Agano Jipya 2023
Mei 15–21. Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12: “Tazama, Mfalme Wako Anakuja”


“Mei 15–21. Mathayo 21–23: Marko 11: Luka 19–20; Yohana 12: ‘Tazama, Mfalme Wako Anakuja” Njoo, unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Mei 15–21. Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
mtu juu ya mti wakati Yesu akikaribia

Zakayo juu ya Mti wa Mkuyu, na James Tissot

Mei 15–21

Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; Yohana 12

“Tazama, Mfalme Wako Anakuja”

Unaposoma Mathayo 21–23; Marko 11; Luka 19–20; na Yohana 12, angalia kanuni ambazo zitasaidia kukidhi mahitaji ya watu unaowafundisha. Roho Mtakatifu atakupa mwongozo kujua jinsi ya kuwasaidia washiriki wa darasa kuzigundua kanuni hizo.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Siku saba kabla ya darasa, waalike washiriki wachache wa darasa waje wakiwa wamejiandaa kushiriki tukio walilokuwa nalo wakati wakijifunza wiki hii sura walizopangiwa. Waombe kueleza kuhusu baraka ambazo huja kwao wanapojifunza maandiko wakati wa siku za wiki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Luka 19:1–10

Mwokozi anatujua sisi kibinafsi.

  • Washiriki wako wa darasa yawezekana wamewahi kuhisi kutotiwa maanani au kusahaulika wakati mwingine katika maisha yao. Hadithi ya Zakayo inaweza kuwasaidia kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanawajua na kuwajali. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kufananisha hadithi hii na maisha yao, waalike kujifikiria wao wenyewe kama Zakayo. Unafikiri alijifunza nini kuhusu Mwokozi kutokana na uzoefi wake? Tunaweza kujifunza nini kutokana na juhudi za Zakayo kuhusu kumtafuta Mwokozi?

Mathayo 21:1–11; Marko11:1–11; Luka 19:29–44; Yohana12:12–16

Yesu Kristo ni Mfalme wetu.

  • Shughuli rahisi inaweza kuanzisha majadiliano kuhusu Mwokozi kuingia kwa shangwe ya ushindi ndani ya Yerusalemu: Washiriki kadhaa wa darasa wanaweza kuchora ubaoni vitu vinavyohusiana na mfalme, kama vile taji, au kiti cha enzi, wakati wengine wakibashiri nini wanachokichora. Kisha washiriki wengine wa darasa wanaweza kuchora mwanapunda na matawi ya miti. Vitu hivi vinahusika vipi na mfalme? Unaweza kisha kuonyesha picha ya kuingia kwa Mwokozi kwa shangwe ya ushindi Yerusalemu kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia na waalike washiriki wa darasa kusoma Marko 11:1–11. Je, ni kwa jinsi gani watu hawa walimtambua Yesu kama Mfalme wao? Je, ni kwa jinsi gani tunamwabudu Yesu Kristo kama Mfalme wetu kupitia maneno na matendo yetu?

Mathayo 23:34–40

Amri mbili kuu ni kumpenda Mungu na kuwapenda wengine kama tunavyojipenda wenyewe.

  • Unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kwamba “kwenye hizi amri mbili”—kumpenda Mungu na kuwapenda majirani zetu—“hutegemea torati yote na manabii”? Mathayo 10:40 Baada ya kusoma Mathayo 22:34–40 kwa pamoja, ungeweza kuandika Mpende Mungu na Mpende jirani yako juu ya ubao. Mpe kila mwanafunzi kipande cha karatasi kilichoandikwa amri juu yake. Waalike wachache wao kusoma amri zao na kuzungumzia kuhusu jinsi amri zao zilivyowasaidia kutii amri moja au zote ya hizi amri kuu mbili. Baada ya kujadili amri zao, wanaweza kuziweka karatasi zao juu ya ubao. Kwa nini ni muhimu kukumbuka kwamba amri zote zinahusiana na amri hizi kuu mbili? (ona “Nyenzo za Ziada”).

Mathayo 23:13–33

Tutalindwa tunapoepuka kuwafuata viongozi vipofu.

  • Washiriki wa darasa wanaweza kufaidika kwa kujadili istilahi “viongozi vipofu” ambayo Mwokozi alilitumia kuelezea Mafarisayo na waandishi waliokuwa vipofu kiroho? Mathayo 23:16. Ungeweza kufikiria njia ya kuonyesha ingekuwa namna gani kwa mtu kumfuata mtu asiyeweza kuona. Au darasa lingeorodhesha ubaoni tabia za mwongozaji kipofu, kama ilivyoelezwa katika Mathayo 23:13–33. Kuongeza kwenye orodha, zingatia kutafuta maandiko ya ziada ambayo yanafundisha kuhusu upofu wa kiroho, kama vile 2 Wakorintho 4:3–4; 2 Nefi 9:28–32; na Yakobo 4:14. Ni kwa jinsi gani tunaweza kutambua na kuepukana na waongozaji vipofu?

Picha
Yesu akizungumza kwa Mafarisayo

Mwokozi anawatangaza Mafarisayo kama wanafiki na waongozaji vipofu.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kumpenda Mungu na kuwapenda majirani zetu ni msingi wa yote tunayofanya.

Akielezea amri kuu hizi mbili zinazopatikana katika Mathayo 22:37–39, Rais M. Russell Ballard alifundisha:

“Utiifu kwa amri hizo mbili unaleta njia ya kupata amani na furaha zaidi. Tunapompenda na kumtumikia Bwana na kuwapenda na kuwatumikia majirani zetu, kwa uhalisia tutahisi furaha zaidi ambayo huja kwetu kwa njia bora zaidi.

“Kumpenda Mungu na kuwapenda majirani zetu ni msingi wa kimafundisho wa kuhudumu; kujifunza nyumbani kunakosaidiwa na Kanisa; kuabudu kiroho siku ya Sabato; na kazi ya wokovu kwa pande zote mbili za pazia inayopata msaada katika Muungano wa Usaidizi na akidi za wazee. Mambo yote haya yamejikita juu ya amri takatifu ya kumpenda Mungu na kuwapenda jirani zetu. Je, kunaweza kuwa na kitu muhimu zaidi, cha msingi zaidi, na rahisi zaidi kuliko hicho?” (“Injili ya Yesu Kristo iliyo ya Kweli, Safi, na Rahisi,” Liahona, Mei 2019, 29).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Hauhitaji kumaliza kila kitu. “Kuna mengi ya kujadili katika kila somo, lakini sio lazima kumaliza kila kitu katika kipindi kimoja cha darasa ili kugusa moyo wa mtu—mara nyingi kipengele kimoja au viwili vikuu huwa vinatosha. Unapotafakari mahitaji ya wanafunzi, Roho atakusaidia kutambua kanuni, hadithi, au maandiko yapi ambayo hususani yana maana zaidi kwao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi7).

Chapisha