Njoo, Unifuate
Desemba 23–29. Ufunuo 12–22: ‘Yeye Ashindaye Atayarithi Haya’


“Desemba 23–29. Ufunuo 12–22: ‘Yeye Ashindaye Atayarithi Haya’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Desemba 23–29. Ufunuo 12–22.“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Yesu Kristo akiwasalimu watu wakati wa Ujio Wake wa Pili

Jiji la Milele, na Keith Larson

Desemba 23–29

Ufunuo 12–22

“Yeye Ashindaye Atayarithi Haya”

Unapojitayarisha kufundisha, fikiria juu ya uzoefu wako mwenyewe wa kujifunza Ufunuo 12–22 binafsi au pamoja na familia yako. Je, ni kitu gani kilichokuwa cha kipekee kwako? Je, ni mawazo gani ulipokea? Kumbuka kwamba shughuli zilizopendekezwa hapa zinaweza kutoholewa kwa ajili ya watoto wa umri wo wote.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waombe watoto waelezee kwa nini wanataka kuishi na Baba wa Mbinguni tena. Katika somo zima, wasaidie kutafuta vitu wanavyoweza kufanya ili kujitayarisha kurudi Kwake.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Ufunuo 12:7–11

Nilionyesha imani katika Yesu Kristo katika maisha kabla ya kuja duniani.

Katika Vita huko Mbinguni, watoto waaminifu wa Mungu walimshinda Shetani kwa “neno la ushuhuda wao” na kwa kuonyesha imani katika Yesu Kristo (Ufunuo 12:11).

Shughuli Yamkini

  • Ili kuwasaidia watoto kuelewa ina maana gani kufuata mfano wa mtu fulani, mchague mtoto mmoja kuwa “kiongozi” na waombe wengine kumfuata kwa kufanya chochote kile anachokifanya yeye. Kisha waache watoto wengine kuwa kiongozi. Wasomee watoto Ufunuo 12:7–11 na uelezee kwamba kabla hatujazaliwa, sisi tulichagua kumfuata Yesu na sio Shetani.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu maisha kabla ya kuja duniani, kama vile “I Lived in Heaven” au “I Will Follow God’s Plan” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 4 164-65). Uliza maswali kama, Ni nini kilitokea Mbinguni kabla hatujazaliwa? Je, sisi tulichagua kufanya nini? (Ona pia “Utangulizi: Mpango wa Baba Yetu wa Mbinguni,” Hadithi za Agano Jipya, 1-5, au video zinazoambatana katika LDS.org.)

Ufunuo 19:7

Ninaweza kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo kwa kuchagua yaliyo mema.

Je, unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa kwamba Ujio wa Pili utakuwa wa matukio ya furaha kwetu sisi kama tutafuata amri za Yesu?

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia, na soma Ufunuo 19:7. Eleza kwamba “ndoa ya mwana kondoo” inawakilisha Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Je, ni kwa nini watu walikuwa na “shangwe”? Waulize watoto kama wamewahi wakati wowote kuhudhuria sherehe za harusi. Je, ilikuwaje? Je, ni kwa nini watu walikuwa na furaha?

  • Shiriki pamoja na watoto kwa nini wewe unatazamia Ujio wa Pili wa Yesu. Mnaweza pia kuimba pamoja wimbo kuhusu Ujio wa Pili, kama vile “When He Comes Again” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82-83).

  • Waalike watoto kuelezea kile wanachokifanya ili kuwa tayari kwa ajili ya Kanisani siku ya Jumapili. Je, ni kwa nini tunafanya vitu hivi kabla hatujaja Kanisani? Je, ni kwa nini tujitayarishe kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Kristo? Kwenye ukurasa wa shughuli za wiki hii, waache watoto wachore kile wanachoweza kufanya ili kujitayarisha kwa ajili ya Ujio wa Pili.

Ufunuo 21:1, 3–4,22–27; 22:1–2

Ninaweza kuishi katika ufalme wa selestia pamoja na Baba wa Mbinguni na watu ninaowapenda.

Katika mwisho wa sura mbili za Ufunuo, Paulo alitumia lugha nzuri kuelezea utukufu wa selestia ambao wenye imani watafurahia.

Shughuli Yamkini

  • Waache watoto wachore mti uliosimuliwa katika Ufunuo 22:2 ubaoni. Eleza kwamba mti huu, ni mti wa uzima, na matunda yake yanawakilisha upendo wa Mungu (ona 1 Nefi 11:21–22). Wape watoto vipande vya karatasi vilivyoumbwa kama tunda, na waombe wachore kwenye karatasi kitu fulani ambacho kinawasaidia kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni. Eleza kwamba wale ambao ni wenye imani wataishi pamoja na Baba wa Mbinguni katika ufalme wa selestia.

  • Shiriki pamoja na watoto baadhi ya taswira au kila kitu Yohana alichotumia ili kuelezea utukufu wa selestia (ona Ufunuo 21:1, 3–4, 22–27; 22:1–2), na waombe watoto wachore picha za vitu hivi.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu mpango wa Mungu, kama vile “I will Follow God’s Plan” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto 164-65). Waalike watoto kutambua kile wanachoweza kufanya ili kuishi na Baba wa Mbinguni tena.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Ufunuo 12:7–11

Nilionyesha imani katika Yesu Kristo katika maisha kabla ya kuja duniani.

Watoto unaowafundisha wapo duniani kwa sababu walikuwa na imani katika Yesu Kristo katika maisha kabla ya kuja duniani na walichagua kumfuata Yeye.

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Ufunuo 12:7–11, na andika ubaoni maneno joka, Vita huko Mbinguni, tupwa nje, ushuhuda, na Mwana kondoo. Waalike watoto kufanya muhtasari wa aya hizi wakitumia maneno yaliyopo ubaoni. Je, tunajifunza nini kuhusu Yesu Kristo (mwana kondoo) kutoka mistari hii? Je, tunajifunza nini kuhusu chaguzi tulizofanya katika maisha kabla ya kuja duniani?

  • Kwenye ubao, umba safu tatu na zitambulishe kama Kabla ya maisha haya, Wakati wa maisha haya, na Vyote. Tayarisha vipande vya karatasi ambavyo vinaeleza ukweli kuhusu maisha kabla ya kuja duniani na kuhusu maisha hapa duniani, kama vile Tunayo miili, Hatuna miili, tunaishi katika uwepo wa Mungu, Tupo vitani dhidi ya Shetani, Tunaonyesha imani katika Yesu Kristo, na Tunafuata mpango wa Mungu. Waache watoto wachukue zamu kuchagua kipande cha karatasi na kuamua ni safu gani kinastahili kuwemo. Elezea mategemeo yako ili watoto waweze kuendelea kuonyesha imani katika Kristo.

Ufunuo 19:7–8

Ninaweza kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Yesu Kristo kwa kuchagua yaliyo mema.

Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kwamba Ujio wa Pili wa Yesu Kristo utakuwa tukio la furaha kwa wenye haki?

Shughuli Yamkini

  • Someni pamoja Ufunuo 19:7–8, na wasaidie watoto kuelewa uashiriaji uliotumika katika mistari hii—harusi ni Ujio wa Pili wa Mwokozi, Mwana Kondoo ni Mwokozi, na mke Wake ni Kanisa (au sisi wote). Je, ni kwa jinsi gani watu wanajitayarisha kwa ajili ya harusi? Je, ni mambo gani tunatakiwa kufanya ili kujitayarisha kwa ajili ya Mwokozi kuja tena?

  • Rejea na ukariri Makala ya Imani 1:10 pamoja na watoto. Eleza kwamba makala hii ya imani inaelezea matukio ya kusisimua, na kufurahisha sana ambayo yatatokea wakati Yesu anapokuja tena. Onyesha picha ya Ujio wa Pili wa Yesu katika Njoo,unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia na waalike watoto kuchora jinsi wanavyofikiri Ujio wa Pili wa Yesu utakavyo kuwa.

Ufunuo 21:1, 3–4,22–27; 22:1–2 17

Ninaweza kuishi katika ufalme wa selestia pamoja na Baba wa Mbinguni na watu ninaowapenda.

Unapojitayarisha kufundisha kuhusu ufalme wa selestia, tafakari juu ya kile ufalme wa selestia unamaanisha kwako wewe. Je, unawezaje kutoa ushuhuda wako kwa watoto unaowafundisha?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kutafuta mistari ifuatayo kwa ajili ya picha au kila kitu ambacho Yohana alitumia kuelezea kuhusu utukufu wa selestia: Ufunuo 21:1, 3–4, 22–27; 22:1–2. Waache wachague picha au maelezo ambayo watapenda kuchora. Kisha wanaweza kuzungumza kuhusu michoro yao na darasa. Watie moyo kuonyesha michoro yao kwa familia zao nyumbani.

  • Someni pamoja Ufunuo 22:17, na uelezee kwamba bibi harusi anayesema “Njoo” ni Kanisa. Je, tunataka kuwaalika wengine “kuja” kwa nani? Je, baadhi ya njia nzuri za kuwaalika watu “kuja” ni zipi?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wasaidie watoto kujitayarisha kusoma Kitabu cha Mormoni mwaka ujao kwa kuwataka wamuulize mwana familia au rafiki kuwaelezea mstari au hadithi aipendayo kutoka katika Kitabu cha Mormoni.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wafundishe watoto kuandika misukumo wanayopata. Kama watoto watajifunza tabia ya kuandika misukumo yao, itawasaidia kugundua na kumfuata Roho Mtakatifu. Watoto wanaweza kuandika misukumo yao kwa kuwekea alama maandiko, kuchora picha, au kuweka kumbukumbu rahisi katika shajara zao. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 30.)

Chapisha