Agano Jipya 2023
Mei 8–14. Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18: “Nimepungukiwa na Nini Tena?”


“Mei 8–14. Mathayo 19–20: Marko 10: Luka 18: ‘Wewe ndiwe Kristo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili; Agano Jipya 2023 (2022)

“Mei 8–14. Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili 2023

Vibarua katika shamba la mizabibu

Mei 8–14

Mathayo 19–20; Marko 10; Luka 18

“Nimepungukiwa na Nini Tena?”

Unapojiandaa kufundisha, kwa sala zingatia jinsi unavyoweza kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki walichojifunza au walivyohisi wakati wa kujifunza kwao wenyewe?

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Inaweza kuwa msaada mara chache kujadili uzoefu wa ujumla wa washiriki kwa kutumia mafunzo ya injili yanayolenga nyumbani. Ni uzoefu gani wa mafanikio wanaoweza kushiriki? Ni vikwazo au changamoto gani wanazokabiliana nazo? Ni ushauri gani wanaweza kupeana?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 19:3–9

Ndoa kati ya mwanamume na mwanamke ni muhimu kwa mpango wa milele wa Mungu.

Mathayo 20:1–16

Kila mmoja anaweza kupokea baraka ya uzima wa milele, bila kujali lini wamepokea injili.

  • Nini kingewasaidia washiriki wa darasa lako kutumia kanuni katika fumbo la wafanyakazi katika shamba la mizabibu? Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa wachache kujiandaa kuigiza fumbo kwa maonyesho darasani. Baada ya wasilisho, watu walioigiza kama wafanyakazi wangeweza kushiriki jinsi walivyohisi kuhusu malipo waliyopokea na kwa nini. Je, fumbo hili linapendekeza nini kuhusu ufalme wa mbinguni? Ni utambuzi gani wa ziada washiriki wa darasa wanapata kuhusu fumbo hili kutokana na ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland “Wafayakazi katika Shamba la Mizabibu”? (Liahona, Mei 2012, 31–33).

Mathayo 19:16–22; Marko 10:17–27

Mwokozi atatuongoza kuja karibu zaidi na Yeye tunapoomba msaada Wake.

  • Je, unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa lako kutambua na kutumia kanuni katika hadithi ya kijana tajiri? Njia mojawapo inaweza kuwa ni kuwaomba wasome Marko 10:17–27 na kufikiria kama kuna wakati wowote wamewahi kujisikia kama kijana tajiri. Ni nini kilichotusaidia sisi kufuata ushauri wa Mwokozi hata wakati kufanya hivyo ilikuwa vigumu? Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki uzoefu ambapo humo wao walijiuliza “Nimepungukiwa nini tena?” (Mathayo 19:20) na walipokea ushawishi binafsi wa kubadilika. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa ambao huenda wakakatishwa tamaa kwa kufokasi kitu wanachopungukiwa, ungeweza kushiriki maelezo katika “Nyenzo za Ziada.”

  • Washiriki wa darasa wanaweza kuwa wamesoma ujumbe wa mkutano kuhusiana na mistari hii kama inavyopendekezwa katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia . Waalike kushiriki utambuzi waliopata.

Mtu mnyenyekevu na Mfarisayo

Mtoza Ushuru Mwenye Toba na Mfarisayo wa Kujifanya Mwenye Haki Hekaluni, na Frank Adams

Luka 18:9–14

Tunapaswa kutumaini katika rehema za Mungu, sio kwa haki zetu wenyewe.

  • Fumbo la Mwokozi la kufananisha sala ya Mfarisayo na ya mtoza ushuru linaweza kukusaidia kusisitiza mtazamo ambao Bwana anawaomba wale wanaotafuta kumfuata Yeye. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutumia fumbo hili kwa siku yetu, unaweza kuwaomba waandike upya sala ya Mfarisayo katika hali ya kisasa lakini iwe inaeleza wazi msimamo ule ule. Wangeweza kufanya hivyo hivyo kwa sala ya mtoza ushuru na kisha uwaombe washiriki kile walichoandika. Jinsi gani mistari ya 15–17 na 18–24 inahusiana na kitu ambacho Mwokozi alifundisha katika fumbo hili? Ungeweza pia kushiriki maelezo yafuatayo kuhusu mistari hii yaliyotolewa na Mzee Dale G. Renlund: “Ujumbe kwa ajili yetu ni wazi: mwenye dhambi anayetubu hujongea karibu zaidi na Mungu kuliko afanyavyo mtu ajionaye mwenye haki ambaye anamlaani yule mwenye dhambi” (“Mchungaji Wetu Mwema,” Liahona, Mei 2017, 31).

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Acha tusiridhike au kukata tamaa.

Mzee D. Todd Christofferson alifundisha:

Kama tutauliza kwa dhati, ‘Ninapungukiwa nini tena?’ [Mungu] hatatuacha tubashiri, bali kwa upendo Yeye atatujibu kwa ajili ya furaha yetu. Naye atatupatia matumaini.

“Ni kazi inayohitaji muda, na ingetisha na kuogofya kama katika mapambano yetu kwa ajili ya utukufu tungekuwa peke yetu. Ukweli mtukufu ni kwamba hatupo peke yetu. Tunao upendo wa Mungu, neema ya Kristo, faraja na mwongozo wa Roho Mtakatifu, na urafiki wa Watakatifu wenzetu katika mwili wa Kristo. Na tusiwe tumetosheka na pale tulipo, lakini wala tusikatishwe tamaa”. (“Mkate wa Uzima Ulioshuka Chini kutoka Mbinguni,” Liahona, Nov. 2017, 39).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Mungu anahitaji vipaji vyako vya kipekee na uwezo wako. “Unaweza kuwabariki watoto wa Mungu kupitia upendo ulio nao kwa wengine, na karama ambazo Mungu amekupatia, na uzoefu wako wa maisha. Unapohudumu kwa uaminifu na kutafuta msaada wa Mungu, Yeye atakuinua, na utaongezeka katika uwezo wako wa kufundisha injili katika njia ya Mwokozi” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi5).