Agano Jipya 2023
Machi 27–Aprili 2. Mathayo 14; Marko 6; Yohana 5–6: “Msiogope”


Machi 27–Aprili 2. Mathayo 14: Marko 6: Yohana 5–6: ‘Msiogope’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

Machi 27–Aprili 2. Mathayo 14; Marko 6; Yohana 5–6.” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Yesu anatembea na wafuasi wakiwa wamebeba vikapu vya mikate

Machi 27–Aprili 2

Mathayo 14; Marko 6; Yohana 5–6

“Msiogope”

Unapojiandaa kufundisha kutoka Mathayo 14; Marko 6; na Yohana 5–6, tafuta jumbe ambazo zinahusika na darasa lako. Unapofanya hivyo, fikiria jinsi ya kuwaunganisha washiriki wa darasa katika uzoefu wenye maana na maandiko.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Njia mojawapo ya kuanza majadiliano ya sura hizi ni kuwaalika washiriki wa darasa wachache kila mmoja kuchagua sura kutoka kwenye somo na kuja amejiandaa kushiriki kifungu kutoka sura ile ambacho kilikuwa chenye maana kwao. Wanaposhiriki, washiriki wengine wa darasa wanaweza kuuliza maswali au kuongeza umaizi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Yohana 5:16–47

Yesu Kristo ni Mwana Mpendwa wa Baba wa Mbinguni.

  • Katika Yohana 5, Yesu alitoa utambuzi kadhaa kuhusu Yeye Mwenyewe, Baba Yake, na uhusiano Wake kwa Baba. Ili kusaidia darasa kugundua umaizi huu, jaribu kuwagawa katika vikundi na uwape dakika chache kuorodhesha kweli nyingi kadiri wawezavyo kuzipata katika mistari ya 16–47 kuhusu hulka ya Mungu, Yesu Kristo na uhusiano Wao. Waalike vikundi kupeana zamu kusoma kweli hizo kutoka kwenye orodha zao. Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinatusaidia kumwelewa vyema Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe? Tunawezaje kufuata mfano wa Yesu Kristo wa utii kwa Baba?

  • Shughuli katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia inapendekeza kuandika kila wakati Yesu alipotumia neno Baba katika Yohana 5: 16–47. Waalike washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza walipokamilisha shughuli. Waulize ni umaizi gani walioupata kuhusu Baba wa Mbinguni na Mwanawe Mpendwa?

Mathayo 2:15–21; Marko 6:33–44; Yohana 6:5–14

Mwokozi anaweza kukuza matoleo yangu haya madogo ili kufikia malengo Yake.

  • Je, ni kitu gani kingeweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata maana binafsi ya muujiza wa Yesu kuwalisha wale elfu tano? Unaweza kuuliza jinsi gani kusoma kuhusu miujiza kunaongeza imani yao katika uwezo wa Mwokozi ili kuwabariki wao binafsi. Wangeweza kuzungumza kuhusu wakati walipojisikia kwamba Mwokozi amezidisha jitihada zao ili kuwasaidia wakamilishe kitu ambacho kilionekena hakiwezekani. Pia, kabla ya darasa ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa kuleta darasani picha au kitu ambacho kinawakilisha uzoefu wao

    Picha
    mikate na samaki

    Yesu aliwalisha watu 5000 kimiujiza kwa mikate mitano na samaki wawili.

  • Video “Tha Feeding of the 5,000” (ChurchofJesusChrist.org) inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari muujiza ulioelezwa katika vifungu hivi. Je, ni maelezo gani ya kina katika hadithi hii yanaongeza imani yetu katika Mwokozi? Je, ni kwa njia zipi Mwokozi anaweza kutulisha sisi kiroho? Je, ni lini tumelishwa na kusaidiwa na Yesu Kristo?

Mathayo 14:22–33

Yesu Kristo anatualika tuweke kando hofu zetu na wasiwasi ili kwamba tuweze kusogea kikamilifu Kwake.

  • Tukio katika Mathayo 14:22–23 linaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuongeza imani yao katika Mwokozi na hamu yao ya kumfuata. Waalike washiriki wa darasa kusoma tukio hili, wakitoa usikivu makini wa kipekee kwa maneno yaliyosemwa na Kristo, Petro na Mitume wengine. Ni kwa jinsi gani maneno ya Yesu yangeliweza kumsaidia Petro kuwa na imani na kuacha mashua na kutembea juu ya maji? Ni kwa jinsi gani onyo la Yesu la “furahini” na “msiogope” (aya 27) linatumika kwetu leo? Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa Petro kuhusu kile kinachomaanishwa kuwa mfuasi wa Yesu Kristo na kumtumaini Yeye? Unaweza kuwahimiza washiriki wa darasa kufikiria kuhusu na kushiriki uzoefu ambamo wao, kama Petro, walichukua hatua kumfuata Mwokozi, hata wakati matokeo yalikuwa hayana uhakika. Waombe washiriki kile walichojifunza kutokana na uzoefu wao. Ni kwa jinsi gani Yesu amekuja kutuokoa katika nyakati zetu za hofu au mashaka?

Yohana 6:22–71

Kama wafuasi wa Kristo, lazima tuwe tayari kuamini na kukubali ukweli hata wakati ambapo ni vigumu kufanya hivyo.

  • Matukio katika Yohana 6 yanaweza kutoa taswira ya usaidizi wakati watu wanapohoji kuhusu mafundisho, historia, au sera za Kanisa la Kristo. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa matukio haya, unaweza kuandika maswali kama yafuatayo ubaoni nao wayajibu: Watu walikuwa wakitegemea nini? (ona mstari wa 26). Kristo aliwapatia nini badala yake? (ona mstari wa 51). Je, n kitu gani watu walikielewa vibaya? (ona mstari wa 41–42, 52). Ungeweza pia kuuliza maswali kama haya ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuitumia hadithi hii kwenye maisha yao: Ni njia gani nyingine tunaweza kuchagua kutembea pamoja na Kristo hata wakati tunapokuwa na maswali au mashaka? (Ona mstari wa 66). Ni yapi baadhi ya mafundisho, ibada au “maneno ya uzima wa milele” mengine ambayo yanaweza kupatikana tu katika Kanisa la urejesho? (Ona mstari wa 67–69). Kwa utambuzi kutoka kwa Mtume wa sasa, ona ujumbe wa Rais M. Russell Ballard “Tutakwenda kwa Nani?,” (Liahona, Nov. 2016, 90–92).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Sikiliza. “Kusikiliza ni tendo la upendo. … Muombe Baba wa Mbinguni akusaidie kuelewa kile washiriki wa darasa lako wanasema. Unapotoa usikivu wa umakini kwa jumbe zao zinazozungumzwa na zisizozungumzwa, utakuja kuelewa vyema mahitaji yao, mashaka yao, na matamanio yao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi34).

Chapisha