Agano Jipya 2023
Aprili 10–16. Mathayo 15–17; Marko 7–9: “Wewe Ndiwe Kristo”


“Aprili 10–16. Mathayo 15–17: Marko 7– 9: ‘Wewe ndiwe Kristo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Aprili 10–16. Mathayo 15–17; Marko 7–9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Kugeuka Sura kwa Kristo

Kugeuka sura, na Carl Heinrich Bloch

Aprili 10–16

Mathayo 15–17; Marko 7–9

“Wewe Ndiwe Kristo”

Moja ya malengo yako makuu kama mwalimu ni kuwasaidia wengine kujenga imani yao katika Yesu Kristo. Weka hili akilini mwako unapojifunza maandiko wiki hii. Je, unapata nini ambacho kinaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kumwamini Yeye kwa kina zaidi?

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Njia mojawapo unaweza kuwahimiza washiriki wa darasa kujifunza maandiko kibinafsi na pamoja na familia zao ni kuwaalika kushiriki kila wiki jinsi mafunzo yao ya maandiko yalivyowasaidia kupokea ushuhuda na kubariki maisha yao. Kwa mfano, jinsi gani mafunzo yao ya sura hizi yanashawishi chaguzi zao walizofanya wiki hii?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 4:13–17

Ushuhuda wa Yesu Kristo unakuja kwa ufunuo.

  • Je, kuna mshiriki wa darasa yeyote aliyewahi kumwelezea mtu jinsi wanavyojua kwamba injili ni kweli? Katika Mathayo 16:13–17, Mwokozi alifundisha nini kuhusu jinsi tunavyopokea ushuhuda? Ungeweza kushiriki jinsi Alma alivyopata ushuhuda wake (ona Alma 5:45–46) au kitu ambacho Bwana alimfundisha Oliver Cowdery kuhusu ufunuo (ona Mafundisho na Maagano 6:14–15, 22–23; 8:2–3). Unafikiri Petro au Alma au Oliver Cowdery wangeweza kusema nini kama mtu angewauliza jinsi wanavyojua kwamba injili ni kweli?

  • Kunaweza kuwa na watu katika darasa lako ambao wanaomba kwa ajili ya ufunuo binafsi lakini hawajui jinsi ya kuutambua wakati unapokuja. Kwenye HearHim.ChurchofJesusChrist.org, unaweza kupata video ambazo viongozi wa Kanisa wanashiriki jinsi wao wanavyotambua sauti ya Bwana. Ungeweza kutazama moja au zaidi ya video hizi pamoja na darasa na kuzungumza kuhusu video hizi zinafundisha nini kuhusu kupokea ushuhuda. Ni mafundisho gani mengine au maandiko ambayo darasa lako wanaweza kufikiria ambayo yangemsaidia mtu kutambua ufunuo binafsi? (Kwa mfano, ona 1 Wafalme 19:11–12; Wagalatia 5:22–23; Enoshi 1:1–8; Mafundisho na Maagano 6:22–24; 8:2–3; 9:7–9.)

Mathayo 16:13–19; 17:1–9

Funguo za ukuhani ni muhimu kwa ajili ya wokovu wetu.

  • Ili kuanza majadiliano kuhusu funguo za ukuhani, unaweza kuandika marejeleo kama haya juu ya ubao: Mathayo 16:19; Mafundisho na Maagano 107:18–20; 128:8–11; 132:18–19, 59; Joseph Smith—Historia ya 1:72; na “Funguo za Ukuhani” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Kisha waalike washiriki wa darasa kusoma moja au zaidi ya vifungu hivi vya maandiko na kushiriki kitu walichojifunza kutoka kwenye vifungu hivyo kuhusu funguo za ukuhani. Kwa nini tunahitaji funguo za ukuhani?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuimarisha shuhuda zao juu ya urejesho wa funguo za ukuhani katika hizi siku za mwisho, ungeweza kuwaomba nusu ya darasa kusoma Mathayo 17:1–9 na nusu nyingine kusoma Mafundisho na Maagano 110. Wanaweza kisha kushirikiana na wengine kile walichojifunza na kufahamu mifanano kati ya hadithi hizo mbili. Video “Priesthood Keys: The Restoration of Priesthood Keys” (ChurchofJesusChrist.org) ingeweza pia kuwa na msaada.

Picha
sanamu ya Petro ameshikilia funguo

Funguo za ukuhani ni mamlaka ya kuelekeza matumizi ya ukuhani.

Marko 9:14–30

Tunapotafuta imani kuu, tunaanza na imani tuliyo nayo tayari.

  • Mzee Jeffrey R. Holland alitumia hadithi ya baba akitafuta uponyaji kwa ajili ya mwanawe ili kufundisha jinsi tunavyotakiwa kumkaribia Bwana tunapohisi kwamba imani yetu haitoshi (ona “Bwana, Naamini,” Liahona, Mei 2013, 93–95). Baada ya kusoma Marko 9:14–12 kama darasa, mnaweza kujadili kwa pamoja mawazo matatu ya Mzee Holland (ona “Nyenzo za Ziada”).

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Hoja tatu za kutusaidia kupata imani zaidi.

Baada ya kusimulia tena hadithi inayopatikana katika Marko 9:14–29, Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

“Hoja nambari moja kulingana na hadithi hii ni kwamba wakati anapokabiliana na changamoto ya imani, baba anaonyesha nguvu zake kwanza na ndipo anakubali upungufu wake. Tamko lake la mwanzo ni kukubali na bila kusita: ‘Bwana, Naamini.’ Ningesema kwa wote wanaotamani imani zaidi, kumkumbuka mtu huyu! Katika nyakati za hofu au wasiwasi au wakati wa matatizo, shikilia nafasi ambayo tayari umeshinda, hata kama nafasi yenyewe ni finyu. …

“Hoja ya pili ni tofauti na ya kwanza. Wakati matatizo yanakuja na maswali yanaibuka, usianze utafutaji wako wa imani kwa kusema kiasi gani ambacho huna, kukuongoza kama ilivyo kawaida katika ‘kutoamini.’ … Sikuambii wewe ujisingizie imani usiyokuwa nayo. Mimi ninakuambia uwe mkweli kwa imani uliyo nayo. …

“Hoja ya mwisho: Wakati wasiwasi au ugumu unapokuja, usiogope kuomba msaada. Kama tunautaka kwa unyenyekevu na kwa uaminifu kama alivyofanya baba huyu, tunaweza kuupata” (“Bwana, Naamini,” Liahona, Mei 2013, 93–94).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Uliza maswali ambayo yanaalika ushuhuda. Kuuliza maswali ambayo yanahimiza wanafunzi kutoa ushuhuda wao kunaweza kuwa njia ya kufaa ya kumwalika Roho. Kwa mfano, tunapojadili Mathayo 16:13–17, unaweza kuuliza, “Mmejifunza nini kuhusu Mwokozi ambacho kimeimarisha ushuhuda wenu juu yake Yeye kama Mwokozi?” (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi32.)

Chapisha