Agano Jipya 2023
Mei 29–Juni 4. Mathayo 26; Marko 14; Yohana 13: “Kwa Ukumbusho”


“Mei 27–Juni 4. Mathayo 26; Marko 14; Luka 23; Yohana 13: ‘Kwa Ukumbusho,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Mei 27–Juni 4. Mathayo 26; Marko 14; Luka 13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Chakula cha Mwisho

Kwa Ukumbusho Wangu, na Walter Rane

Mei 27–Juni 4.

Mathayo 26; Marko 14; Yohana 13

“Kwa Ukumbusho”

Soma Mathayo 26; Marko 14; na Yohana 13, na utafakari mawazo na misukumo ambayo inakuja akilini mwako. Ni jumbe gani zingebariki washiriki wa darasa lako?

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike washiriki wa darasa washiriki kitu walichojifunza wiki hii ambacho kiliwasaidia kupata maana zaidi katika sakramenti. Walifanya nini na kwa jinsi gani iliathiri uzoefu wao wa kushiriki sakramenti?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 26:20–22

Lazima tuyachunguze maisha yetu wenyewe ili kuamua jinsi maneno ya Bwana yanavyotumika kwetu.

  • Tunasikia hadithi nyingi za injili katika maisha yetu, lakini wakati mwingine inashawishi kusadiki kwamba masomo hayo yanatumika sana kwa watu wengine. Majadiliano kuhusu Mathayo 26:20–22 yanatusaidia kushinda mwenendo huu. Ni masomo gani tunaweza kujifunza kutokana na jinsi wafuasi walivyotumia maneno ya Mwokozi kwao wenyewe? Kama mshiriki yeyote wa darasa atasoma ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf wenye kurejelea hadithi hii “Bwana, Ni Mimi?,” wangeweza kushiriki utambuzi walioupata (Liahona, Nov. 2014, 56–59).

Mathayo 26:26–29

Sakramenti ni fursa ya kumkumbuka Mwokozi.

  • Je, ni kwa jinsi gani washiriki wa darasa wangeeleza juu ya utakatifu wa ibada ya sakramenti kwa mtu ambaye haielewi vizuri? Pengine mngeweza kutengeneza pamoja orodha ya maswali ambayo mtu anaweza kuwa nayo kuhusu sakramenti, kama vile “Kwa nini Mwokozi alitupatia sakramenti? Kwa nini mkate na maji ni alama muhimu za Yesu Kristo? Je, ni ahadi gani tunazotoa wakati tunapokula sakramenti? Je, na sisi tunapokea ahadi gani? Washiriki wa darasa wangeweza kutafuta majibu katika vifungu vifuatavyo: Alma 26:26–29; Mafundisho na Maagano 20:75–79; na Mada za Injili, “Sakramenti” (Topics.ChurchofJesusChrist.org). Ungeweza pia kushiriki utambuzi kutoka kwa Mzee D Todd Christofferson katika “Nyenzo za Ziada.”

    Picha
    mwanamke akila sakramenti

    Sakramenti inatusaidia kumkumbuka Yesu Kristo.

  • Washiriki wa darasa wanaweza kunufaika kutokana na kusikia mawazo ya kila mmoja wao kuhusu jinsi ya kumkumbuka Mwokozi wakati wa sakramenti na katika wiki yote (ona Luka 22:19–20; Mafundisho na Maagano 6:36–37). Pengine ungewaalika kushiriki kile kinachowasaidia wao na familia zao kumkumbuka Mwokozi na kuyashika maagano yao. Wangeweza pia kushiriki kile wanachofanya ili kufanya sakramenti kuwa tukio takatifu.

Yohana 13:1–17

Mwokozi ni mfano wetu wa kuhudumia wengine kwa unyenyekevu.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kutafakari umuhimu wa Yesu akiwaosha miguu wanafunzi wake, unaweza kumwita mshiriki wa darasa mbele kuigiza nafasi ya Petro katika maelezo haya na kuhojiwa na washiriki wa darasa wengine. Washiriki wa darasa wangeweza kupekua Yohana 13:1–17 na wafikirie maswali ambayo wangemwuliza Petro kuhusu uzoefu wake. Tunajifunza nini kutokana na hadithi hii ambayo inaweza ikaathiri jinsi tunavyowahudumia wengine?

Yohana 13:34–35

Upendo wetu kwa wengine ni ishara kwamba tu wafuasi wa Yesu Kristo.

  • Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuwashawishi washiriki wa darasa kuwa wenye kupenda zaidi? Pengine unaweza kuwauliza jinsi wanavyoweza kujua kwamba mtu fulani waliyekutana naye ni mfuasi wa Kristo. Unaweza kuwaalika wapekue Yohana 13:34–35 ili kujifunza jinsi wafuasi wa kweli wa Kristo wanavyoweza kutambuliwa. Tunaweza kufanya nini kuufanya upendo kuwa tabia ya utambulisho wa ufuasi wetu? Pengine ungeweza kujadili jinsi gani kuwapenda wengine ni njia ya kushuhudia juu ya Yesu Kristo. Tunawezaje kufanya hili katika familia zetu, mitandao ya kijamii na katika sehemu nyingine?

  • Kama darasa, mmejifunza mengi kuhusu maisha ya Mwokozi mwaka huu, ikijumuisha mifano mingi ya jinsi Alivyoonyesha upendo Wake kwa wengine. Njia mojawapo ya kuwasidia washiriki wa darasa kutafakari amri katika Yohana 13:34 inaweza kuwa kuandika Kama nilivyowapenda ubaoni na kuwataka washiriki wa darasa kuorodhesha mifano wanayokumbuka kutoka Agano Jipya ambayo inaonyesha upendo wa Yesu. Kisha ungeweza kuandika Mpendane ubaoni na waulize washiriki wa darasa kuorodhesha njia tunayoweza kufuata mfano Wake wa upendo. Washiriki wa darasa yawezekana wakapata mawazo katika moja ya video hizi katika “Nyenzo za Ziada.”

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

“Zifanye sifa na tabia za Kristo kuwa zako.”

Mzee D . Todd Christofferson alifundisha, ki-istiari kula mwili [wa Mwokozi] na kunywa damu Yake ina [maana] kuzifanya sifa na tabia za Kristo kuwa zetu, kuvua uanadamu wa asili na kuwa Watakatifu “kupitia upatanisho wa Kristo Bwana’[Mosia 3:19]. Tunapopokea mkate na maji ya sakramenti kila wiki, tutafanya vyema kutafakari ni kwa jinsi gani kwa ujumla na kwa ukamilifu tujumuishe tabia Yake na mpangilio wa maisha Yake yasiyo na dhambi ndani ya maisha yetu na utu wetu.“ (Mkate wa Uzima, Ulioshuka kutoka Mbinguni,” Liahona, Nov. 2017, 37).

Video kuhusu upendo (kwenye ChurchofJesusChrist.org.

  • “Mpendane”

  • “Dhabihu ya Familia, Toa na Upendo”

  • “Matayarisho ya Thomas S. Monson: Alijifunza Huruma katika Ujana Wake”

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tazama kupitia macho ya Mungu. Jitahidi kuwaona washiriki wa darasa lako kama Mungu anavyowaona, na Roho atakuonyesha thamani yao tukufu na uwezekano wao wa kuwa. Utakapofanya hivi, utaongozwa katika juhudi zako za kuwasaidia wao (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi6).

Chapisha