”Wewe ni Mwalimu katika Kanisa la Yesu Kristo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019.)
“Wewe ni Mwalimu katika Kanisa la Yesu Kristo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019
Wewe ni Mwalimu katika Kanisa la Yesu Kristo.
Umeitwa kutoka kwa Mungu kufundisha watoto Wake katika njia ya Mwokozi. Ulisimikwa kwenye wito huu na mamlaka ya ukuhani Wake mtakatifu. Hata kama wewe sio mwalimu mwenye uzoefu, unapoishi kwa kustahili, kusali kila siku, na kujifunza maandiko, Baba wa Mbinguni atakurithia uzoefu na uwezo wa Roho Mtakatifu (ona 2 Nefi 33:1).
Wale uliokabithiwa kuwatunza ni watoto wa Mungu, na anajua nini wanahitaji na njia bora ya kuwafikia. Kupitia kwa Roho Mtakatifu, utaongozwa unapojitayarisha na unapofundisha. Atakufunulia kile unatakiwa kusema na kile unachopaswa kufanya.
Azma muhimu ya kujifunza injili ni kubadili maisha. Lengo lako kama mwalimu ni kuwasaidia wale unaowafundisha kufanya kila wawezacho kuwa waongofu katika injili ya Yesu Kristo—lengo ambalo linaendelea kupita muda wa darasa. Waalike wale unaowafundisha kushiriki hai katika kujifunza kwao wenyewe kanuni na mafundisho ya Yesu Kristo na kutenda yale wanayojifunza. Wahimize kufanya kujifunza kwao binafsi na familia nje ya darasa kuwa lengo la msingi la kujifunza injili kwao. Wanapotenda kwa imani kwa kujifunza kama watu binafsi na familia, watamwalika Roho katika maisha yao na kubarikiwa kwa undani zaidi kuliko kitu chochote mwalimu anaweza kufanya.
Fundisha tu mafundisho ya injili ya urejesho ya Yesu Kristo kama yanavyopatikana katika maandiko na maneno ya manabii wa siku za mwisho. Mafundisho safi—ya milele, ukweli usiobadilika iliofundishwa na Mungu na watumishi Wake—unamwalika Roho na una uwezo wa kubadili maisha.
Mwito wa kufundisha ni wajibu mtakatifu, na ni kawaida kuhisi kuzidiwa wakati mwingine. Lakini kumbuka kwamba Mungu alikuita, na kamwe hatakuacha. Hii ni kazi ya Bwana na unapohudumu “kwa moyo wako wote, uwezo, akili na nguvu” (M&M 4:2), Ataongeza uweza wako, karama na vipaji na huduma yako itabariki maisha ya wale unaowafundisha.