Agano Jipya 2023
Aprili 17–23. Mathayo 18; Luka 10: “Nifanye Nini ili Kurithi Uzima wa Milele?”


“Aprili 17–23. Mathayo 18; Luka 10: Nifanye Nini Kurithi Uzima wa Milele?,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Aprili 17–23. Mathayo 18; Luka 10,” Njoo,Unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Msamaria mwema

Msamaria mwema, na Dan Burr

Aprili 17–23

Mathayo 18; Luka 10

“Nifanye Nini ili Kurithi Uzima wa Milele?”

Soma Mathayo 18 na Luka 10, na uandike misukumo yako ya kiroho. Unapopokea misukumo, unaweza kuuliza kama Mzee Richard G. Scott alivyopendekeza, “Kuna chochote zaidi ningepaswa kujua?” (“Kupata Mwongozo wa Kiroho,” Liahona, Nov. 2009, 8).

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Sura hizi zina mifano mingi ya mafundisho ya injili ambayo ni tofauti kutokana na kile ulimwengu unachotufundisha. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kuelezea baadhi ya mifano waliyoipata katika kusoma kwao wiki hii. Ni namna gani Bwana anatubariki wakati tunapoyatumia mafundisho Yake?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 18:21–35

Lazima tuwasamehe wengine kama tunataka kupokea msamaha kutoka kwa Bwana.

  • Utawezaje kutumia fumbo la mtumishi asiye na huruma kutia moyo washiriki wa darasa wawe wenye kusamehe zaidi? Labda ungeandika maswali kama yafuatayo ubaoni na uwaalike washiriki wa darasa kuyatafakari wakati mtu mmoja anasimulia tena fumbo: Mfalme anamwakilishwa Nani? Mtumishi asiye na huruma anamwakilishwa nani? Mtumishi mwenzake anamwakilishwa nani? Je, madeni yanawakilisha nini? Waalike washiriki wa darasa watafakari fumbo hili lina jumbe gani kwao binafsi. (Ona pia “Nyenzo za Ziada.”)

  • Ungeweza kuwataka washiriki wa darasa kubuni utohoaji wa fumbo la mtumishi asiye na huruma ambalo linafundisha somo lile lile kuhusu msamaha kwa kutumia hali za kisasa na maelezo ya kina. (Fikiria kuwafanya wafanye kazi hii katika vikundi.) Mjadiliane jinsi gani fumbo hili lilijibu swali la Petro kuhusu ni mara ngapi anatakiwa asamehe.

Picha
sarafu za zamani

Yesu alizungumzia fedha na deni ili kufundisha kuhusu msamaha.

Luka 10:25–37

Ili kupata uzima wa milele, lazima tumpende Mungu na majirani zetu.

  • Hapa kuna wazo ambalo linaweza kuwapa washiriki wa darasa mtazamo mpya wa fumbo la Msamaria mwema: Waalike waigize kwamba wanapeleleza kesi ya mashambulizi na unyag’anyi barabarani kati ya Yeriko na Yerusalemu. Waombe washiriki wachache wa darasa waje darasani wakiwa wamejitayarisha kuwawakilisha watu tofauti katika fumbo na kuzungumza kuhusu kuhusika kwao katika kesi. Kwa mfano, kwa nini kuhani na Mlawi hawakusimama kumsaidia mtu aliyejeruhiwa? Kwa nini Msamaria alisimama? Mawazo gani mwenye nyumba ya wageni angeweza kuongeza? Yule mtu aliyejeruhiwa alihisi vipi kuhusu kila mmoja wa wale wengine? Hakikisha majadiliano yanawavutia washiriki wa darasa kuwa kama Msamaria mwema na mwenye nyumba ya wageni na kuepuka kuwa kama kuhani na Mlawi.

  • Je, ni jinsi gani fumbo la Msamaria mwema linajibu maswali yaliyoulizwa juu ya Yesu katika Luka 10:25–29? Waalike washiriki wa darasa kuzungumzia kuhusu nyakati walipohisi kama “mtu fulani,” (mstari wa 30) aliyehitaji msaada wa haraka? Je, msaada ulikujaje? Ni kwa jinsi gani sisi kama washiriki wa kata tunafanya kazi kwa pamoja ili kuwasaidia wengine, kama Msamaria mwema na mwenye nyumba ya wageni walivyofanya?

Luka 10:38–42

Tunachagua “ile sehemu nzuri” kwa kufanya chaguzi kila siku ambazo zinaelekeza kwenye uzima wa milele.

  • Baada ya kusoma Luka 10:38–42 kama darasa, ungeweza kuwauliza washiriki wa darasa jinsi ambavyo wangeweza kujibu ushauri wa Mwokozi kama wangekuwa katika nafasi ya Martha. Jinsi gani uzoefu huu umeathiri chaguzi zao za baadaye. Je, tunawezaje kujua vitu gani katika maisha yetu wenyewe yanastahili muda na umakini zaidi? Washiriki wa darasa wangeweza kupekua ujumbe wa Rais Dallin H. Oaks “Nzuri, Bora, Bora Zaidi” (Liahona, Nov. 2007, 104–8) ili kupta ushauri ambao unaweza kuwasaidia.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Madeni katika fumbo la mtumishi asiye na huruma.

Akitoa maoni juu ya madeni yanayodaiwa katika fumbo la mtumishi asiye na huruma, Mzee Jeffrey R. Holland alisema:

“Kuna tofauti ya maoni miongoni mwa wasomi kuhusu thamani za kifedha zilizotajwa hapa—samahani kwa kutumia fedha ya Marekani—lakini kurahisisha hesabu, ikiwa thamani ndogo, isiyosameheka ni deni la senti 100, tuseme, dola100 kwa wakati huu, basi deni la talanta 10,000 ambalo lilisamehewa bure kabisa lingeweza kuwa linakaribia dola bilioni 1—au zaidi.

Kama deni la kibinafsi, hiyo ni nambari kubwa sana—kubwa kupita kuelewa kwetu. (Hakuna anayeweza kufanya manunuzi makubwa hivyo!) Basi, kwa makusudi ya fumbo hili, inadhaniwa kuwa halieleweki; inadhaniwa kuwa liko nje ya uwezo wetu wa kufahamu, kutosema chochote nje ya uwezo wetu wa kulilipa. Hii ni kwa sababu hii sio simulizi kuhusu watumwa wawili wanaozozana katika Agano Jipya. Ni simulizi kutuhusu sisi, familia ya wanadamu iliyoanguka—wadaiwa walio katika mwili wenye kufa, wavunjaji wa sheria na mahabusu wote. Kila mmoja wetu ni mdaiwa, hukumu ni kifungo gerezani kwa kila mmoja wetu. Na hapo ndipo sote tungebakia kama haingekuwa neema ya Mfalme ambaye anatuachilia huru kwa sababu anatupenda na ‘kusikia huruma kwa ajili yetu’ [Mafundisho na Maagano 121:4]” (“Basi Iweni Wakamilifu—Hatimaye,” Liahona, Nov. 2017, 41).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Fuata mfano wa Mwokozi. Unaposoma hadithi ya Mwokozi akifundisha katika Agano Jipya, tafuta masomo katika mfano Wake ambayo yataweza kukusaidia wewe kuwa mwalimu bora zaidi. Kwa mfano, katika Luka 10:25–37, Yesu alifanya nini ili kumfundisha mwanasheria kuhusu jinsi ya kupata uzima wa milele?

Chapisha