“Februari 13–19. Mathayo 5; Luka 6: ‘Heri Ninyi’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)
“Februari 13–19. Mathayo 5; Luka 6,” Njoo,Unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Februari 13–19
Mathayo 5; Luka 6
“Heri Ninyi ”
Andika misukumo ya kiroho unapojifunza Mathayo 5 na Luka 6. Ufunuo utakuja unapotafuta kukidhi mahitaji ya darasa lako.
Alika Kushiriki
Rais Joseph Fielding Smith alisema kwamba Mahubiri ya Mlimani ni “[mahubiri] muhimu sana yaliyowahi kuhubiriwa, kwa kadri tunavyojua” (Teachings of Presidents of the Church: Joseph Fielding Smith [2013], 234). Waalike washiriki wa darasa kuelezea hisia zao kuhusu kwa nini hili ni kweli.
Fundisha Mafundisho
Furaha ya kudumu huja kwa kuishi jinsi Yesu Kristo alivyofundisha.
-
Katika Mahubiri ya Mlimani, Mwokozi, aliwaalika wanafunzi Wake kufikiri upya kwamba inamaanisha nini kuishi maisha ya heri—maisha ya furaha yasiyo na kikomo. Kuanza majadiliano kuhusu furaha ya kudumu, ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki kitu kiachowafanya wao wawe na furaha. Kulingana na Mathayo 5:1–12, Yesu alisema ni nini kinamfanya mtu kuwa “mwenye heri,” au milele mwenye furaha? Ni kwa jinsi gani mafundisho ya Yesu ni tofauti na njia nyingine ambazo watu wanajaribu kutafuta furaha?
-
Fikiria kuandika ubaoni baadhi ya sifa au viwango kutoka marejeo kadhaa kutoka mstari wa 3–12, kama “walio safi moyoni” au “wapatanishi.” Kisha waalike washiriki wa darasa kupendekeza neno lililo kinyume chake. Tunajifunza nini kuhusu sifa hizi kwa kuzingatia kinyume chake? Waombe washiriki wa darasa kutafakari kile ambacho wanaweza kubadili ili kuwa aina ya mtu aliyeelezwa katika aya hizi. Ni nini 3 Nefi 12:3,6 inaongeza kwenye uelewa wetu wa Mathayo 5:3, 6?
Wafuasi wa Mwokozi wanatakiwa wawe nuru ya ulimwengu.
-
Ina maanisha nini kuwa “nuru ya ulimwengu”? (mstari wa 14). Ina maana gani kuficha nuru yetu “chini ya pishi” (aya ya 15), na kwa nini tunaweza kujaribiwa kufanya hivi? Maelezo ya Rais Bonnie H. Cordon katika “Nyenzo za Ziada” na 3 Nefi 18:24 yanaweza kusaidia washiriki wa darasa kuwa na dhamira zaidi kuhusu kuwa nuru kwa wengine. Wangeweza pia kuzungumza kuhusu watu ambao wamekuwa nuru kwao na kuwaongoza kuja kwa Yesu Kristo. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia watu hawa?
Yesu Kristo alifundisha sheria ya juu zaidi ambayo inaweza kutuongoza kwenye ukamilifu.
-
Baadhi ya hali zilizoelezwa katika Mathayo 5 zilikuwa mahususi kwa siku za Mwokozi, lakini kanuni Alizofundisha ni za wakati wote. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuona matumizi katika maisha yao, waalike wachague mojawapo ya vifungu vifutavyo na wafikirie mfano wa kisasa ambao unaonyesha kile Mwokozi alikuwa anafundisha: aya 21–24; 27–30; 33–37; 38–39; 40–42; na 43–44. Wanaweza kufanya hivi kibinafsi au katika vikundi vidogo vidogo na kushiriki mifano yao na darasa.
-
Unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kuona kwamba amri ya Mwokozi ya kuwa “wakamilifu” (Mathayo 5:48) inamaanisha, kama Rais Russell M. Nelson alivyoelezea, kuwa “kamili” au “waliotimia”? (“Perfection Pending” Ensign, Nov. 1995, 86–88). Ungeweza kukata picha ya Yesu uifanye kuwa chemsha bongo, na waalike washiriki wa darasa kuandika nyuma ya kila kipande mafundisho kutoka Mathayo 5 ambayo wanahisi kutiwa moyo kuyatumia katika maisha yao. Waache wafanye kazi pamoja kukamilisha hiyo chemsha bongo. Ni kwa jinsi gani Upatanisho wa Yesu Kristo unatusaida sisi “kukamilika” au “kutimia?” (ona Kamusi ya Biblia “Grace”). Maneno ya Rais Joy D. Jones katika “Nyenzo za Ziada” yanaongeza nini katika uelewa wetu juu ya mchakato huu?
Nyenzo za Ziada
Kuwa nuru.
Rais Bonnie H. Cordon alifundisha: Mwaliko wa Bwana wa kuacha nuru yetu iangaze si tu kuhusu kupunga bila utaratibu mwali wa mwanga na kufanya ulimwengu kwa ujumla angavu. Ni kuhusu kufokasi nuru yetu ili wengine waweze kuona njia ya kwenda kwa Kristo. Ni kukusanya Israeli upande huu wa pazia—kuwasaidia wengine kuona hatua inayofuata kwenda mbele katika kufanya na kushika maagano na Mungu” (“Ili Wapate Kuona,” Liahona, Mei 2020, 79).
Kutafuta ukamilifu.
Rais Joy D. Jones alielezea:
“Bwana anapenda jitihada, na jitihada huleta tuzo. Tunaendelea kufanya mazoezi. Sisi daima tunaendelea kadiri tunavyojitahidi kumfuata Bwana. Yeye hatarajii ukamilifu leo. Tunaendelea kupanda Mlima wetu binafsi wa Sinai. Kama nyakati zilizopita, safari yetu hakika inahitaji jitihada, bidii na kujifunza, lakini nia yetu thabiti ya kuendelea huleta tuzo za milele. …
“Acha tutangaze kwa ujasiri kujitolea kwetu kwa Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu, ‘kwa imani isiyotingishika ndani yake, tukitegemea kabisa ustahili wa yule aliye mkuu katika kuokoa’ [2 Nefi 31:19]. Acha kwa furaha tuendeleze safari hii kuelekea uwezekano wetu wa juu zaidi” (“Wito Mkuu Mahususi,” Liahona, Mei 2020, 16–17).