Njoo, Unifuate
Desemba 9–15. Ufunuo wa Yohana 1–11: ‘Utukufu, na Ukuu, Una … Mwana Kondoo Milele’


Desemba 9–15. Ufunuo wa Yohana 1–11: ‘Utukufu, na Ukuu, Una … Mwana Kondoo Milele’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

Desemba 9–15. Ufunuo wa Yohana 1–11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Kristo akichunga kundi la kondoo

Mchungaji Mwema, na Del Parson

Desemba 9–15

Ufunuo wa Yohana 1–11

“Utukufu, na Ukuu, Una … Mwana Kondoo Milele’”

Kupokea misukumo ya kiroho hukuwezesha kutambua kwamba Roho Mtakatifu anataka kukufundisha. Kuandika na kufuata misukumo hiyo kunaonyesha kwamba wewe unathamini na unatamani kupokea zaidi.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Unapoanza mjadala kuhusu Ufunuo wa Yohana, inaweza kusaidia kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki taarifa yoyote ya kihistoria waliyojifunza kuhusu kitabu cha Ufunuo wa Yohana katika kujifunza kwao binafsi au kifamilia. Mngeweza kurejea kwa pamoja baadhi ya taarifa zilizotolewa kwenye Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia au kusoma kwa pamoja “Yohana” na “Ufunuo wa Yohana.”

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Ufunuo wa Yohana 1

Yesu Kristo ni Mwana aliye Hai wa Mungu aliye Hai.

  • Kwa kuwa Yohana alitumia lugha ya taswira na alama katika Ufunuo wa Yohana 1 ili kumwelezea Mwokozi mfufuka na matendo Yake, kujifunza sura hii ni njia kuu ya kujenga imani kwamba yu hai na Anaongoza Kanisa Lake. Labda washiriki wa darasa wangeandika kwenye ubao virai kadhaa kutoka Ufunuo wa Yohana 1 ambavyo vinajumuisha taswira au alama na kushiriki kile ambacho kila moja kinawafundisha wao kuhusu Yesu Kristo. Kwa mfano, tunajifunza nini kutokana na alama hizi kuhusu namna ambavyo Kristo analiongoza Kanisa Lake leo? Ni kwa namna gani maelezo ya Yohana kuhusu Mwokozi yanalingana na yale katika Mafundisho na Maagano 110:1–4?

Ufunuo wa Yohana 2–3; 7:13–17

Tunaweza kuzishinda changamoto kupitia Yesu Kristo.

  • Sisi ni kama Watakatifu ambao Yohana aliwaandikia katika angalau njia moja: ambayo sisi tunakabiliana na dhiki. Waalike washiriki wa darasa kutafuta kutoka Ufunuo wa Yohana 2–3 na kubainisha majaribu ambayo Watakatifu wa wakati wa Yohana walikuwa wakikabiliana nayo, na wasaidie kuelewa kwamba Yesu Kristo alijua kila majaribu ya kila tawi na uwezo wake. Labda wangeweza kuelezea matukio ambayo walihisi kwamba Mwokozi alikuwa akijua hali zao za kipekee. Je, ni ushauri gani Mwokozi aliutoa kwa Watakatifu hao ambao unaweza pia kutusaidia kushinda changamoto zetu?

  • Katika sura hizi Bwana alitoa ahadi zenye mwongozo wa kiungu kwa wale wanaoshinda. Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kufanya kazi kwa jozi kutafuta kutoka Ufunuo wa Yohana 2–3; 7:13–17 ili kupata ahadi za Bwana. Labda pia wangechora picha ubaoni kuonyesha baadhi ya kanuni hizi, kisha walielezee darasa kile walichopata. Je, ni kwa namna gani ahadi hizi zinawatia hamasa kuendelea kujitahidi kushinda majaribu na udhaifu wao wenyewe?

Ufunuo wa Yohana 5

Yesu Kristo alikuwa ndiye pekee ambaye angeweza kuufanya mpango wa Baba wa Mbinguni uwezekane.

  • Je, somo la vyombo lingeweza kulisaidia darasa lako kuelewa lugha ya alama katika Ufunuo wa Yohana 5 kuhusu Mwokozi kufungua kitabu kilichofungwa? Unaweza kuleta zawadi ikiwa imefungiwa katika chombo kwa ajili ya kushiriki na darasa. Kabla ya darasa, kwa siri mpe mtu mmoja ufunguo wa kufuli. Elezea darasa ni kitu gani kilichomo ndani ya chombo, na waruhusu baadhi ya washiriki wa darasa wajaribu kukifungua chombo kabla ya mtu mwenye funguo hajakifungua. Kisha washiriki wa darasa wangeweza kulinganisha hili somo la vyombo na Ufunuo wa Yohana 5. Maswali kama haya yangeweza kusaidia: Ni kwa namna gani ukombozi wa watoto wa Baba wa Mbinguni ni kama chombo kilichofungwa au kitabu kilichofungwa? Kwa nini Yesu Kristo alikuwa ndiye pekee ambaye angeweza kufungua mihuri hiyo? (ona nukuu kwenye “Nyenzo za Ziada.”) Ni baraka zipi zilikuwa za kutegemewa kwa ustahiki wa Mwokozi ili kufungua hiyo mihuri? (ona Ufunuo wa Yohana 7:14–17).

  • Kama watu wenye shangwe waliosemwa katika Ufunuo wa Yohana 5, leo pia tunaweza kupaza sauti zetu kumsifu Mwokozi kama Mmoja ambaye anastahiki kutupatia wokovu. Labda washiriki wa darasa wangeweza kuimba kwa pamoja baadhi ya nyimbo pendwa za kusifu kuhusu Mwokozi. Kwa mfano, mngeweza kuimba “Glory to God on High” (Wimbo, namba. 67; au ona video “Worthy Is the Lamb” kwenye LDS.org) na kuainisha ukweli wimbo huu unafundisha kuhusu Yesu Kristo. Je, ni mambo gani yameweza kutusaidia sisi kupata shuhuda juu ya ukweli huu? Je, ni mifanano gani tunayoiona kati ya ujumbe wa nyimbo zetu za kusifu na tamko katika Ufunuo wa Yohana 5:9–14? Ni kwa namna gani tunaweza kutumia vizuri zaidi nyimbo nyumbani na kanisani ili kumwabudu na kumsifu Bwana?

Ufunuo wa Yohana 7

Kabla ya Ujio wa Pili, Bwana atawakusanya wenye haki na kuwandaa kukaa pamoja Naye.

  • Ufunuo wa Yohana 7 inaelezea matukio ya “muhuri wa sita,” baadhi yakiwakilisha siku yetu. Pia inajibu swali katika mwisho wa sura ya 6: “Siku iliyo kuu, ya ghadhabu yake, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?” (mstari wa 17). Labda washiriki wa darasa wangeweza kutafuta majibu kwa swali hili katika sura ya 7. Hapa kuna baadhi ya maswali mengine ambayo wanaweza kujadili: Kwa nini Bwana alichelea kuiharibu dunia kwa muda? Ni kwa namna gani ibada na maagano “hutuunganisha [sisi] hadi siku ambayo ghadhabu ya Mungu itamwagwa”? (Mafundisho na Maagano 1:9). Je, kazi yetu ni ipi katika kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya Ujio wa Pili? Mafundisho na Maagano 1:4–23; 77:8–11 ingeweza kutoa umaizi wa ziada.

Ufunuo wa Yohana 1–11

Ono la Yohana linatufundisha namna ambavyo Baba wa Mbinguni huwaokoa watoto Wake.

  • Baadhi ya washiriki wa darasa wanaweza kuona kwamba kitabu cha Ufunuo wa Yohana ni kigumu kueleweka. Inaweza kusaidia kama watafikiria maandiko ya Yohana katika muktadha wa mpango wa Baba wa Mbinguni wa kuwainua watoto wake. Wakati washiriki wa darasa wakisoma Ufunuo wa Yohana 1–11 nyumbani wanaweza kupata ukweli ambao uliwasaidia wao kuelewa Mpango wa Baba wa Mbinguni kwa watoto Wake (ona muhtasari wa wiki h katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waalike wanafunzi waelezee kile walichokiona. Wanaweza pia kugundua kwamba inasaidia kufanya marejeo katika sehemu ya “Nyenzo za Ziada” yenye kichwa cha habari “Maandiko kuhusu Mpango wa Wokovu.” Wahimize washiriki wa darasa kuendelea kutafuta maandiko ambayo yanafundisha ukweli kuhusu mpango wa wokovu wanaposoma sehemu iliyobaki ya Ufunuo wa Yohana, na wape fursa katika masomo yajayo kuelezea wanachopata.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waombe washiriki wa darasa kufikiria kuhusu desturi yao waipendayo ya Krismasi. Waalike kurejea muhtasari wa wiki ijayo kwa mawazo ya jinsi gani wanaweza kumweka Yesu Kristo kuwa kitovu cha sherehe yao

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Ufunuo wa Yohana 1–11

Maandiko kuhusu mpango wa wokovu.

Upatanisho wa Yesu Kristo.

Maisha kabla ya Maisha ya duniani

Maisha ya Duniani

Maisha baada ya maisha ya duniani

Ni Yesu pekee angeweza kulipia dhambi zetu.

Akizungumzia matukio kabla ya maisha ya duniani, Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

“Kristo alijitolea kuheshimu maadili ya haki ya kujiamulia ya wanadamu wote hata wakati Yeye akilipia dhambi zao. Katika mchakato huo, Yeye angerudisha utukufu wote kwa Baba kwa upendo huo wenye kukomboa.

“Upatanisho huu usio na mwisho wa Kristo uliwezekana kwa sababu (1) Yeye alikuwa ni mtu pekee asiye na dhambi aliyewahi kuishi katika dunia hii na hivyo hakuwa chini ya kifo cha kiroho kitokanacho na dhambi, (2) Yeye alikuwa ni Mwana Pekee wa Baba na hivyo kumiliki sifa za kiungu ambazo zilimpa Yeye nguvu juu ya kifo cha kimwili, na (3) Yeye ni wazi alikuwa mtu mnyenyekevu vya kutosha na aliye kuwa tayari katika baraza la kule mbinguni kutawazwa kwenye huduma hiyo ” (“Upatanisho wa Yesu Kristo,” Ensign au Liahona, Machi. 2008, 35).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia Maandiko na Maneno ya Manabii wa Siku za Mwisho. Bwana ametuamuru “kufundishana mafundisho ya ufalme” (Mafundisho na Maagano 88:77) na kutumia maandiko “kufundisha kanuni za injili [Yake] (Mafundisho na Maagano 42:12). Maandiko na maneno ya manabii na mitume wa siku za mwisho ni chanzo cha ukweli tunaofundisha” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 21).