Agano Jipya 2023
Mei 1–7. Luka 12–17; Yohana 11: “Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea”


“Mei 1–7. Luka 12–17: Yohana 11: Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea ’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Mei 1–7. Luka 12–17; Yohana 11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
mtu akimkumbatia mwanaye

Mwana Mpotevu, na Liz Lemon Swindle

Mei 1–7

Luka 12–17; Yohana 11

“Furahini pamoja Nami; kwa kuwa Nimekwisha Kumpata Kondoo Wangu Aliyepotea”

Anza maandalizi yako kwa kujifunza kwa maombi Luka 12–17 na Yohana 11 “Kondoo gani aliyepotea” katika darasa lako anayekuja akilini mwako? Tumia Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na muhtasari huu unapotafuta mwongozo wa Bwana juu ya njia bora ya kukidhi mahitaji ya washiriki wa darasa hata kama hawahudhurii darasa.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kutenda ni sehemu muhimu ya kijifunza, kwa hiyo waalike washiriki wa darasa kushiriki jinsi wanavyochagua kuishi jambo fulani walilojifunza kutoka katika maandiko wiki hii.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Luka 14:15–24

Hakuna sababu inayotosha kwa kuikataa injili.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza fumbo la karamu kuu, unaweza kuwaalika kwenye sherehe ya kubuni ambayo wewe utakuwa mwenyeji. Waruhusu washiriki baadhi ya sababu kwa nini watahudhuria au hawatahudhuria. Someni Luka 14:15–24 pamoja, na mjadili visingizio walivyovitoa watu katika fumbo walipoalikwa kwenye karamu ambayo iliwakilisha baraka za injili. Visingizio gani watu wanavitoa leo kwa kushindwa kukubali mialiko ya Mwokozi ya kupokea baraka za Baba wa Mbinguni? Labda washiriki wa darasa wanaweza kushiriki baraka walizozipokea wakati walipofanya dhabihu muhimu ili kuishi kanuni fulani za injili.

Luka 15

Tunaweza kuwatafuta wale waliopotea na kufurahi pamoja na Baba wanaporudi.

  • Ni kwa jinsi gani utawapatia washiriki wa darasa fursa ya kitu walichojifunza kuhusu mafumbo haya matatu katika Luke 15? Fikiria kumpatia kila mshiriki wa darasa moja ya mafumbo hayo ili arejelee. Wangeweza kutafuta na kushiriki majibu ya maswali kama haya: Ni maneno gani katika fumbo yanafunua jinsi Baba wa Mbinguni anavyojisikia kuhusu wale wanaopotea? Mafumbo yanapendekeza nini kuhusu jinsi gani tunapaswa kujaribu kuwafikia watoto wote wa Mungu? Washiriki wa darasa wangeshiriki jinsi ambavyo Mwokozi amewapata wakati walipokuwa wanahisi wamepotea.

  • Kuimba “Dear to the Heart of the Shepherd” (Nyimbo za Kanisa, na. 221) pamoja inaweza kuwa nyongeza ya maana kwenye mafundisho ya mafumbo haya.

  • Mnaporejelea fumbo la mwana mpotevu kwa pamoja, washiriki wa darasa wanaweza kunufaika kutokana na kufokasi kwenye maneno, matendo na imani ya kila mtu katika fumbo. Tunajifunza nini kutoka kwa kila mtu? Labda washiriki wa darasa wanaweza kuandika hatima nyingine kwa fumbo ambapo msimamo wa kaka mkubwa kwa ndugu yake ni tofauti. Namna gani ushauri wa baba katika fumbo unatufundisha sisi kuhusu jinsi tunavyopaswa kuhisi kuhusu wale waliopotea na wale wanaorudi kwenye injili? (Ona pia maelezo ya Mzee Jeffrey R. Holland katika “Nyenzo za Ziada.”) Au unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kufikiria kama wao ni baba katika fumbo hili. Ushauri gani wa ziada watakaompa mwana mkubwa ili kumsaidia kufurahia maendeleo au mafanikio ya wengine?

Luka 11:11–19

Shukrani kwa ajili ya baraka zangu kutanisogeza karibu na Mungu.

  • Waalike washiriki wa darasa kuelezea kitu walichojifunza kuhusu shukrani kutoka katika kujifunza kwao Luka 17:11–19 na video ya “Rais Russell M. Nelson juu ya Nguvu ya Uponyaji ya Shukrani” (ChurchofJesusChrist.org). Ni kwa namna gani mkoma mwenye shukrani alibarikiwa kwa ajili ya kuelezea shukrani zake? Je, ni kwa jinsi gani tunabarikiwa tunapotoa shukrani? Washiriki wa darasa wangeweza kupendekeza njia tunazoweza kuonyesha shukrani zetu kwa Mungu na watu wengine.

Yohana 11:1–46

Yesu Kristo ni Ufufuo na Uzima.

  • Njia moja ya kuchanganua Yohana 11:1–46 ni kuwaomba washiriki wa darasa kupeana zamu kusoma mistari na uwaalike kuacha na kujadili kila mara pale wanapopata ushahidi wa imani katika Yesu kristo. Ungeweza pia kuwaomba washiriki wa darasa kuzingatia uhusiano wa watu waliohusika—kama vile Mwokozi, Mitume, Martha, Mariamu na Lazaro. Twaweza kujifunza nini kutoka kwa kila mmoja wao? Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu wakati imani yao katika Yesu Kristo ilipoimarishwa wakati wa jaribu.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kujifunza kutoka kwa mwana mpotevu mwingine.

Mzee Jeffrey R. Holand alitoa wazo hili kuhusu kaka mkubwa wa mwana mpotevu: “Huyu kijana hakukasirika sana kwamba mwenzake amerudi nyumbani kama alivyokasirika kwamba wazazi wake wanafurahia hilo. … Yeye bado hajawa na huruma na rehema, upana wa fadhila wa ono la kuona kwamba huyu sio mpinzani anayerudi. Ni ndugu yake. Kama baba yake alivyomsihi aone, ni yule aliyekufa na sasa yu hai. Ni yule aliyepotea na sasa amepatikana” (“Mwana Mpotevu Mwingine,” Ensign, Mei 2002, 63).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kumfikia yule mmoja. Kama vile mchungaji katika fumbo la Mwokozi (ona Luka 15:4), “wewe unaweza kuwafikia wale ambao wanakosekana darasani mwako. Fursa zako kuwafundisha na kuwainua washiriki wa darasa na kuwasaidia kuja kwa Kristo zinaendelea hata nje ya darasa na zaidi ya wale wanaohudhuria masomo yako rasmi” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi8).

Chapisha