Agano Jipya 2023
Aprili 24–30. Yohana 7–10: “Mimi Ndimi Mchungaji Mwema”


“Aprili 24–30. Yohana 7–10 ‘Mimi ni Ndimi Mchungaji Mwema’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022.)

“Aprili 24–30. Yohana 7–10 “ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Yesu na mwanamke aliyeanguka chini

Hata Mimi Sikuhukumu, na Eva Koleva Timothy

Aprili 24–30

Yohana 7–10

“Mimi Ndimi Mchungaji Mwema”

Wewe na washiriki wa darasa lako mtapata umaizi mnaposoma Yohana 7–10 wiki hii. Kumbuka kwamba mawazo katika muhtasari huu yanapaswa kuongezea badala ya kubadilisha mwongozo wa kiungu unaopokea kwa kujifunza maandiko.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wakumbushe washiriki wa darasa kuhusu umuhimu wa kuzifanya nyumba zao kuwa kituo cha kujifunza injili. Waombe washiriki kile ambacho Roho Mtakatifu aliwafundisha wakati walipokuwa wakijifunza Yohana 7–10 nyumbani, binafsi au pamoja na familia zao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Yohana 7–10

Yesu Kristo ni Mwokozi wa ulimwengu.

  • Kote katika Yohana 7–10, Mwokozi alitoa matangazo kadhaa ambayo yanaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa vyema huduma yake na kusogea karibu zaidi na Yeye. Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa wasome vifungu vifuatavyo vya maandiko na kushiriki vinafundisha nini kuhusu huduma takatifu ya Mwokozi. Je, Kristo anatimizaje majukumu haya katika maisha yetu?

Picha
Yesu Kristo

Nuru ya Ulimwengu, na Howard Lyon

Yohana 7:14–17

Tunapoishi mafundisho ya Yesu Kristo, tutakuja kujua kuwa ni ya kweli.

  • Kwa namna fulani, kupata ushuhuda ni kama kujifunza ujuzi fulani—vyote vinahitaji mazoezi na uzoefu. Ili kufafanua hili, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa walio na ujuzi maalumu kama vile kupiga chombo cha muziki, kueleza jinsi walivyokuza ujuzi huo. Kwa nini haitoshi kusoma kuhusu ujuzi fulani au kumwangalia mtu akifanya hivyo? Kama darasa, jadilini jinsi juhudi zinazohusika katika kujifunza ujuzi fulani zinavyofanana na mpangilio wa kiroho Mwokozi aliouelezea katika Yohana 7:14–17. Ni kwa jinsi gani hii ni tofauti?

  • Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki matukio ambayo kwa kuishi ukweli wa injili kuliwasaidia wao kupata ushuhuda wake. Wape muda washiriki wa darasa kufikiria kanuni ya injili ambayo wangependa kupata ushuhuda wenye nguvu zaidi juu yake, na kisha wahimize kuweka malengo mahsusi ya kuishi kanuni ile kwa ukamilifu zaidi.

Yohana 8:1–11

Huruma ya Mwokozi imetolewa kwa wote wanaotubu.

  • Kwa wale wanaojiona wamelaaniwa kwa sababu ya dhambi zao, hadithi ya Mwokozi akitoa rehema na toba kwa mwanamke aliyekamatwa katika uzinzi inaweza kuwa chanzo cha kutiwa moyo. Au, kama washiriki wa darasa wanahisi kujaribiwa kulaani wengine kwa sababu ya dhambi zao, hadithi hii inaweza kutumika kama onyo. Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa wasome Yohana 8:1–11, wakitafuta majibu kwa maswali kama yafuatayo: Hadithi hii inafundisha nini kuhusu huruma ya Mwokozi? Jinsi gani kupokea huruma Yake tunapofanya dhambi kunatusaidia wakati tunahisi kujaribiwa kuwahukumu wengine? (ona Alma 29:9–10).

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kupata uhusiano binafsi katika Yohana 8:1–11, fikiria kugawa darasa katika vikundi vitatu—kimoja kulenga kwenye maneno na vitendo vya Mafarisayo, cha pili kulenga kwenye maneno na vitendo vya Mwokozi na cha tatu kulenga kwenye maneno na vitendo vya yule mwanamke. Wangeweza kufanya hivi wakati wakisoma hadithi au wakati wakitazama video ya ”Go and Sin No More” (CurhofJesusChrist.org). Alika kila kundi litengeneza orodha ya kweli za kiroho wanazojifunza kutokana na kusoma kila sehemu ya hadithi hiyo.

  • Wakati mwingine hatufahamu njia ambazo tunawahukumu wengine. Hapa kuna shughuli ya kuwasaidia washiriki wa darasa kushinda mwenendo huu: liombe darasa likusaidie kutengeneza orodha ya njia tunazowahukumu watu (kwa mwonekano wao, tabia zao, walikotoka, na mengine mengi). Wape washiriki wa darasa vipande vya karatasi vilivyokatwa katika umbo la jiwe, na waombe wachague njia ya kuwahukumu wengine ambao wanawaona wana hatia na waandike kwenye jiwe la karatasi. Tunajifunza nini kutokana na maneno ya Mwokozi kwa Mafarisayo katika Yohana 8:1–11? Alika darasa liandike upande mwingine wa karatasi zao za jiwe kitu ambacho kitawakumbusha kutohukumu (labda msemo kutoka Yohana 8).

Yohana 8:18–19, 26–29

Tunapomjua Yesu Kristo, tunamjua Baba.

  • Maneno ya Mwokozi katika Yohana 8:18–19, 26–29 yanatufundisha nini kuhusu uhusiano kati ya Yeye na Baba Yake? Baada ya kusoma na kujadiliana mistari hii, washiriki wa darasa wangeorodhesha ubaoni baadhi ya vitu ambavyo Yesu alifanya, alisema au kufundisha. Tunajifunza nini kuhusu Mungu Baba kutokana na vitu hivi?

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ishi kwa kustahili mwongozo wa Roho. Unapoishi injili, unakuwa mwenye kustahili wenzi wa Roho. Unapotafuta mwongozo Wake, Yeye atakupa mawazo na misukumo kuhusu jinsi ya kutosheleza mahitaji ya wale unaowafundisha. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi5.)

Chapisha