Agano Jipya 2023
Aprili 3–9. Pasaka: “Ee Kaburi, U Wapi Ushindi Wako?”


“Aprili 3–9. Pasaka: ‘Ee Kaburi, U Wapi Ushindi Wako?,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2023 (2022)

“Aprili 3–9. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Bustani ya Kaburi.

Aprili 3–9

Pasaka

“Ee Kaburi U Wapi Ushindi Wako?”

Unapojiandaa kufundisha wiki hii, fikiria jinsi majadiliano ya darasa lako kuhusu Jumapili ya Pasaka yavyoweza kujenga imani katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waulize washiriki wa darasa jinsi watakavyojibu maswali kama “Upatanisho wa Yesu Kristo ni nini?” na “Ninawezaje kupokea baraka za Upatanisho wa Kristo? Waalike kushiriki andiko lolote walilosoma wiki hii ambalo linasaidia kujibu maswali haya.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Yesu Kristo anatuokoa sisi kutokana na dhambi na kifo, anatuimarisha katika udhaifu wetu na anatufariji katika majaribu yetu.

  • Je, washiriki wa darasa lako wanaelewa kwamba Yesu anatufariji katika majaribu yetu na kutuimarisha katika udhaifu wetu, vilevile kutuokoa kutokana na dhambi na mauti? Njia mojawapo ya kuwasaidia kugundua kanuni hizi ingeweza kuwa kuandika maneno haya ubaoni: Dhambi, Kifo, Majaribu, Udhaifu. Kila mshiriki wa darasa angeweza kusoma mojawapo ya maandiko yaliyoorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada” na kutakafari jinsi Mwokozi anavyotusaidia kushinda au kuvumilia vitu hivi. Washiriki wa darasa wanaweza kisha kuandika kile walichojifunza kutoka katika maandiko haya chini ya kila kichwa cha habari na kushiriki ushuhuda wao juu ya Mwokozi na Upatanisho Wake.

    Picha
    Yesu msalabani

    Kusulubiwa, na Louise Parker

  • Pengine somo la kitu rahisi lingeweza kusaidia kuonyesha tofauti kati ya kusafishwa kutokana na dhambi na kufanywa mkamilifu: Ungeweza kuandika ubaoni mistari michache ya mwanzo kutoka Moroni 10:32, lakini jumuisha makosa ya tahajia au ya kisarufi. Kisha mwalike mshiriki wa darasa kufuta (bila kusahihisha) makosa. Je, hii ilitatua tatizo? Ni masomo gani tunayojifunza kutoka kwenye andiko hili na somo hili la vitendo kuhusu madhara ambayo Upatanisho unaweza kuwa nayo kwetu. Kauli hii kutoka kwa Rais Dieter F. Uchtdorf inaweza pia kusaidia: “Kama wokovu unamaanisha kufuta makosa na dhambi zetu tu, basi wokovu—kwa uzuri ulivyo—haukamilishi hamu ya Baba kwetu sisi. Nia yake ni ya juu zaidi: Anawataka wana na mabinti zake kuwa kama Yeye” (“Kipawa cha Neema,” Liahona, Mei 2015,108).

  • Hadithi na anolojia vinaweza kutusaidia kuelewa vyema Upatanisho wa Kristo. Ungetaka kushiriki hadithi au analogia kutoka ujumbe mmojawapo wa mkutano mkuu katika “Nyenzo za Ziada.” Au mnaweza kutazama pamoja “Handel’s Messiah: Debtor’s Prison” (video), ChurchofJesusChrist.org, na kujadiliana jinsi Upatanisho wa Yesu Kristo unavyotuweka huru kutokana na magereza yetu. Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mawazo yoyote na hisia walizo nazo juu ya Mwokozi na Upatanisho Wake kwa ajili yetu.

Mathayo 28:1–10; Luka 24:13–35; Yohana 20:1–29; 1 Wakorintho 15:3–8, 55– 58

Mashahidi katika Agano Jipya walitoa ushuhuda kwamba Yesu Kristo alishinda kifo.

  • Fikiria kurejelea hadithi za kimaandiko juu ya Pasaka ya kwanza—Kufufuka kwa Yesu Kristo. Unaweza kumwambia mshiriki wa darasa kueleza tena hadithi katika maneno yake mwenyewe (ona Yohana 20:1–17). Unaweza pia kuonyesha video ya Biblia, kama vile “He Is Risen” (ChurchofJesusChrist.org).

  • Labda darasa lako lingepata kwa undani zaidi uelewa wa umuhimu wa mashahidi wa Kufufuka kwa Yesu Kristo kama wanajifikiria wao ni wanasheria au waandishi wa habari wanaopeleleza madai kwamba Kristo alifufuka. Waalike wao watafute watu katika maandiko ambao wangehudumu kama mashahidi (ona Mathayo 28:1–10; Luka 24:13–35; Yohana 20:19–29; 1 Wakorintho 15:3–8, 55–58). Wanaweza hata kuandika muhtasari mfupi wa nini watu hawa wangeweza kusema wakati wa kushuhudia katika mahakama au wakati wakihojiwa kwa ajili ya taarifa ya habari.

  • Njia mojawapo ya kuongeza shukrani zetu kwa kina kwa ajili ya Kufufuka kwa Mwokozi ni kufikiria kuhusu jinsi tutakavyoelezea imani zetu kwa wengine. Washiriki wa darasa wangewezaje kushiriki shuhuda zao juu ya Yesu Kristo katika hali zifuatazo: mwana familia amebainika ana ugonjwa wa hatari; rafiki amempoteza mpendwa wake; jirani anauliza kwa nini mnasherehekea Pasaka. Wahimize warejelee kwenye maandiko (kama hayo katika “Nyenzo za Ziada” wanapoyapanga majibu yao. Waalike washiriki wachache wa darasa kushiriki mawazo yao.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Maandiko kuhusu Upatanisho wa Mwokozi na Ufufuko.

Jumbe kuhusu Upatanisho wa Mwokozi na Ufufuko.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Uwe chombo cha Roho. “Lengo lako kama mwalimu sio kuwasilisha somo lenye kuvutia bali ni kuwasaidia wengine kupokea ushawishi wa Roho Mtakatifu, ambaye ni mwalimu wa kweli” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi10).

Chapisha