Njoo, Unifuate
Desemba 9–15. Ufunuo 1–11: ‘Utukufu, na Ukuu, Una … Mwana Kondoo Milele’


“Desemba 9–15. Ufunuo 1–11: ‘Utukufu, na Ukuu, Una … Mwana Kondoo Milele’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)

“Desemba 9–15. Ufunuo 1–11,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Kristo akichunga kundi la kondoo

Mchungaji Mwema, na Del Parson

Desemba 9–15

Ufunuo 1–11

“Utukufu, na Ukuu, Una … Mwana Kondoo Milele”

Fikiria kuandika maswali uliyonayo kuhusu kile unachosoma katika Ufunuo. Kisha unaweza kutafuta majibu ya maswali yako au kuyajadili na mwana familia au katika madarasa ya kanisani.

Andika Misukumo Yako

Je, umewahi kupata taabu kuwaelezea wengine kile ulichojisikia wakati wa tukio lenye nguvu za kiroho? Kila siku lugha inaweza kuonekana isiyotosheleza kuelezea hisia na misukumo ya kiroho. Pengine hii ndiyo sababu Yohana alitumia ishara nyingi kama hizo na tamathali za semi kuelezea ufunuo wake mtukufu. Angeweza kiurahisi kuelezea kwamba alimuona Yesu Kristo, lakini kutusaidia kuelewa tukio lake hili, alimuelezea Mwokozi kwa kutumia maneno kama haya: “macho yake yalikuwa kama mwali wa moto,” “kwenye kinywa chake kulitoka upanga mkali wenye makali kuwili,” na “uso wake kama jua liking’aa kwa nguvu zake” (Ufunuo 1:14–16). Unaposoma kitabu cha Ufunuo, jaribu kugundua ujumbe Yohana alitaka ujifunze na uhisi, hata kama huelewi maana iliyoko ndani ya kila ishara. Kwa nini aliweza kufananisha mikutano ya Kanisa na vinara vya mshumaa, Shetani na mnyama, na Yesu Kristo na mwana kondoo? Hatimaye, siyo lazima kuelewa kila ishara katika Ufunuo ili kuelewa dhamira yake muhimu, ikijumuisha dhamira yake kuu kuliko zote: Yesu Kristo na wafuasi Wake watashinda falme za watu na Shetani.

ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Ufunuo

Ninawezaje kukielewa kitabu cha Ufunuo?

Kitabu cha Ufunuo kinaweza kuwa kigumu kukielewa, lakini usikate tamaa. Ahadi ya Yohana inaweza kukushawishi kuendelea kujaribu: “Heri wasomao, na wao wayasikiao na kuelewa maneno ya unabii huu, na kuyashika yale mambo yaliyoandikwa humo, kwa maana wakati wa kurudi kwa Bwana u karibu” (Tafsiri ya Joseph Smith, Ufunuo 1:3 [katika kielezo cha Biblia], msisitizo umeongezwa).

Maswali na nyenzo zifuatazo zinaweza kutoa utambuzi unapojifunza Ufunuo.

Inaweza pia kusaidia kutafuta utambuzi katika Tafsiri ya Joseph Smith ya vifungu mbalimbali vya Ufunuo. (Ona tanbihi na kiambatisho cha Biblia.)

Ufunuo

Ono la Yohana hufundisha jinsi Baba wa Mbinguni anavyowaokoa watoto Wake.

Unapoanza kujifunza kitabu cha Ufunuo, fikiria kuhusu jinsi mambo unayosoma yanavyohusiana na kile unachojua kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni kwa ukombozi na kuinuliwa kwa watoto Wake. Unaweza kuanza kwa kupitia upya mwanzo hadi mwisho mpango wa wokovu katika Hubiri Injili Yangu (kurasa 47–59). Kisha, unaposoma maelezo ya Yohana juu ya ono lake, jiulize maswali kama haya: Ni kweli zipi ninazojifunza kutoka katika Ufunuo kuhusu kile Baba wa Mbinguni amekifanya ili kunisaidia kurudi Kwake? Ni kwa jinsi gani hii hunisaidia mimi kuelewa mpango wa Mungu kwa ajili yangu?

Inaweza kukusaidia kujua kwamba kwa ujumla:

  • Mengi kwenye sura ya 12 yanahusika na matukio ya maisha kabla ya kuja duniani (ona pia “Maisha kabla ya kuja duniani,” Mada za Injili, topics.lds.org).

  • Sura 6–11, 13–14, 16–19 zinaelezea maisha ya duniani na matukio katika historia ya dunia (ona pia “Maisha katika mwili wenye kufa,” Mada za Injili, topics.lds.org).

  • Sura 2–3, 15, 20–22 huelezea Hukumu ya Mwisho na utukufu ambao huwasubiri waaminifu katika falme za milele (ona pia “Maisha baada ya kifo,” Mada za Injili, topics.lds.org).

Ufunuo 2–3

Yesu Kristo ananijua mimi binafsi na atanisaidia kushinda changamoto zangu.

Maneno ya Mwokozi katika Ufunuo 2–3 hufunua kwamba Yesu alielewa mafanikio na masumbuko ya kipekee kwa kila tawi la Kanisa katika siku ya Yohana. Aliwahakikishia Watakatifu katika mikusanyiko kadhaa kwamba alifahamu, miongoni mwa mambo mengine, “kazi” zao, “mateso,” yao “umasikini” wao na “hisani” yao (Ufunuo 2:2, 9, 19)—sambamba na baadhi ya njia ambazo wangeweza kufanya vizuri zaidi.

Sura hizi zinaweza kukumbusha kwamba Mwokozi anaelewa nguvu zako na udhaifu wako na anataka kukusaidia kushinda changamoto zako za duniani. Ni nini Yesu Kristo huahidi kwa wale wanaoshinda? Ni mabadiliko gani unahisi kuvuviwa kufanya ili kushinda changamoto zako?

Ufunuo 5

Ni Yesu Kristo pekee ambaye angeweza kufanya mpango wa Baba wa Mbinguni kuwezekana.

Japokuwa wewe hukumbuki, huenda ulikuwepo kwenye matukio Yohana aliyoelezea katika Ufunuo 5. Unaposoma kuhusu matukio haya, fikiria jinsi ambavyo ilikuwa wakati wote tulipotambua kwamba Yesu Kristo (“Mwana Kondoo”) angefanya mpango wa Baba wa Mbinguni kuwezekana (kufungua kitabu na kuvunja mihuri saba). Kwa nini Yesu Kristo pekee ndiye angeweza kufanya hili? Ni kwa jinsi gani unaweza kuonyesha imani yako Kwake kama Mwokozi wako?

Ona pia Ayubu 38:4–7; “Upatanisho wa Yesu Kristo.,” Mada za Injili, topics.lds.org

Ufunuo 6–11

Urejesho ulitangulia maangamizo ambayo yatatokea kabla ya Ujio Wa Pili wa Yesu Kristo.

Ufunuo 6–11 huelezea matukio yatakayotokea wakati wa uwepo wa maisha ya dunia (ona M&M 77:6), ikijumuisha Urejesho wa injili katika siku za mwisho (ona Ufunuo 7). Unaposoma kuhusu matukio Yohana aliyotolea unabii na kutazama baadhi yake yakitukia, nini unashawishika kufanya ili kujiandaa vizuri zaidi na familia yako kwa ajili ya Ujio wa Pili?

ikoni ya kujifunza Kifamilia.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:

Ufunuo 2–3

Jifanye Yohana aliombwa kutoa ujumbe kwa familia yako kama ule aliotoa kwa makanisa wakati wa kipindi chake. Je, nini ambacho angesema kinakwenda vizuri? Je, ni kwa namna gani mngeweza kufanya vizuri zaidi?

Ufunuo 3:20

Onyesha picha ya Mwokozi akibisha mlangoni (ona picha inayoambatana na muhtasari huu). Waalike familia yako kusoma Ufunuo 3:20 na kujadili maswali kama yafuatayo: kwa nini Yesu anabisha badala ya kuingia tu ndani? Ni kwa jinsi gani tunaweza kuialika nguvu Yake katika nyumba zetu?

Ufunuo 7:9, 13–14

Je, mistari hii inaweza kutufundisha nini kuhusu kwa nini tunavaa mavazi meupe kwa ajili ya ibada za hekaluni?

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza maswali. Maswali ni kiashirio kwamba wanafamilia wako tayari kujifunza na kutoa utambuzi wa jinsi wanavyoitikia katika kile wanachofundishwa. Wafundishe familia yako jinsi ya kutafuta Majibu Katika Maandiko. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25–26.

Kristo akibisha mlangoni

Mkaribishe ndani, na Greg K. Olsen