Njoo, Unifuate
Desemba 16–22. Krismasi: ‘Habari Njema ya Furaha Kuu’


“Desemba 16–22. Krismasi ‘Habari Njema ya Furaha Kuu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 (2019)

“Desemba 16–22. Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2019

mtoto Yesu horini

Salama Zizini, na Dan Burr

Desemba 16–22

Krismasi

“Habari Njema ya Furaha Kuu”

Somo hili ni nafasi ya kuwasaidia watoto unaowafundisha kusherehekea kuzaliwa, maisha, na misheni ya Mwokozi wakati wa Krismasi. Weka wazo hili katika akili unapojitayarisha kufundisha.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia, na waalike watoto kuelezea kile wanachojua kuhusu kuzaliwa kwa Mwokozi.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wadogo

Mathayo 2:1–12; Luka 2:1–14

Yesu Kristo alikuja duniani kama mtoto.

Hadithi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo inawavutia watoto. Ni ukweli gani wa kimafundisho unaouna katika hadithi hii ambao unaona watoto wanapaswa kuuelewa?

Shughuli Yamkini

  • Wasomee watoto Luka 2:1–44, au uelezee matukio katika aya hizi kwa kurejea kwenye “Sura ya 5: Yesu Kristo Amezaliwa,” Hadithi za Agano Jipya, 13–15, au video zinazofanana nazo katika LDS.org. Waalike watoto kuchora picha za matukio haya na wao wenyewe wazitumie picha hizi kueleza hadithi hizo. Je, ni kwa nini wewe unafurahi kwamba Yesu alikuja duniani kama mtoto?

  • Waombe watoto kukueleza hadithi ya Mamajusi wakifuata nyota kumtafuta Yesu. Kama wanahitaji kukumbushwa juu ya hadithi, ona Mathayo 2:1–12 au ”Sura ya 7: Mamajusi,” Hadithi za Agano Jipya, 18 au video inayofanana katika LDS.org. Ficha picha ya Yesu chumbani. Chora au kata kutoka kwenye karatasi nyota na uishike hewani. Waalike watoto kujifanya kuwa mamajusi wakibeba zawadi, na waongoze kuzunguka chumba kumtafuta Yesu. Je, ni zawadi gani ambazo tunaweza kuzitoa kwa Yesu katika maisha yetu leo?

  • Imbeni nyimbo chache za Krismasi pamoja na watoto, kama vile “Furaha kwa Ulimwengu” na “ Usiku Kimya” (Nyimbo, Nam. 201, 204) au “ Stars Were Gleaming,” “ Awayin a Manger,” na “Oh, Hush Thee,My Baby” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 37, 42-43, 48).

Yohana 3:16

Yesu Kristo alifanya iwezekane kwangu mimi kuishi pamoja na Baba wa Mbinguni tena siku moja.

Je, watoto unaowafundisha wanaelewa kwa nini Yesu Kristo alikuja duniani? Chukua muda kutafakari kile Mwokozi amekifanya kwako wewe binafsi na jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa kile alichofanya kwa ajili yao.

Shughuli Yamkini

  • Leta zawadi iliyofungwa darasani na picha ya Yesu Kristo ikiwa ndani yake. Weka kibandiko kwenye zawadi na “Yohana 3:16” kimeandikwa juu yake, na waeleze watoto kwamba hii ni ishara kuhusu zawadi hiyo ni kitu gani. Soma Yohana 3:16 pamoja na watoto, na waalike kukisia zawadi hiyo ni kitu gani na ifungue. Je, ni kwa nini Mungu alimtuma Mwanaye kwetu?

  • Chagua picha kutoka kwenye Kitabu cha Sanaa za Injili (kama vile nam. 1, 30, 35–6684) ambazo zinaeleza kwa mifano baadhi ya njia ambazo kwazo Yesu aliwabariki watu wengine wakati alipoishi duniani. Waache watoto washikilie picha wakati unaposimulia hadithi hizo. Unaweza kuchagua picha ambazo zinaendana na maneno ya “Alimtuma Mwanaye” na “Niambie Hadithi za Yesu” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34-35, 57) na waache watoto wazishike picha wanapoimba nyimbo hizi.

  • Waalike watoto kusimulia hadithi wanazozipenda kuhusu Yesu. Baada ya kila hadithi kusimuliwa, wasaidie watoto kumalizia sentensi: “Yesu Kristo alikuja duniani ku .” Kisha onyesha picha zinazohusiana na dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi, kifo, na Ufufuko (ona Kitabu cha Sanaa za Injili, nam. 56, 57, 58, 59) na kwa kifupi simulia kuhusu matukio haya. Toa ushuhuda wako kwamba Yesu Kristo alikuja duniani ili kufa kwa ajili yetu na kufufuka ili tuweze kurudi kwa Baba wa Mbinguni.

    Yesu akipiga magoti katika Bustani ya Gethsemane

    Gethsemane, na J. Kirk Richards

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Watoto Wakubwa

Mathayo 1:18–25; 2:1–12; Luka 1:26–38; 2:1–20

Yesu Kristo alikuja duniani kama mtoto.

Utawezaje kuwasaidia watoto kuzingatia juu ya Yesu Kristo wakati wa Krismasi?

Shughuli Yamkini

  • Muombe mmoja wa watoto kusoma kuhusu matukio yanayohusisha kuzaliwa kwa Mwokozi katika Mathayo 1:18–25; 2:1–12; Luka 1:26–38; 2:1–20. Waombe watoto wengine kuchukua zamu kuchora picha ubaoni za kile maandiko yanaelezea. Je, hadithi hizi zinatufundisha nini kuhusu Yesu Kristo?

  • Onyesha video “Good Tidings of Great Joy: The Birth of Jesus Christ” (LDS.org). Waombe watoto waandike chochote wanachosikia ambacho kitawasaidia kuzingatia juu ya Yesu Kristo wakati wa Krismasi. Baada ya video, waalike kuelezea kile walichoandika.

  • Waalike watoto waandike kwenye vipande kadhaa vya karatasi vitu ambavyo wangeweza kufanya ili kuwasaidia kuzingatia kwa Mwokozi wakati wa msimu wa Krismasi. Weka karatasi zao katika mifuko au vyombo vingine kwa ajili ya watoto kwenda nazo nyumbani. Baadhi ya mawazo yanaweza kuwa ya kusoma maandiko, kuimba nyimbo za Krismasi, na kufanya matendo ya dhati ya upendo.

  • Kuimba nyimbo za Krismasi kuhusu Mwokozi (ona Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 36–54; Nyimbo nam. 201–214), na waalike watoto kushiriki na wengine msitari wanaoupenda au kirai kutoka kwenye nyimbo.

Yohana 3:16

Yesu Kristo alifanya iwezekane kwangu mimi kuishi pamoja na Baba wa Mbinguni tena siku moja.

Unawezaje kuwasaidia watoto kupitia upya kile walichojifunza mwaka huu na kuelewa kwa nini wanamhitaji Yesu Kristo katika maisha yao?

Shughuli Yamkini

  • Weka lebo kwenye vipande viwili vya karatasi Yesu Kisto ni nani? Na Kwa nini alikuja duniani? Na vibandike kwenye viambaza tofauti vya darasa. Mwalike kila mtoto kusoma mojawapo ya maandiko yafuatayo: Mathayo 16:15–16; Yohana 3:16; 1 Nefi 10:4; Mosia 3:8; Alma 7:10–13; 3 Nefi 27:14–15. Waambie watoto watafute majibu ya maswali mawili yaliyo ukutani katika maandiko wanayosoma. Waalike kuandika majibu yao kwenye vipande hivyo vya karatasi na wavibandike kwenye ukuta karibu na swali sahihi. Je, tunawezaje kuonyesha shukrani zetu kwa kile ambacho Yesu Kristo amefanya kwa ajili yetu?

  • Waalike watoto kuorodhesha ubaoni majina yote au vyeo vya Yesu ambavyo wanaweza kuvifikiria (ona Kamusi ya Biblia, Kristo, majina ya). Je, majina haya yanatufundisha nini kuhusu Yesu Kristo na misheni Yake? Kwa nini tunamhitaji Yesu Kristo katika maisha yetu? Kusaidia kujibu swali hili, onyesha video “Why We Need a Savior—A Christmas Message about Our Savior Jesus Christ” (LDS.org).

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Himiza watoto kutafuta angalau njia moja ya kumhudumia mtu fulani mwingine au kuja karibu zaidi kwa Kristo Krismasi hii.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto wanapenda kuelezea kile wanachojifunza. Hata watoto wadogo wanaweza kuwaimarisha wanafamilia wao. Wahimize watoto unaowafundisha kushiriki na familia zao kitu walichojifunza katika darasa la Msingi. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 30.