“Desemba 16–22. Krismasi: ‘Habari njema ya Furaha Kuu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya 2019 (2019)
“Desemba 16–22. Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019
Desemba 16–22.
Krismasi
“Habari Njema ya Furaha Kuu”
Kwa wengine, Krismasi yaweza kuwa wakati wa shughuli nyingi. Fikiria jinsi gani kujifunza kwako Agano Jipya kunaweza kuleta roho ya amani na utakatifu katika maisha yako. Tafakari ushawishi wa kuzaliwa kwa Mwokozi na huduma yake katika maisha yako, na andika misukumo yo yote ya kiroho inayokujia.
Andika Misukumo Yako
Kwa nini kuzaliwa kwa mtoto kunaleta furaha kuu kama hiyo? Labda kwa sababu mtoto mpya anaweza kuwa ishara ya tumaini. Kuna kitu kuhusu maisha mapya kabisa yaliyojaa uwezekano ambayo hutualika kutafakari nini maisha yanaweza kubeba kwa yule mtoto na mambo gani mazuri atakayofanikisha. Kamwe hili halijawahi kuwa kweli kuliko wakati wa kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu, Yesu Kristo. Kamwe hakujawahi kuwa na tumaini la juu kabisa kuwekwa kwa mtoto, na kamwe hakujawahi kuwa na yeyote aliyezaliwa na ahadi nyingi.
Wakati malaika alipowaalika wachungaji kumtafuta mtoto aliyezaliwa ndani ya hori, aliwapa pia ujumbe kuhusu mtoto yule. Ulikuwa ni ujumbe wa tumaini—kwamba mtoto huyu alikuja duniani kutimiza wito mtakatifu. Wachungaji walifanya ujumbe wao “kujulikana kila mahali … na wote waliousikia walistaajabu juu ya mambo hayo ambayo yalisemwa kwao na wachungaji. Lakini Mariamu aliyatunza mambo haya yote, na kuyatafakari moyoni mwake” (Luka 2:17–19). Pengine ingekuwa vizuri kufuata mfano wa Mariamu Krismasi hii: kutafakari moyoni mwako mambo uliyojifunza kuhusu Mwokozi mwaka huu. Ni kwa jinsi gani alitimiza wito Wake wa ukombozi katika maelezo uliyosoma? Na muhimu zaidi, ni kwa jinsi gani wito Wake umebadilisha maisha yako?
Mawazo ya Kujifunza Maandiko Binafsi
Mathayo 1:18–25; 2:1–12; Luka 1:26–38; 2:1–20
Yesu Kristo alijishusha hadhi kwa kuzaliwa miongoni mwetu duniani.
Hata kama umesoma au kusikia hadithi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo mara nyingi kabla, jifunze wakati huu ukiwa na wazo hili akilini: Krismasi siyo tu sherehe ya jinsi gani Yesu alikuja ulimwenguni bali pia ya kujua Yeye ni nani—Bwana wetu na Mwokozi, Yesu Kristo—na kwa nini alikuja” (Craig C. Christensen, “Utimilifu wa Hadithi ya Krismasi” [ibada ndogo ya Krismasi ya Urais wa Kwanza, Des. 4, 2016], broadcasts.lds.org).
Je, unafahamu Yesu Kristo alikuwa nani kabla hajazaliwa? (ona, kwa mfano, Yohana 17:5; Mosia 3:5; M&M 76:13–14, 20–24; Musa 4:2). Ni kwa jinsi gani uelewa huu huathiri jinsi unavyojisikia unaposoma kuhusu kuzaliwa Kwake?
Unafahamu nini kuhusu kwa nini Yesu Kristo alikuja duniani? (ona, kwa mfano, Luka 4:16–21; Yohana 3:16–17; 3 Nefi 27:13–16; M&M 20:20–28). Ni kwa jinsi gani ufahamu huu huathiri jinsi unavyojisikia kuhusu Mwokozi? Ni kwa jinsi gani huathiri jinsi unavyoishi?
Ona pia 2 Wakorintho 8:9; Waebrania 2:7–18; 1 Nefi 11:13–33; Alma 7:10–13; “Kuzaliwa kwa Yesu Kristo” (filamu, LDS.org).
1 Wakorintho 15:21–26; Wakolosai 1:12–22; 1 Petro 2:21–25
Yesu Kristo alitimiza misheni Yake na kufanya iwezekane kwangu kurithi uzima wa milele.
Japokuwa hadithi ya kuzaliwa kwa Kristo ilizungukwa na matukio ya kimiujiza, kuzaliwa Kwake kungekuwa tu kama kuzaliwa kwingine isingekuwa kwa kazi kuu ambayo aliikamilisha baadaye katika maisha Yake. Kama Rais Gordon B. Hinckley alivyosema, “Mtoto Yesu wa Bethlehemu angekuwa tu kama mtoto mwingine bila Kristo mkombozi wa Gethsemane na Kalvari, na kweli ya shangwe ya ushindi wa ule Ufufuko”“Maajabu na Hadithi ya Kweli ya Krismasi,” Ensign, Des. 2000, 5).
Ushahidi wa misheni takatifu ya Mwokozi na upendo Wake wenye nguvu kwa wengine unapatikana kote kwenye Agano Jipya. Je, ni vifungu vipi au hadithi gani hukujia akilini? Unaweza kuangalia nyuma kupitia nyenzo hii au shajara yako ya kujifunza na kurudia baadhi ya misukumo uliyoandika. Unaweza pia kusoma 1 Wakorintho 15:21–26; Wakolosai 1:12–22; 1 Petro 2:21–25 na kutafakari ni jinsi gani Mwokozi na kazi Yake vimebariki maisha yako. Je, unahisi kushawishika kubadili nini katika maisha yako? Je, ni kwa jinsi gani utaivuta nguvu ya Mwokozi?
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.
Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:
Ni kwa jinsi gani unaweza kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo na familia yako? Hapa kuna baadhi ya mawazo, au unaweza kuja na ya kwako:
-
Someni na igizeni pamoja vipengele vya hadithi ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
-
Ona pia filamu “Kuzaliwa kwa Yesu Kristo” (LDS.org).
-
Tafuta baadhi ya nyenzo kwenye christmas.mormon.org; jesuschrist.lds.org; au “Krismasi,” Mada za Injili, topics.lds.org.
-
Tazama ibada ya Krismasi ya Urais wa Kwanza(broadcasts.lds.org;).
-
Imbeni pamoja nyimbo za kanisa za Krismasi, au chagueni majirani au marafiki wa kuwatembelea na kuwaimbia (see Nyimbo za kanisa, nos. 201–14).
-
Fanya tendo la huduma.
-
Waambie wanafamilia kutafuta maelezo katika hadithi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambayo yanawapa mawazo kwa ajili ya madoido au mapambo wanayoweza kutengeneza ili kuwakumbusha juu ya Yesu Kristo.
Kwa nini tunashukuru kwamba Yesu Kristo alizaliwa? Ni zawadi gani Yeye ametupatia sisi? Tunawezaje kumwonyesha shukrani zetu ?
“Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume”
Ukitaka kuisaidia familia yako kuzingatia kwa Mwokozi wakati wa Krismasi, pengine unaweza kutumia muda kusoma na kujifunza pamoja “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume” (Ensign au Liahona, Mei 2017, ndani ya jalada la mbele). Labda mnaweza kukariri vifungu kutoka “Kristo Aliye Hai” au kutafuta maelezo ya maisha ya Mwokozi ndani ya Agano Jipya ambayo huunga mkono kauli zilizomo. Unaweza pia kumualika kila mwanafamilia kuandika ushuhuda wake wa Yesu Kristo na, kama atavuviwa hivyo, ausome kwa familia.
Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.