Agano Jipya 2023
Machi 20-26. Mathayo 13; Luka 8; 13: “Mwenye Masikio na Asikie”


“Machi 20-26. Mathayo 13; Luka 8:13: ‘Mwenye Masikio na Asikie’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Machi 20-26. Mathayo 13; Luka 8; 13” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili; 2023

ngano tayari kuvunwa

Machi 20-26

Mathayo 13; Luka 8;13

“Mwenye Masikio, na Asikie”

Unaposoma, fikiria maswali washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa nayo wanapojaribu kuelewa ujumbe wa mafumbo haya. Je, ni niini kinaweza kuwa kigumu kuelewa? Kujifunza kwako kunawezaje kukuandaa kujibu maswali yao?

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Rejea pamoja na darasa “Mawazo ya Kuboresha Kujifunza Kwako Binafsi Maandiko” katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waalike washiriki wa darasa kushiriki njia walizotumia kujifunza Mathayo 13 na Luka 813.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 13:1–23

Mioyo yetu lazima itaandaliwe kupokea neno la Mungu.

  • Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia fumbo la mpanzi kuwatia moyo washiriki wa darasa lako kuandaa mioyo yao kupokea neno la Mungu? Unaweza kuandika Wafuasi na Wengine ubaoni. Waalike washiriki wa darasa kusoma Mathayo 13:10–17 na kutafuta jinsi Mwokozi alivyoelezea tofauti kati ya wafuasi Wake na wengine waliosikia mafumbo Yake. Kisha waombe washiriki wa darasa wapekue aya 18–23, wakitafuta nini kinaweza kusababisha masikio yetu kuwa “mazito kusikia” au macho yetu kufungwa kwa vitu vya kiroho. Mwelekeo gani tunaoupokea katika siku zetu kutoka kwa Mungu na watumishi Wake? Je, tunawezaje kulima “udongo mzuri” ili tupokee maelekezo? (mstari wa 23).

  • Unaweza kuwaalika washiriki wachache wa darasa kila mmoja aje amejiandaa kufundisha kifungu kutoka kwenye ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Fumbo la Mpanzi” (Liahona, Mei 2015, 32–35). Ujumbe wake unaongeza nini katika uelewa wetu wa fumbo hili?

Mathayo 13:24–35, 44–53

Mafumbo ya Yesu yanatusaidia kuelewa ukuaji, hatima, na thamani ya Kanisa Lake.

  • Utawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa kweli kuhusu Kanisa ambazo zilifundishwa katika mafumbo ya Yesu katika Mathayo 13? Unaweza kuorodhesha mafumbo machache ubaoni (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Watu Binafsi na Familia na Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith, 293–303). Washiriki wa darasa wanaweza kusoma moja au zaidi kibinafsi au katika vifungu vidogo vidogo na kushiriki wanachojifunza kuhusu ukuaji na hatima ya Kanisa la Kristo.

mtu akivua kwa wavu

Ufalme wa mbinguni ni kama wavu wa mvuvi.

  • Tunajifunza nini kuhusu thamani ya kustahili kuwa katika Kanisa kutoka kwa mafumbo ya hazina katika shamba na lulu ya thamani kuu, yanayopatikana katika Mathayo 13:44–46? Baadhi ya washiriki wa darasa lako (au watu wanaowajua) wamefanya dhabihu—iwe ni kubwa au ndogo—ili kuwa waumini wa Kanisa. Waalike washiriki wa darasa kushiriki dhabihu walizofanya au kuona wengine wakifanya ili kuwa wa Kanisa hili. Ni baraka gani zimekuja kama matokeo? Waalike washiriki wa darasa kutafakari nini wanahisi kushawishika kutoa dhabihu kwa ajili ya Kanisa.

Mathayo 13:24–30, 36–43

Hapo mwisho wa ulimwengu, Bwana atawakusanya wenye haki na kuwaangamiza waovu.

  • Ni kwa jinsi gani utaweza kusaidia darasa lako kujifunza masomo kutoka fumbo la ngano na magugu ambayo yatawasaidia kubaki Watakatifu wa Siku za Mwisho waaminifu? Anza kwa kumwalika mshiriki wa darasa kufupisha fumbo na tafsiri yake. Ni yapi baadhi ya masomo katika fumbo hili ni kwa ajili ya siku yetu? Kwa nini ni muhimu kujua kwamba Bwana anaruhusu Watakatifu Wake “kukua pamoja” (Mathayo 13:30) na waovu mpaka wakati wa mavuno? Tunawezaje kushika imani yetu katika Yesu Kristo imara wakati uovu umetuzunguka kote? Kristo anawezaje kutusaidia sisi? Mafundisho na Maagano 86:1–7 na maelezo ya Mzee L. Tom Perry’ “Nyenzo za Ziada” yanaweza kutoa utambuzi wa ziada katika matumizi ya siku za mwisho ya fumbo hili.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Tunapaswa kustawisha kilicho bora.

Mzee L. Tom Perry alifundisha: “Yule adui wa kale wa wanadamu wote amepata vifaa vingi kadiri awezavyo kufikiria ili kutawanya magugu mbali na kwa mapana. Amepata njia ya kuyafanya yapenyeze katika hata utakatifu wa nyumba zetu wenyewe. Njia za uovu na mambo ya kilimwengu yamesambaa huko na kuonekana kama hakuna njia ya kuyang’oa kabisa. Yanakuja kwa njia ya waya na kupitia hewani hadi ndani ya vifaa tulivyo vitengeneza ili kutuelimisha na kutuburudisha. Ngano na magugu vyote vimekua karibu kwa pamoja. Mtumishi atunzaye shamba lazima, kwa nguvu zake zote, lazima akirutubishe kilicho bora na kukifanya kiwe imara na cha kupendeza ili magugu yasiwe na mvuto kwa macho au masikio.” (“Kupata Amani Isiyo na Kikomo na Kujenga Familia za Milele,” Liahona, Nov. 2014,44).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Lenga ufundishaji wako kwenye mafundisho. Hakikisha majadiliano ya darasa lako yanajikita katika mafundisho ya kimsingi katika maandiko. Unaweza kufanya hivi kwa kuwaomba wanafunzi wasome maandiko mapema, ukikita majadiliano ya darasa kwenye maandiko, na kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki shuhuda zao juu ya mafundisho ya kweli. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 20–21.)