“Nyenzo za Ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili : Agano Jipya 2019 (2019)
“Nyenzo za Ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili; 2019
Nyenzo za Ziada
Nyingi kati ya nyenzo hizi zinaweza kupatikana katika Gospel Library app na kwenye LDS.org.
Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia
Unaweza kutohoa shughuli zozote kutoka nyenzo hii kwa matumizi katika darasa lako la Shule ya Jumapili. Kama washiriki wa darasa wametumia shughuli hizi katika mafunzo yao binafsi au familia, wahimize washiriki uzoefu na umaizi wao.
Majarida ya Kanisa
Majarida ya New Era, Ensign, na Liahona yanatoa makala na habari za ziada ambazo zinaweza kuongezea kanuni ambazo unafundisha kutoka Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili.
Nyimbo na Kitabu cha Nyimbo za Watoto
Muziki mtakatifu humwalika Roho na unafundisha mafundisho katika njia ya kukumbukwa. Kama nyongeza kwa matoleo yaliyochapishwa ya Nyimbo na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata nyimbo nyingi na nyimbo za watoto zilizorekodiwa kwenye music.lds.org na katika LDS Music app.
Maktaba ya Vyombo vya Habari
Sanaa za mchoro, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kupata taswira ya mafundisho na hadithi zilizopo katika Agano Jipya. Tembelea medialibrary.lds.org kupitiapitia mkusanyiko wa nyenzo za vyombo vya habari, ikijumuisha mfululizo wa Video za Biblia, ambazo zinaonyesha kwa mchoro matukio katika Agano Jipya.
Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo
Vitabu vya kiada vya seminari na chuo vinatoa usuli wa kihistoria na fasili ya mafundisho kwa kanuni zinazopatikana katika maandiko. Pia vina mawazo ya kufundishia ambayo yanaweza kutoholewa kwa ajili ya madarasa ya Shule ya Jumapili.
Mada za Injili
Kwenye topic.lds.org unaweza kupata taarifa za msingi kuhusu mada tofauti za injili, pamoja na viunganishi kwa nyenzo zenye msaada, kama vile hotuba zinazohusiana za mkutano mkuu, makala, maandiko, na video. Pia unaweza kupata Fasihi za Mada za Injili ambazo zinatoa majibu kwa kina kwa maswali ya injili.
Kweli kwa Imani
Nyenzo hii inatoa maelezo rahisi ya mada za injili, zilizoorodheshwa kwa mpangilio wa kialfabeti
Hubiri Injili Yangu
Mwongozo huu wa wamisionari hutoa maelezo ya jumla ya kanuni za msingi za injili.
Kwa Nguvu ya Vijana
Nyenzo hii inatoa muhtasari wa viwango gezi vya Kanisa ambavyo vinaweza kutusaidia kubaki tunaostahili kwa baraka za Bwana. Hususani kama unawafundisha vijana, fikiria kuirejelea mara kwa mara.
Kufundisha katika Njia ya Mwokozi
Nyenzo hii inaweza kukusaiia kujifunza kuhusu na kutumia kanuni za kufundisha za kama Kristo. Kanuni hizi zimejadiliwa na kujaribiwa katika mikutano ya halmashauri za mwalimu.