Njoo, Unifuate
Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili


“Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Iumapili,Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2019 (2019)

Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili,Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2019

Kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili

Kujiandaa Kufundisha katika Shule ya Jumapili

Nyumbani panapaswa kuwa kituo cha kujifunza injili. Hii ni kweli kwa ajili yako na kwa ajili ya wale unaowafundisha. Unapojiandaa kufundisha, anza kwa kuwa na uzoefu wako mwenyewe katika maandiko. Maandalizi yako muhimu yatatokea unapotafuta msukumo wa Roho Mtakatifu.

Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia pia ni sehemu muhimu ya maandalizi yako. Itakusaidia kupata uelewa wa kina wa kanuni za kimafundisho zinazopatikana katika maandiko. Utaweza pia kuwatia moyo na kuwataka washiriki wa darasa kutumia Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia kuboresha kujifunza maandiko kwao binafsi na kwa familia (kwa msaada katika kufanya hivi, ona “Mawazo ya Kuhimiza Kujifunza Binafsi na Familia” katika nyenzo hii). Unapofanya hivi, kumbuka kuwa mwepesi kuona washiriki wa darasa ambao familia zao mazingira yanaweza yasiweze kuruhusu kujifunza maandiko kwa familia kila mara.

Wakati wa maandalizi yako, mawazo na fikra itakuja kwako kuhusu watu unaowafundisha, jinsi kanuni katika maandiko zitakavyobariki maisha yao, na jinsi unavyoweza kuwatia moyo kuzigundua kanuni hizo wanapojifunza maandiko kwa ajili yao wenyewe.

Mawazo ya Kufundishia

Unapotengeneza mpango wako wa kufundishia, unaweza kupata mwongozo wa ziada kwa kuchunguza muhtasari katika nyenzo hii. Usifikiri mawazo haya kama maelekezo ya hatua kwa hatua bali kwa kiasi kama mapendekezo ya kuchochea mwongozo wako mwenyewe. Unawajua washiriki wa darasa lako, na Bwana anawajua pia. Atakupa mwongozo wa njia nzuri za kuwasaidia washiriki wa darasa kujenga juu ya kujifunza injili wanavyofanya majumbani mwao.

Una nyenzo zingine nyingi zinazopatikana unapojiandaa, ikijumuisha mawazo katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na majarida ya Kanisa. Kwa taarifa zaidi kuhusu hizi na nyenzo zingine, ona “Nyenzo za Ziada.”.

Baadhi ya Vitu vya Kuweka Akilini

  • Nyumbani ni sehemu bora zaidi kwa ajili ya kujifunza injili. Kama mwalimu, una wajibu muhimu kuhimili, kutia moyo, na kujenga juu ya kujifunza injili nyumbani.

  • Wongofu wa washiriki wa darasa katika injili ya Yesu Kristo utaongezeka wanapoelewa na kutumia mafundisho ya kweli. Wahimize waandike na kutenda juu ya ushawishi wanaopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu.

  • Kufundisha ni zaidi ya kutoa mhadhara, bali pia ni zaidi ya kuongoza tu mazungumzo. Sehemu ya wajibu wako ni kutia moyo ushiriki ambao unaadilisha na wenye msingi katika maandiko.

  • Baba wa Mbinguni anakutaka ufanikiwe kama mwalimu. Ametoa nyenzo nyingi kukusaidia ufanikiwe, ikijumuisha mikutano ya baraza la mwalimu. Katika mikutano hii unaweza kushauriana na walimu wengine kuhusu changamoto zozote unazoweza kukabiliana nazo. Unaweza pia kujadili na kufanyia mazoezi kanuni za kufundisha za kama Kristo.

  • Watu hujifunza vizuri wanapokuwa na nafasi ya kufundisha. Mara kwa mara, fikiria kuwaruhusu washiriki wa darasa, ukijumuisha vijana, kufundisha sehemu ya somo. Weka msingi wa uamuzi huu kwenye mahitaji na uwezo wa washiriki wa darasa. Kama unamtaka mshiriki wa darasa kufundisha, chukua muda kumsaidia kujiandaa mapema kwa kutumia mawazo yanayopatikana katika nyenzo hii na katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Kumbuka kwamba kama mwalimu aliyeitwa, unawajibika kwa kile kinachofundishwa katika darasa.

  • Nyenzo hii inajumuisha muhtasari kwa ajili ya kila wiki katika mwaka isipokuwa kwa Jumapili mbili wakati mkutano mkuu unapofanyika. Kwenye Jumapili ambazo Shule ya Jumapili haifanyiki kwa sababu ya mkutano mkuu wa kigingi au sababu yoyote, familia zinaweza kuendelea kusoma Agano Jipya nyumbani kufuatana na ratiba ya muhtasari. Ili kuweka darasa lako la Shule ya Jumapili kwenye ratiba, unaweza kuchagua kuruka somo au kuunganisha masomo mawili. Kuepuka mkanganyiko, marais wa Shule ya Jumapili wanaweza kuwashauri walimu wa Shule ya Jumapili kuhusu marekebisho haya kabla ya muda.

Chapisha