“Februari 25–Machi 5. Mathayo 8; Marko 2–4; Luka 7: ‘Imani Yako Imekuponya’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shuie ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)
“Februari 27–Machi 5. Mathayo 8; Marko 2 –4; Luka 7,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Februari 27–Machi 5
Mathayo 8; Marko 2 –4; Luka 7
“Imani Yako Imekuponya”
Maandalizi yako ya kufundisha yanaanza unapojifunza kwa maombi Mathayo 8; Marko 2–4; na Luka 7. Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia inaweza kuboresha kujifunza kwako na kuchochea mawazo ya kufundisha zaidi ya yale yaliyowasilishwa hapa.
Alika Kushiriki
Washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa wamepata umaizi wenye nguvu wakati wa kujifunza binafsi juu ya miujiza katika sura hizi (ona orodha ya uponyaji wa Mwokozi katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki umaizi wao na mwenza au na darasa zima.
Fundisha Mafundisho
Miujiza inatokea kulingana na mapenzi ya Mungu na imani yetu katika Yesu Kristo.
-
Je, unawezaje kutumia hadithi za miujiza ya Mwokozi ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuongeza imani yao Kwake? Unaweza kuwaomba kuorodhesha ubaoni miujiza kadhaa ya uponyaji kutoka Mathayo 8; Marko 2; na Luka 7. Washiriki wa darasa wangeshiriki jinsi ambavyo watu hao walivyoonyesha imani yao katika Kristo. Je, hadithi hizi zinatufundisha nini kuhusu imani na miujiza? Washiriki wa darasa wangeweza kueleza kweli za ziada kuhusu imani na miujiza kutoka Mormoni 9:15–21; Etheri 12:12–16; Moroni 7:27–37; na Mafundisho na Maagano 35:8 (ona pia Kamusi ya Biblia, “Miujiza”) Je, ni lini tuliona miujiza pale tulipofanyia kazi imani katika Yesu Kristo?
-
Hadithi ya muujiza katika Marko 2:1–12 inafundisha, miongoni mwa vitu vingine, thamani ya kufanya kazi pamoja katika umoja ili kumsaidia Mwokozi katika utumishi kwa wale walio na mahitaji ya kiroho na kimwili. Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kurejelea hadithi kutoka kwenye maandiko na kushiriki utambuzi wa ziada kutoka katika ujumbe wa Mzee Chi Hong (Sam) Wong “Okoa katika Umoja” (Liahona, Nov. 2014, 14–16; ona pia “Nyenzo za Ziada”). Tunajifunza nini kutoka Marko 2:1–12 kuhusu faida ya kufanya kazi pamoja kuwahudumia wale walio katika shida? (Ona pia Marko 3:24–25)
Yesu Kristo ana uwezo wa kuleta amani katikati ya dhoruba za maisha.
-
Unaweza kufahamu baadhi ya changamoto washiriki wa darasa lako wanakabiliana nazo. Kwa sababu sisi wote tunakuwa na majaribu wakati fulani katika maisha yetu, kurejelea matukio katika Marko 4:35–41 kunaweza kujenga imani ya washiriki wa darasa kwamba Mwokozi anaweza kuwaletea amani. Mpe kila mtu kipande cha karatasi, na waombe waandike kwenye upande mmoja wa karatasi jaribu walilopitia. Upande mwingine, waombe waandike kitu fulani kutoka Marko 4:35–41 kile kinachowavutia kumgeukia Mwokozi wakati wa majaribu yao. Wahimize washiriki wa darasa kushiriki kile walichoandika, ikiwa watajisikia vizuri kufanya hivyo.
-
Wimbo “Master, the Tempest Is Raging,” (Nyimbo za Kanisa, na.105) msingi wake ni hadithi katika Mathayo 4:35–41. Labda washiriki wa darasa wanaweza kutafuta mashairi katika wimbo ambayo yanahusiana na virai katika maandiko. Unaweza pia kuonyesha picha inayoonyesha tukio hilo (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 40) na jadili ni muda gani msanii anauonesha. Ni njia gani zingine ungeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa maana na nguvu ya muujiza huu?
Tunaposamehewa dhambi zetu, upendo wetu kwa Mwokozi unaongezeka.
-
Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wa mwanamke na mafundisho ya Mwokozi katika Luka 7:36–50 tunapotafuta msamaha wa dhambi zetu wenyewe? Je, ni kwa jinsi gani toba inatusaidia kujongea karibu na Yesu Kristo? Je, ni kwa jinsi gani hadithi hii inashawishi njia tunayowatazama wale walio tenda dhambi?
Nyenzo za Ziada
“Naye Yesu, alipoiona imani yao.”
Mzee Chi Hong (Sam) Wong alishiriki utambuzi ufuatao kuhusu hadithi katika Marko 2:1–12:
Naomba kushiriki nanyi hazina nyingine moja iliyofichika inayopatikana katika hadithi hii ya maandiko. Iko katika mstari wa 5: ‘Naye Yesu, alipoiona imani yao’ (msisitizo umeongezwa). Sikuwa nimegundua jambo hili katika siku za nyuma—imaniyao. ….
Ni akina nani ambao Yesu aliwataja? Wangeweza kujumuisha wale wanne ambao walimbeba mtu mwenye kupooza, mtu mwenyewe, watu ambao walikuwa wamemuombea na wale wote ambao walikuwa pale wakisikiliza mahubiri ya Yesu na kushangilia kimya kimya katika mioyo yao kwa ajili ya muujiza uliotarajia kutokea hivi punde. Wangeweza kujumuisha pia mwenzi, mzazi, mwana au binti, mmisionari, rais wa akidi, rais wa Muungano wa Usaidizi, askofu na rafiki aliye mbali. Sote tunaweza kusaidiana. Tunapaswa daima tujishughulishe kwa shauku katika kutafuta kuwaokoa wale walio katika shida” (“Kuokoa katika Umoja,” Liahona, Nov. 2014, 16). .