Njoo, Unifuate
Desemba 16–22. Krismasi: ‘Habari Njema ya Shangwe Kuu’


Disemba 16–22. Waefeso: ‘Habari Njema ya Shangwe Kuu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

Desemba 16–22. Krismasi,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Picha
Mtoto Yesu akiwa horini

Salama Zizini, na Dan Burr

Desemba 16–22

Krismasi

“Habari Njema ya Shangwe Kuu”

Majadiliano ya injili yanakuwa na nguvu za kiroho yanapokuwa na kiini katika Yesu Kristo. Unaposoma kuzaliwa na misheni ya Yesu Kristo wiki hii, tafuta mwongozo wa kiungu kutoka kwa Roho Mtakatifu ili kujua jinsi gani unaweza kuweka kiini cha mjadala wa darasa lako kuwa juu ya Mwokozi.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike washiriki wa darasa kuelezea kile wanafanya au wamefanya hapo mbeleni kibinafsi au kifamilia ili kusherehekea kuzaliwa kwa Mwokozi katika njia ambayo inawasogeza karibu Naye.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 1:18–25; Luka 1:26–38; 2:1–20

Yesu Kristo alijishusha ili kuzaliwa duniani.

  • Kujishusha humaanisha kwa hiari kujiweka chini kutoka hali au cheo au utukufu wa juu (ona 1 Nefi 11:14–26). Krismasi ni muda mzuri wa kutafakari na kusheherekea kujishusha kwa Kristo–utayari Wake kuacha “enzi ya Baba yake mbinguni, kuishi pamoja na binadamu, kufa kwa ajili ya binadamu” (“Again We Meet around the Board,” Wimbo, na. 186). Ili kuupa mwongozo wa kiungu mjadala juu ya mada hii, ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa walijifunza nini katika kujifunza kwao binafsi au kifamilia wiki hii kuhusu Yesu Kristo alikuwa nani kabla Yeye hajazaliwa (ona Yohana 17:5; Mosia 7:27; Mafundisho na Maagano 76:12–14, 20–24; Musa 4:2). Kisha ungeweza kuonyesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Nifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia wakati washiriki wa darasa wakisoma kuhusu kuzaliwa kwa Mwokozi (ona Mathayo 1:18–25; Luka 1:26–38; 2:1–20). Je, ni mawazo na hisia gani wanazo wanapolinganisha utukufu wa Mwokozi kabla ya maisha ya duniani na kuzaliwa Kwake kwa hali duni?

  • Swali moja kama Nefi aliloulizwa na malaika katika 1 Nefi 11:16 lingeweza kuwa njia nzuri ya kuanza mjadala, ingawa ungeweza kuliuliza kwa namna nyingine. Labda ungeweza kuandika kwenye ubao Ufadhili wa Mungu ni nini? Na waombe washiriki wa darasa kutafakari swali hili wakati wakisoma 1 Nefi 11:17–33. Waombe washiriki mawazo yoyote kuhusu Mwokozi ambayo yanaelezwa na mistari hii. Je, ni picha zipi ungeweza kuonyesha kwa darasa ambazo zinaelezea matukio kutoka kwenye maisha ya Mwokozi yaliyoelezwa na Nefi? Wangeweza pia kufikiria ufadhili wa Mwokozi wakati wakiangalia video kuhusu kuzaliwa Kwake kama “A Gift to the World,” “The Nativity,” “Infant Holy, Infant Lowly (Music Video)—Mormon Tabernacle Choir,” au “He Is the Gift” (zote hizi zinaweza kupatikana kwenye LDS.org).

  • Muziki ni njia nzuri ya kumwalika Roho katika darasa lako. Fikiria kucheza nyimbo za Krismasi zilizoimbwa na kwaya ya Tabernacle (ona mormontabernaclechoir.org), mwalike mtu fulani kuimba wimbo wa Krismasi, au kusoma au kuimba nyimbo chache kwa pamoja kama darasa (ona Nyimbo, na. 201–14). Washiriki wa darasa wangeweza kutafuta virai katika nyimbo na maandiko yaliyoorodheshwa na nyimbo ambayo yanaongeza shukrani zao kwa Mwokozi na utayari Wake wa kuja duniani.

Luka 4:16–21; Yohana 3:16

Yesu Kristo alitimiza kazi Yake, ambayo ilifanya kuwa ya kuwezekana kwetu kuurithi uzima wa milele.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujadili sababu za Kristo kuzaliwa, ungeweza kuwaalika kutafuta na kushiriki maandiko ambayo yanatoa muhtasari wa kazi Yake (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa msaada). Labda washiriki wa darasa wangeweza kutafuta na kusoma mistari katika jozi au vikundi vidogo. Wanajifunza nini kuhusu kazi ya Mwokozi kwenye mistari waliyoipata? Je, tunajifunza nini kuhusu kazi Yake kutokana na baadhi ya majina Aliyopewa katika maandiko? (Ona Kamusi ya Biblia, “Kristo, jina la”).

  • Washiriki wa darasa wangeweza kujifunza kuhusu kazi ya Mwokozi kwa kusoma “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume” (Ensign au Liahona Mei 2017, ndani ya jalada la mbele) na kushiriki kauli walizopata ambazo zinaelezea kwa nini Alikuja duniani. Au wangeweza kurejea ujumbe wa Rais Gordon B. Hinckley katika “Nyenzo za Ziada” na kujadili wanajifunza nini kuhusu Mwokozi. Je, ni kwa namna gani tunaweza kutenga muda msimu huu wa Krismasi kwa ajili ya “kufikiria na kutafakari kiundani” juu ya Mwokozi na misheni Yake?

  • Wape washiriki wa darasa muda wa kutafakari juu ya shuhuda zao juu ya Yesu Kristo na misheni Yake. Wangeweza kuelezea uzoefu binafsi au hadithi kutoka katika maisha ya Mwokozi ambazo zimeongeza imani yao Kwake au upendo wao Kwake. Je, ni kwa namna gani kujifunza Agano Jipya mwaka huu kumechangia kuufanya msimu huu wa Krismasi kuwa wa maana zaidi? Ili kurejea baadhi ya hadithi za Agano Jipya ambazo washiriki wa darasa wamejifunza mwaka huu, ungeweza kuonyesha video “For God So Loved the World” or “To This End Was I Born” (LDS.org).

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Pendekeza kwa washiriki wa darasa lako kwamba kujifunza Ufunuo wa Yohana 12–22 wiki hii kunaweza kuzidisha shukrani zao kwa nafasi ya Mwokozi katika mpango wa wokovu na kuongeza maana katika jinsi wanavyoichukulia Krismasi.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Krismasi

Kiini cha kweli cha Krismasi.

Rais Gordon B. Hinckley alifundisha:

“Wakati yote yamekwisha semwa na kufanyika, … hakuna kilicho kizuri zaidi, kitukufu, kilicho kikubwa kama kitendo hiki cha neema wakati Mwana wa Mwenyezi, … Yeye ambaye alijishusha kwa kuja duniani kama mtoto akizaliwa Bethlehemu, alitoa uhai Wake katika fedheha na maumivu ili kwamba wana wote na mabinti wa Mungu wa vizazi vyote, kila mtu ambaye lazima afe, aweze kutembea tena na kuishi milele. Alifanya kwa ajili yetu ambapo hakuna yeyote kati yetu angeweza kufanya kwa ajili yetu. …

“Hii ni hadithi ya kushangaza na ya kweli juu ya Krismasi. Kuzaliwa kwa Yesu katika Bethlehemu ya Uyahudi ni utangulizi. Miaka–mitatu ya huduma ya Bwana ni dibaji. Sehemu kuu ya hadithi ni dhabihu Yake, kitendo kamili kisicho na ubinafsi cha kufa katika maumivu kwenye msalaba wa Kalvari ili kulipia dhambi zetu wote.

Picha
Yesu akipiga magoti katika Bustani ya Gethsemane

Gethsemane, na J. Kirk Richards

“Hitimisho ni muujiza wa Ufufuko, ukileta uhakikisho kwamba ‘kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa’ (1 Wakorintho 15:22).

“Hapangekuwepo na Krismasi kama isingekuwepo Pasaka. Mtoto Yesu wa Bethlehemu angekuwa kama mtoto mwingine tu bila Kristo wa kukomboa wa Gethsemane na wa Kalvari, na ushindi wa kweli wa Ufufuko.

“Ninaamini katika Bwana Yesu Kristo, Mwana wa milele, wa Mungu Aliye hai. Hakuna aliye mkuu zaidi aliyewahi kutembea duniani. Hakuna yeyote aliyetoa dhabihu kama yake au kutoa baraka kama zake. Yeye ni Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu. Ninaamini katika Yeye. Ninatoa tamko la uungu Wake bila kuficha au kusita. Ninampenda. Ninalitaja jina Lake kwa heshima na kustaajabu. …

Na kwa kila mmoja wenu na hii iwe heri ya Krismasi. Lakini muhimu zaidi, ninakutakieni kila mmoja wenu muda, labda saa moja, kuwa kwenye kufikiria na kutafakari kwa kina juu ya maajabu na utukufu wa huyu, Mwana wa Mungu. Shangwe yetu katika msimu huu ni kwa sababu Yeye alikuja ulimwenguni. Amani ambayo hutoka Kwake, upendo Wake usio na kikomo ambao kila mmoja wetu anaweza kuhisi, na shangwe isiyo kifani kwa kile ambacho Alikitoa bure kwetu Akilipia gharama Yeye Mwenyewe—hiki ni kiini cha kweli cha Krismasi,”(“Maajabu na Hadithi ya Kweli ya Krismasi,” Ensign, Desemba. 2000, 4–5).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tenga muda kwa wanaojifunza ili kushiriki. “Wakati wanafunzi wanaposhiriki kile wanachojifunza, hawahisi tu Roho na kuimarisha shuhuda zao pekee, bali pia wanawahimiza washiriki wengine wa darasa kugundua ukweli wao wenyewe. … Tenga muda kwa ajili ya wanafunzi kushiriki katika kila somo—katika hali fulani, unaweza kugundua kwamba mazungumzo haya ndiyo somo” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 30).

Chapisha