinsi gani lugha inatumika kuumiza au kuwabariki wengine; baadhi ya washiriki wa darasa wanaweza kufurahia kuchora picha za taswira hizi. Je, ni kwa namna gani taswira hizi zinaelezea maelezo ya Yakobo katika sura hii? Kwa mfano, ni kwa namna gani maneno yetu yanaweza kuwa kama moto? Je, ni taswira gari washiriki wa darasa wanaweza kufikiria ili kuonyesha nguvu chanya ambayo lugha inaweza kuwa nayo. Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kutafakari ni kwa namna gani wanaweza kutumia ushauri wa Yakobo.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kusoma 1 na 2 Petro, waalike kutafuta mafundisho katika nyaraka hizo ambayo yanaeleweka vizuri zaidi kwa sababu ya Urejesho wa injili. Je, ni kwa namna gani mafundisho haya yanashuhudia kuhusu misheni ya Joseph Smith?
Nyenzo za Ziada
Imani na Matendo
Rais Dieter F. Uchtdorf alifundisha:
“Kuna hekaya ya kale ya Kiyahudi kuhusu mtengeneza sabuni ambaye hakumwamini Mungu. Siku moja akiwa anatembea na rabi, alisema, ‘Kuna kitu nisichoweza kukielewa. Tumekuwa na dini kwa maelfu ya miaka. Lakini kila unakoangalia kuna maovu, ufisadi, udanganyifu, udhalimu, maumivu, njaa, na vurugu. Inaonekana kwamba dini haijausaidia ulimwengu kabisa. Hivyo nakuuliza wewe, ina uzuri gani?”
“Rabi hakujibu kwa muda bali aliendelea kutembea na mtengeneza sabuni. Hatimaye walikaribia uwanja wa michezo ambapo watoto, wakifunikwa na vumbi, walikuwa wanachezea udongo.
“‘Kuna kitu sikielewi,’ rabi alisema. ‘Waangalie wale watoto. Tumekuwa na sabuni kwa maelfu ya miaka, na bado wale watoto ni wachafu. Je, uzuri wa sabuni ni nini?’
“Mtengeneza sabuni akajibu, ‘Lakini rabi, si sahihi kuilaumu sabuni kwamba watoto hawa ni wachafu. Sabuni inabidi itumike kabla haijatimiza malengo yake.’
Rabi akatabasamu na kusema, ‘Barabara’ (“Wenye Haki Wataishi Kwa Imani,” Ensign au Liahona, Apr. 2017, 4)