Agano Jipya 2023
Februari 20–26. Mathayo 6–7: “Aliwafundisha kama Mtu Mwenye Mamlaka”


“Februari 20–26. Mathayo 6–7: ‘Aliwafundisha Kama Mtu Mwenye Mamlaka’” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Februari 20–26. Mathayo 6–7,” Njoo,Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Yesu Akifundisha kwenye ufukwe wa bahari

Yesu Akifundisha Watu kwenye Ufukwe wa Bahari, na James Tissot

Februari 20–26

Mathayo 6–7

“Aliwafundisha Kama Mtu Mwenye Mamlaka”

Unapojiandaa kufundisha, anza kwa kujiandaa mwenyewe. Jifunze Mathayo 6–7, na uandike misukumo ya kiroho. Hii itakusaidia kupokea ufunuo juu ya jinsi bora ya kukidhi mahitaji ya darasa lako. Kisha pekua muhtasari huu kwa ajili ya mawazo ya kufundishia.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike washiriki wa darasa kushiriki vifungu katika Mahubiri ya Mlimani ambayo wanadhani vinahitajika sana leo. Wahimize washiriki wa darasa kuongeza juu ya umaizi wa kila mmoja.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 6–7

Kama tutasikia na kutenda juu ya mafundisho ya Bwana, maisha yetu yatakuwa yamejengwa juu ya msingi imara.

  • Ni mafundisho gani maalumu kutoka Mathayo 6–7 yatakuwa yenye manufaa zaidi kwa wale unaowafundisha? Fikiria kuandika ubaoni marejeleo kadhaa kutoka Mathayo 6–7 ambayo yana mafundisho haya. Washiriki wa darasa wanaweza kuchagua mojawapo ya marejeleo hayo kujisomea kimya kimya na kisha waandike ubaoni kweli zozote za kiroho wanazojifunza. Ni kwa jinsi gani mafundisho haya yameshawishi maisha yetu?

  • Mwokozi alihitimisha mahubiri Yake kwa fumbo ambalo linaweza kusaidia darasa lako kuelewa vizuri umuhimu wa kuishi kwa mafundisho ya Mwokozi (ona Mathayo 7:24–27; ona pia Helamani 5:12). Ili kupata taswira ya fumbo hili, washiriki wa darasa wanaweza kufanya kazi pamoja ya kujenga msingi imara kwa kutumia matofali, vikombe, au vifaa vingine na kisha kupima uthabiti wa misingi yao. Labda wanaweza pia kuwekea alama vifaa vyao vya ujenzi pamoja na vitu wanavyoweza kufanya ili kutumia mafundisho ya Mwokozi. Ni kwa jinsi gani kufanya vitu hivyo kungetusaidia sisi kustahmili dhoruba za maisha?

Mathayo 6:5–13

Mwokozi alitufundisha jinsi ya kusali.

  • Kujifunza Sala ya Bwana kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutambua jinsi wanavyoweza kuboresha sala zao wenyewe kwa kufuata mfano wa Bwana. Ungeweza kuwaalika waandike ubaoni virai kutoka Mathayo 6:9–13 (au Luka 11:1–4) ambavyo vinajitokeza kwa kipekee kwao. Tunapotafakari maneno ya Mwokozi, tunajifunza nini kuhusu sala? Inaweza kuwa ya kuelemisha kwa washiriki wa darasa kufafanua baadhi ya misemo ya Mwokozi kama vitu wanavyoweza kusema katika sala zao wenyewe. Kwa mfano, “Utupe leo mkate wetu wa kila siku” ingeweza kufafanuliwa kama “Tafadhali nisaidie katika juhudi zangu za kuikimu familia yangu.”

  • Baada ya kusoma Yohana 6:5–13 kama darasa, mnaweza kujadili maswali kama haya: Je, ni kwa jinsi gani sala imeimarisha uhusiano wako wewe na Baba wa Mbinguni? Je, ni kwa jinsi gani sala imekusaidia wewe kujua mapenzi ya Mungu?

Mathayo 7:7–11

Baba wa Mbinguni anajibu sala.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuimarisha imani yao kwamba Mungu atasikia na kujibu sala zao, unaweza kuandika omba, tafuta, na bisha ubaoni. Kisha waalike washiriki wa darasa kutafuta maandiko kwa ajili ya mifano ya watu ambao “waliomba,” “walitafuta,” na “walibisha” (kwa mfano, ona 1 Nefi11:1; Etheri 2:18–3:6; Joseph Smith—Historia 1:11–17) Tunajifunza nini kutokana na mifano hii kuhusu kupata majibu kwa sala zetu?

  • Baadhi ya maudhui muhimu kwa Mathayo 7:7–11 yanaweza kupatikana katika Tafsiri ya Joseph Smith ya Mathayo 7:17 (katika kiambatisho cha Biblia). Katika aya hizi, wafuasi wa Yesu walibashiri baadhi ya sababu ambazo watu wangeweza kuzitoa kwa kutotafuta ukweli kutoka kwa Baba wa Mbinguni. Unaweza kuwauliza washiriki wa darasa kufikiria kuwa wanaye rafiki ambaye hataki kutafuta mwongozo au baraka kutoka kwa Bwana. Washiriki wa darasa wanaweza kusema nini ili kumhimiza rafiki huyu? Ni kwa jinsi gani wanaweza kutumia maneno ya Mwokozi katika Mathayo 7:7–11?

Mathayo 7:15–20

Tunaweza kuwatambua manabii wa kweli na wa uongo kwa matunda yao.

  • Washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa wamewahi kukutana na falsafa za uongo na udanganyifu mwingine wa adui, ama kwenye mtandao au kutoka katika vyanzo vingine. Yawezekana pia wamewahi kusikia wengine wakiwalaumu watumishi wa Bwana. Unawezaje kuwasaidia kuelewa jinsi ya kuwatambua manabii wa uongo na mafundisho kutoka kwa wale wa kweli? Unaweza kuonyesha vipande kadhaa vya matunda na kuuliza ni nini tunaweza kudhania kuhusu miti ambapo matunda hayo yametoka. Ni kwa jinsi gani zoezi hili linatusaidia kuelewa Mathayo 7:15–20? Mngeweza pia kusoma pamoja baadhi ya jumbe za hivi karibuni kutoka kwa manabii wanaoishi. Ni “matunda” au matokeo gani yanakuja kutokana na kufuata ushauri wao?

    Picha
    tunda

    Tunaweza kuwajua manabii wa kweli kwa matunda yao.

  • Mathayo 7:15–20 inaweza kusaidia kujenga imani ya washiriki wa darasa katika misheni takatifu ya Nabii Joseph Smith. Je, ni yapi matunda ya kazi iliyotimizwa na Joseph Smith? Kwa baadhi ya mawazo, ona ujumbe wa Mzee Neil L. Andersen “Joseph Smith” (Liahona, Nov. 2014, 28–31). Ni kwa jinsi gani tungeweza kutumia analojia ya Mwokozi katika Mathayo 7:15–20 kutoa ushuhuda kwa marafiki zetu na familia kuhusu Nabii Joseph?

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Usiogope ukimya. “Maswali mazuri huchukua muda kuyajibu. Yanahitaji kutafakari, kutafiti na mwongozo wa kiungu. Muda unaotumia kungoja majibu kwa swali unaweza kuwa wakati mtakatifu wa kutafakari. Epuka jaribu la kukatisha muda huu mapema kwa kujibu swali lako mwenyewe au kwenda kwenye jambo jingine” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi31).

Chapisha