Njoo, Unifuate
Desemba 23–29. Ufunuo 12–22: ‘Yeye Ashindaye Atayarithi Haya’


“Desemba 23–29. Ufunuo 12–22: ‘Yeye Ashindaye Atayarithi Haya’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano Jipya (2019)

“Desemba 23–29. Ufunuo 12–22,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2019

Picha
Yesu Kristo akiwasalimu watu katika Ujio Wake wa Pili

Jiji la Milele, na Keith Larson

Desemba 23–29

Ufunuo 12–22

“Yeye Ashindaye Atayarithi Haya”

Unaposoma Ufunuo 12–22, tafuta kufananisha kati ya kile Yohana alichokiona na kile wewe unachokiona katika ulimwengu wa leo. Tafuta mwongozo wa kiroho ili ukusaidie kupata masomo binafsi unapojizamisha katika lugha ya Yohana ya kiishara.

Andika Misukumo Yako

Fikiria mwanamke “hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.” Sasa fikiria “joka kubwa jekundu, likiwa na vichwa saba na pembe kumi” likimzunguka mwanamke, likisimama “ili azaapo amle mtoto wake ” (Ufunuo 12:2–4). Ili kuelewa mistari hii ya ufunuo wa Yohana, kumbuka kwamba taswira hizi huwakilisha Kanisa na ufalme wa Mungu na hatari ambazo ingekabiliana nazo. Kwa Watakatifu ambao walipitia matukio ya mateso makali katika siku za Yohana, ushindi dhidi ya uovu yaweza kuwa haikuonekana kuwezekana. Ushindi huu pia unaweza kuwa mgumu kutazamia katika siku kama yetu, pale adui anapokuwa “vitani na watakatifu” na ana “nguvu … juu ya jamaa zote, na ndimi, na mataifa” (Ufunuo 13:7). Lakini mwisho wa ufunuo wa Yohana kwa utukufu unaonyesha kwamba wema utashinda dhidi ya uovu. Babeli itaanguka. Yesu Kristo atatawala kama Mfalme wa Wafalme. “Mungu atafuta machozi yote,” na waaminifu watatawala pamoja Naye na “kurithi vitu vyote” (Ufunuo 21:4, 7).

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Binafsi

Ufunuo 12:7–17

Vile Vita vya Mbinguni vinaendelea duniani.

Hatujui mengi kuhusu Vita vya Mbinguni, lakini kuna maelezo yake ya wazi ingawa mafupi katika Ufunuo 12:7–11. Unaposoma mistari hii, jitazame wewe mwenyewe kama sehemu ya mapigano yale ya kabla ya kuja duniani. Je, mistari hii inafundisha nini kuhusu jinsi wewe na watoto wengine waaminifu wa Mungu mlivyomshinda Shetani? Hii inadokeza nini kuhusu jinsi unavyoweza kumshinda katika siku yetu anapoendelea “kufanya vita na [wale ambao] wana ushuhuda juu ya Yesu Kristo”? (mstari 17).

Ona pia 1 Nefi 14:12–14; “Vita Mbinguni,” Mada za Injili, topics.lds.org; Kamusi ya Biblia, “Mikaeli,” “Vita Mbinguni.”

Ufunuo 14:6–7

Ni nani malaika ambaye Yohana alimuona akihubiri injili?

Utimizwaji mmoja wa unabii katika mistari hii ulitokea wakati Moroni alipomtokea Joseph Smith na kumuongoza kwenye kumbukumbu ambazo alitafsiri na kuchapisha kama Kitabu cha Mormoni. Kitabu hiki kina “injili ya milele” ambayo sisi tumepewa jukumu la kuihubiri kwa “kila taifa, na kabila, na lugha, na jamaa” (Ufunuo 14:6).

Ufunuo 17–18

Mwokozi hunialika kuikimbia Babeli na dhambi zake.

Ufunuo 17–18 una taswira za kufadhaisha zinazoelezea dhambi, tamaa ya anasa za dunia, na tamaa za Babeli—ishara ya tamaa za dunia na uovu. Fikiria juu ya mifano ya hali za Kibabeli zilizopo leo ulimwenguni, na tafakari nini unachoweza kufanya ili kufuata ushauri wa “kutoka nje ya Babeli na kutoshiriki dhambi zake” (Ufunuo 18)

Ufunuo 20:12–15

Watoto wote wa Mungu watahukumiwa kutoka katika kitabu cha uzima.

Chukulia kwamba mwandishi amejitolea kuandika kitabu kuhusu maisha yako. Ni maelezo gani au matukio gani ungependa yajumuishwe? Kama ungejua kwamba matendo yako ya baadaye yangeandikwa pia, jinsi gani ungeyakabili maisha yako kwa namna tofauti? Fikiria kuhusu hili unaposoma kuhusu Siku ya Hukumu katika Ufunuo 20:12–15. Nini unatumaini kitaandikwa kuhusu wewe katika kitabu cha uzima?

Ona pia Kamusi ya Biblia, “Kitabu cha uzima.”

Ufunuo 21; 22:1–5

Kama mimi ni mwaminifu, nitapokea utukufu wa selestia.

Kinyume cha maelezo ya Babeli, Ufunuo 21–22 huelezea utukufu wa selestia ambao huwasubiri wafuasi waaminifu wa Kristo. Ni taswira gani, virai au ahadi katika sura hizi hukupa mwongozo wa kiungu wa kubaki mwaminifu hata wakati inapokuwa vigumu”

Ufunuo 22:18–19

Je, mistari hii humaanisha kwamba hakuwezi kuwepo maandiko yoyote ya ziada tofauti na Biblia?

Baadhi ya watu wamedondoa Ufunuo 22:18–19 kama sababu ya kukataa Kitabu cha Mormoni na maandiko mengine ya siku za mwisho. Hata hivyo, Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

“Sasa kuna muafaka wa kushinda kabisa ulio wa kweli miongoni mwa wasomi wa kibiblia kwamba mstari huu ni kwa kitabu cha Ufunuo huu tu, siyo Biblia yote. Wasomii hawa wa siku yetu wanatambua idadi kadhaa ya ‘vitabu’ vya Agano Jipya ambavyo kwa hakika viliandikwa baada ya ufunuo wa Yohana katika kisiwa cha Patmo kupokelewa. …

Lakini kuna jibu rahisi zaidi. … Biblia yote kama tunavyoijua—mkusanyiko mmoja wa maandishi yaliyo unganishwa katika juzuu moja—ambayo haikuwepo wakati mstari huo ulipoandikwa” (“Maneno yangu … Hayakomi kamwe,” Ensign au Liahona, Mei 2008, 91).

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia.

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani.

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Hapa kuna baadhi ya mapendekezo:

Ufunuo 12; 19; 21

Baadhi ya wana familia wanaweza kufurahia na kunufaika kutokana na kuchora picha za maono yaliyoelezewa katika Ufunuo. Kwa mfano, kuchora picha kutokana na Ufunuo 12 kunaweza kuwapeleka kwenye mjadala kuhusu Vita Mbinguni (ona mistari 7–11). Picha kutokana na Ufunuo 21 zinaweza kuchochea mazungumzo kuhusu ufalme wa selestia. Unaweza pia kuonyesha picha ambazo zinaambatana na muhtasari huu na kuwataka wanafamilia kutafuta mistari katika Ufunuo 19 ambayo picha inaelezea.

Ufunuo 12:11

Kirai “neno la ushuhuda wao” kinaweza kumaanisha nini? Je, ni kwa jinsi gani shuhuda zetu juu ya Yesu Kristo hutusaidia sisi na wengine kumshinda Shetani?

Ufunuo 13:11–14

Je, ni mawazo gani wanafamilia wako wanayo kuhusu mnyama mdanganyifu? Je, ni kwa jnsi gani tunagundua na kuepukana na uongo tunaouona ulimwenguni leo?

Ufunuo 20:2–3

Je, ni kwa jinsi gani 1 Nefi 22:26; Mafundisho na Maagano 43:30–31 hutusaidia kuelewa kile kinachoweza kumaanisha kwa Shetani “kufungwa”?

Ufunuo 22:1–4

Je, nini yaweza kuwa maana ya kiishara ya kuwa na jina la Kristo katika “paji za nyuso [zetu]”? (Ufunuo 22:4; ona pia Ufunuo 13:16–17).

Kwa mawazo zaidi juu ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii ndani ya Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fuatilia Mialiko ya Kutenda. Wakati unapofuatilia mualiko wa kutenda, wewe unawaonyesha [wanafamilia wako] kwamba unawajali na jinsi gani injili inabariki maisha yao. Pia unawapa wao nafasi ya kuelezea uzoefu wao, ambao huimarisha kujitolea kwao na huwapa fursa ya kusaidiana katika kuishi injili” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 35).

Picha
Yesu Kristo akishuka na farasi kutoka mbinguni katika Ujio Wake wa Pili

Kristo katika vazi jekundu ameketi juu ya farasi mweupe

Chapisha