“Novemba 25–Disemba 1. 1 na 2 Petro: ‘Furahini kwa Furaha Isiyoneneka na Iliyojaa Utukufu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)
“Novemba 25–Disemba 1. 1 na 2 Petro 2–16,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019
Novemba 25–Disemba 1
1 na 2 Petro
“Furahini kwa Furaha Isiyosemeka na Iliyojaa Utukufu”
Kumbuka kwamba lengo lako ni kufundisha watu, na si tu kuwasilisha somo. Wakati ukisoma Waraka wa Petro, fikiria kuhusu mshiriki mmoja wa darasa. Ni kanuni ipi itawasaidia kujenga imani yao?
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Andika vichwa 1 Petro na 2 Petro kwenye ubao. Wape washiriki wa darasa muda wa kurejea sura hizi, na waalike kuandika chini maneno ya vichwa hivi au virai kutoka kwenye sura ambazo wameona kuwa ni za muhimu. Kisha tumia orodha hiyo kuwaalika watu kushiriki umaizi wao.
Fundisha Mafundisho
1 Petro 1:3–9; 2:19–24; 3:14–17; 4:12–19
Ninaweza kupata furaha katika nyakati za majaribu na mateso.
-
Ili kuwasaidia wale unaowafundisha kuelewa vizuri zaidi na kutumia ushauri wa Petro kuhusu kupata furaha katika mazingira magumu, ungeweza kuwapa washiriki wa darasa vipande vya karatasi na kuwaomba waandike kirai kutoka 1 Petro 1:3–9; 2:19–24; 3:14–17; 4:12–19 ambacho kingeweza kuwasaidia katika nyakati za majaribu na ugumu. Katika upande mwingine wa karatasi wangeweza kuandika kuhusu wakati wa majaribu walipohisi amani au furaha. Wachache waliojitolea wangeweza kushiriki kirai hicho na uzoefu wao, na kisha washiriki wa darasa wangeweza kujadili wamejifunza nini.
-
Njia nyingine ya kurejea ushauri wa Petro katika 1 Petro 1:3–9; 2:19–24; 3:14–17; 4:12–19 ni kwa kuwaalika washiriki wa darasa kufikiria kuhusu mtu fulani ambaye wanamjua anayepitia majaribu. Wape muda katika darasa kuandika barua kwa mtu huyo, ikijumuisha kweli kutoka mistari hii ambazo zingeweza kumuhamasisha mtu huyo (ona pia Mafundisho na Maagano 121:1–8; 123:17). Kisha washiriki wa darasa wangeweza kuongea kuhusu ukweli ambao waliuchagua.
Tumeitwa kuwa “taifa la Mungu.”
-
Kama waumini wa Kanisa la Kristo, tumeitwa kumfuata Yesu Kristo. Hii humaanisha kwamba chaguzi zetu mara nyingi zitatofautiana na za watu wengine. Je, ni kwa namna gani mafundisho ya Petro katika 1 Petro 1:13–20; 2:1–12 yanawasaidia wale unaowafundisha kuelewa zaidi misheni ya Mwokozi na hamu ya kuwa zaidi kama Yeye? Labda ungewaalika washiriki wa darasa kutafuta mistari hii wakiangalia maelezo ya inamaanisha nini kuwa “taifa la Mungu” (1 Petro 2:10) na kisha wajadili wanachokipata. Ungeweza kuelezea kwamba neno “wateule” katika 1 Petro 2:9 humaanisha “kununuliwa” au “kuhifadhiwa” (ona tanbihi f). Hii hutufundisha nini kuhusu jinsi gani Mungu anahisi kuhusu sisi na jinsi gani anataka tuishi?
Injili inahubiriwa kwa wafu ili kwamba waweze kuhukumiwa kwa haki.
-
Waraka wa kwanza wa Petro unajumuisha moja kati ya marejeo machache katika Biblia ya matembezi ya Kristo kwenye ulimwengu wa roho baada ya kifo Chake—tukio ambalo ufunuo wa sasa hutusaidia kuelewa kwa ukamilifu zaidi. Ili kuweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kwa kina juu ya ulimwengu wa roho, ungeweza kuwaalika kusoma maandiko yafuatayo na kuandika ubaoni kile wanachojifunza: Yohana 5:25; 1 Petro 3:18–20; 4:6; Alma 40:7–14, 21; Mafundisho na Maagano 138:11–32.
Kauli zilizotolewa kwenye “Nyenzo za Ziada” huonyesha kwamba matembezi ya Kristo kwenye ulimwengu wa roho yalieleweka na kufundishwa sio tu na Mitume Wake bali pia waalimu wa kale wa Kikristo. Kuelewa kwamba elimu hii ilipotea katika kipindi cha Ukengeufu Mkuu na kurejeshwa katika siku zetu kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuimarisha shuhuda zao juu ya Joseph Smith na Urejesho wa injili.
-
Kujadili 1 Petro 3:18–20; 4:6 kunaweza kusaidia kuwahamasisha washiriki wa darasa kushiriki kikamilifu zaidi katika historia ya familia na kazi ya hekalu. Ili kufanya hivi, ungeweza kuligawanya darasa katika makundi matatu na kuwapa kila kundi moja kati ya maswali haya kuhusu ukombozi wa wafu: Jukumu la Mwokozi ni lipi katika kuwakomboa wafu? Jukumu la wale ambao wamekufa ni lipi—wote waaminifu na wale waliokufa bila kuielewa injili? Jukumu letu sisi ni lipi? Omba kila kundi kurejea 1 Petro 3:18–20; 4:6; Mafundisho na Maagano 128:17–18; 138:11–32, 57–59, wakitafuta majibu kwa ajili ya maswali yao. Omba kila kundi kuelezea kile walichojifunza, na kufikiria kushiriki nukuu toka kwa Mzee D. Todd Christofferson au mojawapo ya video zipatikanazo katika “Nyenzo za Ziada.” Je, ni baraka gani tumezishuhudia pale tuliposhiriki katika kuleta wokovu kwa mababu zetu waliofariki?
Kupitia nguvu ya Yesu Kristo, tunaweza kukuza asili yetu ya kiungu.
-
Ili kuwahimiza wale unaowafundisha katika jitihada zao za kuwa zaidi kama Yesu Kristo, ungeweza kuwaalika kuzitambua sifa kama za Kristo zilizoelezewa katika 2 Petro 1:1–11. Fikiria kuandika sifa hizi kwenye ubao na kuwaomba washiriki wa darasa kuzielezea. Kisha washiriki wa darasa wangeweza kujadili jinsi gani kukuza sifa moja hutupeleka katika kukuza sifa zingine. Toa muda kwao kutafakari sifa gani wangependa kuikuza zaidi (ona pia Hubiri Injili Yangu, 126).
Himiza Kujifunza Nyumbani
Ungeweza kuelezea kwamba washiriki wa darasa watasoma waraka wa Yohana katika wiki ijayo. Nyaraka hizi husaidia kusahihisha mafundisho ya uongo kuhusu Yesu Kristo na zinaweza kuimarisha shuhuda za uhalisia wa Mwokozi aliye hai.
Nyenzo za Ziada
Kazi ya kuwakomboa wafu hushuhudia kuhusu misheni ya Mwokozi.
Mzee D . Todd Christofferson alifundisha:
Wanatheolojia wa kikiristo kwa muda mrefu wamekuwa wakisumbuka na swali, je, ni nini hatima ya mabilioni yasiyohesabika ya walioishi na kufa bila uelewa juu ya Yesu? Kwa Urejesho wa injili ya Yesu Kristo umekuja uelewa wa jinsi gani waliokufa bila kubatizwa wanaokolewa na jinsi gani Mungu anaweza kuwa Mungu ‘mkamilifu, Mungu mwenye haki, na Mungu mwenye rehema pia’ [Alma 42:15].
“Akiwa bado yu hai, Yesu alitoa unabii kwamba Yeye angewahubiria wafu pia [ona Yohana 5:25] Petro anatuambia kwamba hii ilitokea katika kipindi kati ya kusulubiwa kwa Mwokozi na Ufufuko [ona 1 etro 3:18–19]. Rais Joseph F. Smith alishuhudia katika ono kwamba Mwokozi alikwenda kwenye ulimwengu wa roho [ona Mafundisho na Maagano 138:30, 33]. …
Shauku yetu ya kukomboa wafu, na muda na rasilimali tunazoweka nyuma ya ahadi hii, ni, na zaidi ya yote, ni onyesho la ushahidi wetu kuhusu Yesu Kristo. Inatengeneza kauli yenye nguvu ambayo tunaweza kuitengeneza kuhusu sifa Yake ya kiungu na misheni Yake takatifu. Hushuhudia, kwanza, kuhusu Ufufuko wa Kristo; pili, juu ya ufikiaji wake usio na mwisho wa Upatanisho Wake; tatu, kwamba yeye ni chanzo pekee cha wokovu; nne, kwamba Yeye ameweka masharti ya ukombozi; na, tano, kwamba Yeye atakuja tena” (“Kuwakomboa Wafu na Ushuhuda wa Yesu,” Ensign au Liahona, Nov. 2000, 9–10).
Maandishi ya wahubiri wa Kikristo (karne ya kwanza hadi ya tatu) kuhusu kuhubiriwa kwa wafu.
Origen: “Wakati [Kristo] alipokuwa [roho], bila kufunikwa mwili, Aliishi miongoni mwa hizo roho ambazo hazikuwa zimefunikwa na mwili, akiwaongoa wale ambao walikuwa tayari Kwake” (katika The Ante-Nicene Fathers, ed. Alexander Roberts na James Donaldson [1907], 4:448).
Hermas: “Mitume na walimu ambao walihubiria jina la Mwana wa Mungu, baada ya kuwa wamekufa katika nguvu na imani ya Mwana wa Mungu, waliwahubiria na wale waliolala kabla yao” (katika The Apostolic Fathers, trans. J. B. Lightfoot [1898], 472).
Video kuhusu historia ya familia (ona LDS.org).
-
“Mioyo yao imeunganishwa kwenu”
-
“Familia Zote Duniani”
-
“Je, Nitafanya Sehemu Yangu?”