“Mei 22–28. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24– 25; Marko 12–13; Luka 21: ‘Mwana wa Mtu Atakuja,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)
“Mei 22–28. Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24– 25; Marko 12–13; Luka 21,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Mei 22–28
Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24 –25; Marko 12–13; Luka 21
“Mwana wa Mtu Atakuja”
Kumbuka kuanza matayarisho yako ya kufundisha kwa kusoma kwa maombi Joseph Smith—Mathayo 1; Mathayo 24 –25; Marko 12–13; na Luka 21. Tafuta mwongozo wa kiungu wewe mwenyewe, na kisha urejelee muhtasari huu kwa mawazo ya ziada.
Alika Kushiriki
Tengeneza orodha ubaoni ya mafumbo ya Mwokozi yaliyopatikana katika masomo ya wiki hii, kama vile mti wa mtini, mtu mwema na mwizi, watumishi waaminifu na waovu, wanawali kumi, talanta na kondoo na mbuzi. Waombe washiriki wa darasa kushiriki kweli walizojifunza kutokana na mafumbo haya ambayo yanaweza kuwasaidia kujitayarisha kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Bwana. Wanafanya nini kutumia ukweli huu katika maisha yao?
Fundisha Mafundisho
Unabii kuhusu Ujio wa Pili wa Mwokozi unaweza kutusaidia kuukabili wakati ujao kwa imani.
-
Ishara za Ujio wa Pili zinaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya washiriki wa darasa kuzielewa. Inaweza kuwasaidia kufanya kazi katika makundi na kuzitambua ishara wanazozipata katika Joseph Smith—Mathayo 1:21–37. Inaweza pia kuwasaidia kuelewa vyema umuhimu wa ishara hizi kama watazifananisha na alama za barabarani. Kwa nini alama za barabarani ni muhimu? Je, ni kwa jinsi gani ishara za Ujio wa Pili ni kama alama za barabarani? Je, ni kwa jinsi gani ni tofauti? Unaweza hata ukawapa kila kikundi vipande vya karatasi vyenye umbo la ishara za barabarani na kuwaalika waandike kila karatasi ishara ambayo itatangulia Ujio wa Pili. Waache washiriki kile walichopata, na alika darasa lijadili ushahidi wa ishara hizi ulimwenguni leo.
Joseph Smith—Mathayo 1:26–27, 38–55; Mathayo 25:1–13
Ni lazima daima tuwe tayari kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi.
-
Mafumbo katika Joseph Smith—Mathayo 1:26–27, 38–55 na Mathayo 25:1–13 yanaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kutambua umuhimu wa kujitayarisha kwa ajili ya Ujio wa Pili. Waalike washiriki wa darasa kupekua mistari hii na kushiriki kile wanachohisi Mwokozi anatualika sisi tufanye. Mzee David A. Bednar alitoa tafsiri moja ya fumbo la wale wanawali kumi ambalo lingeweza kusaidia (ona “Nyenzo za Ziada”). Kwa nini lazima kila mmoja wetu apitie uongofu kwa ajili yetu wenyewe? Je, ni kwa jinsi gani tutafanya hili? Je, Mafundisho na Maagano 45:56–57) inaongeza nini kwenye uelewa wetu juu ya fumbo hili?
-
Unapojifunza kuhusu kurudi kwa Mwokozi, unaweza kusoma au kuimba pamoja nyimbo za Kanisa kuhusu Ujio wa Pili (ona “Jesus Christ—Second Coming” katika kiambatisho cha mada nyuma ya kitabu cha nyimbo za Kanisa).
Kwenye Hukumu ya Mwisho, tutampa Bwana maelezo juu ya maisha yetu.
-
Fumbo la talanta na fumbo la kondoo na mbuzi yanaweza kutushawishi kufikiri kuhusu hadithi za maisha yetu tutakayotoa kwa Bwana kwenye Hukumu ya Mwisho. Mnaweza kuyasoma mafumbo pamoja na kumtaka kila mshiriki wa darasa ashiriki swali moja Mwokozi analoweza kuuliza wakati tutakapotoa maelezo ya maisha yetu. Toa muda kwa washiriki wa darasa kupanga njia watakazofanya kwa misukumo waliyopokea wakati wa majadiliano.
-
Ili kushawishi majadiliano kuhusu Mathayo 25:34–40, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki mifano ya watu walioonyesha huruma iliyoelezwa katika aya hizi. Wape muda kutafakari nani anaweza kuhitaji huduma yao. Ni zipi baadhi ya njia tunazoweza kuwalisha wenye njaa, kuwavika walio uchi, na kuwatembelea wagonjwa?
Nyenzo za Ziada
Mafuta ya uongofu.
Mzee David A. Bednar alitoa ushauri wa uwezekano wa ufafanuzi wa fumbo hili la wale wanawali kumi:
“Fikiria mafuta kuwa mafuta ya uongofu [ona Mathayo 25:4–9]. …
“Je, wale wanawali watano wenye busara walikuwa wachoyo na wasio tayari kugawana, au walikuwa wanaonyesha kwa usahihi kwamba mafuta ya uongofu hayawezi kuazimwa? Je, nguvu ya kiroho inayotokana na utiifu endelevu kwa amri inaweza kutolewa kwa mtu mwingine? Je, maarifa yaliyopatikana kupitia kujifunza kwa bidii na kutafakari maandiko yanaweza kupelekwa kwa mtu mwingine mwenye shida? Je, amani ambayo injili inaleta kwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho mwaminifu inaweza kuhamishiwa kwa mtu anayepata shida au changamoto kubwa? Jibu la wazi kwa kila moja ya maswali haya ni hapana.
“Kama walivyosisitiza vizuri wanawali wale wenye busara, kila mmoja wetu lazima ‘ajinunulie mwenyewe.’ Wanawake hawa wenye mwongozo wa kiungu hawakuwa wakielezea mapatano ya kibiashara, bali, walikuwa wanasisitiza wajibu wetu binafsi kuweka taa yetu ya ushuhuda ikiwaka na kupata akiba ya kutosha ya mafuta ya wongofu. Mafuta haya ya thamani yanapatikana tone moja baada ya jingine—‘mstari juu ya mstari [na] kanuni juu ya kanuni’ (2 Nefi 28:30), kwa subira na kwa kusonga bila kuchoka” (“Kuongolewa kwa Bwana,” Liahona, Nov. 2012,109).