Njoo, Unifuate
Desemba 9–15. Ufunuo 1–11: ‘Utukufu, na Ukuu, Una … Mwana kondoo Milele’


“Desemba 9–15. Ufunuo 1–11: ‘Utukufu, na Ukuu Una … Mwana kondoo Milele’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Desemba 9–15. Ufunuo 1–11.“ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

Picha
Kristo akichunga kundi la kondoo

Mchungaji Mwema, na Del Parson

Desemba 9–15

Ufunuo 1–11

“Utukufu, na Ukuu Una … Mwana kondoo Milele”

Uashiriaji katika Ufunuo unaweza kuwa mgumu kwa watoto kuuelewa, lakini Ufunuo pia una mafundisho muhimu ambayo ni mazuri na ya kawaida.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto kuelezea jinsi wanavyoweza kujisikia kama wangemwona Yesu Kristo katika ono. Eleza kwamba katika kitabu cha ufunuo, Yohana alielezea ono ambamo alimwona Yesu na vitu vingi muhimu kuhusu yaliyopita na yajayo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Ufunuo 3:20

Ninaweza kumwalika Yesu Kristo katika maisha yangu.

Sitiari ya Yesu akisimama mlangoni na akigonga inaweza kuwasaidia watoto kuelewa kwamba anataka kuwa karibu nao.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia na soma Ufunuo 3:20. Waalike watoto wawaze kwamba Yesu alikuwa anagonga mlangoni kwenye nyumba yao. Je, watamfungulia aingie ndani? Je, wanafikiri atasema au kufanya nini?

  • Waalike watoto wakuelezee kuhusu nyakati walipomsubiri mtu fulani kutembelea nyumbani kwao mtu ambaye walisisimka kumwona. Je, ilikuwaje kumsubiri mtu yule kugonga mlango? Je, ingekuwaje kama wasingemruhusu aingie ndani? Soma Ufunuo 3:20, na waache watoto wachukue zamu kushika picha ya Yesu na kujifanya kuwa anagonga mlango. Washiriki wengine wa darasa wajifanye wanafungua mlango. Je, tunaweza kufanya nini ili kumwacha Yesu awe karibu nasi, hata kama hatuwezi kumwona? Fikiria kumpa kila mtoto picha ya Yesu aende nayo nyumbani.

Ufunuo 5:1–10

Yesu Kristo ni mtu pekee anayestahili kuwa Mwokozi wangu.

Yohana alijifunza kutokana na ono hili kwamba Yesu Kristo ni mtu pekee (aliewakilishwa na mwana kondoo) ambaye angeweza kuwa Mwokozi wetu na kutimiza mpango wa Baba (uliowakilishwa na kitabu kilichotiwa muhuri).

Shughuli Yamkini

  • Kabla ya darasa, tafuta picha ambazo zinawakilisha baraka zinazopatikana kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo (kama vile hekalu, ubatizo, na familia), ziweke ndani ya kitabu na funga kitabu kwa karatasi au kamba. Ukitumia virai vichache muhimu kutoka Ufunuo 5:1–10, elezea ono Yohana aliloona. Waoneshe watoto kitabu hicho, na waambie kwamba njia pekee ya kufungua kitabu ni kutafuta picha ya Yesu ambayo umeificha ndani ya chumba. Watakapoipata picha, fungua kitabu na shiriki pamoja na watoto picha zilizoko ndani ya kitabu. Shuhudia kwamba Mwokozi alikuwa ni mtu pekee ambaye angeweza kufanya vitu hivyo viwezekane.

  • Fanya muhtasari wa ono lililoelezwa katika Ufunuo 5:1–10, na waalike watoto waigize jinsi Yohana na wengine walivyojisikia wakati wa sehemu tofauti za ono. Kwa mfano, wanaweza kujifanya wanalia wakati hakuna yoyote anayeweza kufungua kitabu, au wanaweza kushangilia wakati Mwokozi alipokifungua.

Ufunuo 7:9,13–14

Yesu Kristo ananisaidia niwe msafi kutokana na dhambi.

Yohana aliwaona watu wengi waliovishwa majoho “yaliyotengenzwa … meupe katika damu ya Mwanakondoo” (aya 14). Fikiria jinsi ono hili linavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa umuhimu wa kufanywa wasafi kutokana na dhambi zetu kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Shughuli Yamkini

  • Waonyeshe watoto baadhi ya mavazi ya ubatizo au nguo nyingine nyeupe na picha ya Yesu. Wasomee watoto Ufunuo 7:9, 13–14, na waombe kuonesha picha na nguo kila wakati wanaposikia neno nyeupe. Eleza kwamba nguo nyeupe inawakilisha usafi na kutukumbusha kwamba Yesu Kristo anaweza kutufanya kuwa wasafi kutokana na makosa yetu.

  • Waonyeshe watoto kipande cha nguo nyeupe, na waache waichafue kwa kuiweka alama na kalamu au kuweka uchafu juu yake. Eleza kwamba dhambi inafanya roho zetu ziwe chafu. Onyesha picha ya Yesu katika Gethsemane (kama vile Kitabu cha Sanaa za Injili, nam 56), weka nguo chafu kando, na waoneshe nguo safi nyeupe. Shuhudia kwamba kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, tunaweza kuwa safi.

  • Imbeni wimbo kuhusu ubatizo, kama vile “When I Am Baptized” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto 103), na mjadiliane jinsi Yesu anavyotusaidia kuwa wasafi wakati tunapobatizwa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Ufunuo 3:20

Ninaweza kuchagua kumruhusu Yesu Kristo kuwa sehemu ya maisha yangu.

Je, unawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha kufungua mioyo yao na maisha kwa uwezo na ushawishi wa Yesu Kristo?

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kutazama picha kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia unaposoma Ufunuo 3:20. Ili kuwasaidia kupata maana kutoka kwenye picha, waalike kufanya kazi katika majozi ili kujibu maswali kama haya: Je, kwa nini unafikiri Yesu anagonga mlangoni? Je, kwa nini hakuna kitasa chenye mkono nje ya mlango? Je, inamaanisha nini kumruhusu Yesu ndani ya maisha yetu?

  • Waombe watoto kuandika ubaoni njia tofauti za “kufungua mlango” kwa ajili ya Yesu. Baadhi ya mifano inaweza kujumuisha kuwahudumia wengine, kusoma maandiko na kupokea sakramenti.

Ufunuo 5:1–10

Yesu Kristo ni mtu pekee anayestahili kuwa Mwokozi wangu.

Ono lililoelezwa katika Ufunuo 5 lilifundisha kwamba Yesu Kristo pekee ndio alistahili na kuweza kutekeleza Upatanisho na kutuokoa kutokana na dhambi.

Shughuli Yamkini

  • Waalike watoto kueleza juu ya wakati ambapo walipomhitaji mtu fulani kufanya kitu fulani wasichoweza kujifanyia wao wenyewe. Waombe kusoma Ufunuo 5:1–10 na kutafuta kile kilichotakiwa kufanywa ambacho mtu mmoja pekee ndiye angeweza kufanya (eleza kwamba mwana kondoo ni Yesu Kristo na kitabu kinawakilisha mpango wa Mungu). Je, Yesu alifanya nini kwa ajili yetu ambacho hakuna mtu mwingine ye yote angeweza kufanya?

  • Waombe watoto kutafuta wimbo au wimbo wa watoto ambao unamshuhudia Yesu Kristo (kama vile “Beautiful Savior” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 62–63). Maneno ya wimbo yanafundisha nini kuhusu Yesu Kristo? Je, ni kwa namna gani wimbo huu unaweza kuwa kama wimbo wa kusifu kuhusu Yesu Kristo katika Ufunuo 5:9–10?

Ufunuo 9:1–2

Injili inaweza kunisaidia kushinda majaribu.

Moshi ambao ulitia giza hewa katika Ufunuo 9:2 unaweza kufananishwa na majaribu (ona 1 Nefi 12:17).

Shughuli Yamkini

  • Chora picha za jua na wingu zito, na uikate. Waalike watoto kusoma Ufunuo 9:2 na 1 Nefi 12:17 na andika juu ya hilo wingu zito kile ambacho moshi au ukungu katika aya hizi unawakilisha. Weka wingu zito juu ya ubao, na waombe watoto kutengeneza orodha ya majaribu watoto wa umri wao wanayakabili. Kisha weka jua juu ya ubao na waombe kutengeneza orodha ya zana Baba wa Mbinguni ametupa ili kushinda giza katika ulimwengu.

  • Je, ni kwa jinsi gani watoto wanaweza kuwasaidia wengine ambao wako gizani kiroho? Kuwasaidia kufikiria kuhusu swali hili, onyesha video “Choose the Light” (LDS.org), na waalike kuzungumzia kuhusu mwendesha pikipiki.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki na familia zao njia wanazoweza kukaribisha ushawishi wa Mwokozi ndani ya nyumba zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza staha. Kipengele muhimu cha staha ni kufikiria juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Unaweza kuwakumbusha watoto kuwa wenye staha kwa kuimba kimya kimya au wimbo wa mvumo au kuonyesha picha ya Yesu.

Chapisha