“Desemba 2–8, 1–3, Yohana; Yuda: ‘Mungu ni Upendo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)
“Desemba 2–8, 1–3, Yohana; Yuda.” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019
Desemba 2–8
1–3 Yohana; Yuda
“Mungu ni Upendo”
Nyaraka za Yohana na Yuda zinafundisha kuhusu upendo na nuru ya Baba wa Mbinguni. Unapojifunza wiki hii, tafakari kwa nini watoto unaowafundisha wanahitaji nuru na upendo Wake katika maisha yao. Kumbuka kufikiria shughuli zote katika muhtasari huu, sio tu hizo zilizoorodheshwa chini ya rika unalofundisha.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Waalike watoto kuelezea jinsi walivyouhisi upendo wa Baba wa Mbinguni au kwa nini wanafikiri Baba wa Mbinguni ni kama nuru.
Fundisha Mafundisho
Watoto Wadogo
Kumfuata Yesu kunaleta nuru kwenye maisha yangu.
NI kwa jinsi gani kufananisha nuru halisi na giza kuna kusaidia kufundisha watoto kuhusu nuru ambayo Baba wa Mbinguni anaileta katika maisha yao?
Shughuli Yamkini
-
Waombe watoto wataje vitu vinavyotoa nuru. Wasaidie kuelewa faida za nuru, kama kusaidia mimea kukua, kutuwezesha kuona, na kutoa joto. Waalike watoto kuchukua zamu kupiga tochi picha ya Yesu wanaposema, “Mungu ni nuru” (1 Yohana 1:5). Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaweza kuleta nuru katika maisha yetu tunapotii amri.
-
Tia giza chumba, na waalike watoto kupendekeza njia ambazo nuru inaweza kuletwa ndani ya chumba. Wasaidie wafikirie njia tunazoweza kuleta nuru ya Yesu Kristo ndani ya maisha yetu. Wanapotoa majibu yao, washa tochi au fungua dirisha pole pole kuongeza nuru kwenye chumba.
Ninaonyesha upendo wangu kwa Mungu ninapoonyesha upendo kwa wengine.
Wasaidie watoto kuona uhusiano kati ya upendo wanaouhisi kwa Baba wa Mbinguni na upendo wanaoonyesha kwa watoto Wake.
Shughuli Yamkini
-
Wasomee watoto 1 Yohana 4:11, na uimbe wimbo kuhusu upendo wa Mungu, kama vile “My Heavenly Father Loves Me” (Kitabu cha nyimbo za Watoto, 228). Waombe watoto wachache kuelezea jinsi wanavyojua kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda, Baada ya kila jibu, waalike watoto kukumbatiana na kusema, “Mungu ni upendo, na Mungu ananipenda.”
-
Wasomee watoto 1 Yohana 4:21. Waalike kuelezea au kuigiza njia mbalimbali wanazoweza kuonyesha upendo kwa rafiki, kama vile kumkumbatia au kumtengenezea kadi. Je, vitu hivi vinamfanya rafiki yetu ajisikieje? Baba wa Mbinguni anahisi tunapofanya mambo ya huruma kwa wengine?
Ninaonyesha upendo wangu kwa Mungu ninaposhika amri Zake.
Watoto wanaweza kujifunza katika umri mdogo kwamba “amri za Mungu hazihuzunishi” na kwamba kuzifuata ni njia ya kuonyesha upendo Kwake.
Shughuli Yamkini
-
Soma 1 Yohana 5:3, na waombe watoto wasikilize ni nini aya hii inasema kuhusu jinsi tunavyoweza kuonyesha kwamba tunampenda Mungu. Waalike watoto kutaja amri nyingi kadiri wanavyoweza. Baba wa Mbinguni huhisi vipi tunapotii amri zake?
-
Waalike watoto kuchora picha inayoonesha mojawapo ya njia wanayoweza kuonyesha upendo wao kwa Baba wa Mbinguni. Kwa mfano, wanaweza kuchora picha yao wenyewe wakishika moja ya amri hizo. Imbeni pamoja wimbo kuhusu utii, kama vile “Choose the Right Way” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 160). Tunajisikiaje tunapotii ?
Fundisha Mafundisho
Watoto Wakubwa
Ninaonyesha upendo wangu kwa Mungu ninapoonyesha upendo kwa wengine.
Unawezaje kuwasaidia watoto kujua kwamba kumpenda Mungu kunahusisha kuwapenda wale wanaotuzunguka—hata watu wanaoweza kuwa tofauti nasi au vigumu kuwapenda?
Shughuli Yamkini
-
Waombe watoto wawaze kwamba mtu mpya ameanza kuhudhuria shule yao au kata na hamjui mtu yo yote pale. Mtu huyu anaweza kuwa anajisikiaje? Mwalike mtoto asome 1 Yohana 4:7–8. Aya hii inapendekeza nini kuhusu jinsi tunavyotakiwa kumtendea mtu huyu? Elezea matukio yanayofanana, au waombe watoto kufikiria hali ambazo wao wanaweza kuwa na nafasi kuonyesha upendo.
-
Waombe watoto wasome 1 Yohana 4:7–8, 20–21, na waalike kila mmoja kuandika sentensi moja ili kufanya muhtasari wa kile wanachofikiri ni somo muhimu sana katika mistari hii. Baada ya kuelezea sentensi zao, unaweza kuwasimulia hadithi ya Chy Johnson kutoka hotuba ya Kaka David L. Beck ”Jukumu Lako Takatifu la Kuhudumu” (Ensign au Liahona Mei 2013 55). Je, ni kwa jinsi gani watoto wataweza kufuata mifano ya wavulana katika hadithi hii ambao walionesha upendo kwa Chy? Waalike watoto kuelezea njia zingine wanazoweza kuonyesha upendo kwa wale wanaowazunguka.
1 Yohana 2:3–6; 4:17–18; 5:2–5
Ninaonyesha upendo wangu kwa Mungu ninaposhika amri Zake.
Kushika amri kunaweza kuwa rahisi mno wakati tunapoelewa kweli zinazofundishwa katika 1 Yohana 5:3. Je, unawezaje kuwasaidia watoto kuziona amri sio kama mizigo bali kama nafasi ya kuonyesha upendo wao kwa Mungu?
Shughuli Yamkini
-
Waalike watoto kuorodhesha ubaoni njia wanazoweza kumwonesha Mungu kwamba wanampenda. Kisha someni pamoja 1 Yohana 2:5–6; 5:2–5 kwa mawazo ya ziada. Je, ni kwa jinsi gani kushika amri kunaonyesha kwamba tunampenda Baba wa Mbinguni?
-
Soma 1 Yohana 4:17, na uwaelezee watoto kwamba “kuwa na ujasiri katika siku ya hukumu” maana yake ni kuwa na matumaini na amani watakaposimama mbele ya Mungu kuhukumiwa. Je, mstari huu unafundisha nini ambacho tunahitaji kufanya ili kuwa na matumaini haya? Je, ni vitu gani vingine tunavyoweza kufanya sasa ili tujiamini mbele ya Mungu?
Naweza kuwa mwaminifu hata wakati wengine wanaponifanyia mzaha.
Watoto wanaweza kudhihakiwa kwa ajili ya imani zao au kwa njia wanavyoishi kama wafuasi wa Yesu Kristo. Mistari hii ina ushauri wa Yuda juu ya jinsi ya kubaki waaminifu katika hali kama hizo.
Shughuli Yamkini
-
Waombe watoto kusimulia nyakati walipofanyiwa mzaha kwa kufanya kile kilicho sahihi. Waalike watoto wasome Yuda 1:18–22 na kutafuta jinsi tunavyoweza kubaki waaminifu tunapofanyiwa mzaha au tunapokejeliwa. Andika ubaoni kile wanachokipata, na jadili njia wanazoweza kufuata ushauri huu.
-
Fanya muhtasari wa ndoto ya Lehi (ona 1 Nefi 8:1–35), waombe watoto wachache wasome mistari kutoka 1 Nefi 8:26–28 33. Jadili jinsi watu katika jumba kubwa na pana walivyokuwa kama wafanya mzaha ambao Yuda aliowazungumzia. Je, tufanye nini ili tusishawishiwe na hao wanaotufanyia mzaha au wasiokubaliani na kile tunachoamini? (Ona 1 Nefi 8:30 33).
Himiza Kujifunza Nyumbani
Wahimize watoto kutengeneza mpango wa kufanya kitu fulani ili kushiriki nuru yao pamoja na familia zao.