“Juni 19–25. Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19: ‘Imekwisha’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)
“Juni 19–25. Mathayo 27; Marko 15: Luka23; Yohana 19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Juni 19–25
Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19
“Imekwisha”
Anza matayarisho yako ya kufundisha kwa kusoma kwa maombi Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; na Yohana 19. Tafuta kuishi ukiwa mwenye kumstahili Roho ili uweze kutoa ushahidi wenye nguvu juu ya Mwokozi na Upatanisho Wake.
Alika Kushiriki
Alika kila mshiriki wa darasa kuchagua sura kutoka masomo ya wiki hii na kutumia dakika chache kuikagua, akitafuta neno, kirai au maelezo ya kina yenye kuwafundisha kitu chenye maana kuhusu Mwokozi na misheni Yake. Wape nafasi za kushiriki kile walichopata na kuelezea kwa nini kina maana kwao.
Fundisha Mafundisho
Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; Yohana 19
Utayari wa Yesu Kristo kuteseka unaonyesha upendo Wake kwa Baba Yake na kwetu sisi sote.
-
Ili kusaidia darasa kuelewa jinsi gani mateso na kifo cha Mwokozi juu ya msalaba vilionyesha upendo Wake, jaribu shughuli kama hii: Mpe kila mshiriki wa darasa moyo wa karatasi, na waalike kuandika juu ya mioyo yao kirai kutoka 1 Wakorintho 13:4–7 ambacho kinaelezea kuhusu hisani. Kisha waombe wapekue Mathayo 27; Marko 15; Luka 23; au Yohana 19 na waandike juu ya upande mwingine wa mioyo yao mistari michache ambayo inaonyesha jinsi Mwokozi alivyoonyesha upendo ulioelezwa katika kirai walichochagua. Waache washiriki kile walichokipata. Ni matukio gani yametusaidia sisi kuelewa upendo wa Mwokozi?
-
Sanaa inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kupata taswira ya baadhi ya matukio wanayoyasoma wiki hii. Pengine ungeligawa darasa katika vikundi na kutoa picha kwa kila kikundi (ona “Nyenzo za Ziada” kwa picha zilizopendekezwa). Vikundi vinaweza kusoma mistari ambayo inaelezea matukio yaliyoonyeshwa katika picha zao. Baadaye wanaweza kushiriki mawazo yao na hisia kuhusu matukio haya—ikijumuisha jinsi picha inavyowasaidia wao kuelewa vyema Upatanisho wa Mwokozi. Unaweza pia kufikiria kuonyesha video “Jesus Is Condemned before Pilate” na “Jesus Is Scourged and Crucified” (ChurchofJesusChrist.org). Wahimize washiriki wa darasa kutoa shuhuda zao juu ya Mwokozi na Upatanisho Wake.
Manabii wa zamani waliona mapema mateso na Kusulubiwa kwa Mwokozi.
-
Manabii wa kale walitabiri mengi miongoni mwa matukio katika saa ya mwisho ya Mwokozi. Njia moja ya kuwasaidia washiriki wa darasa kuliona hili ni kumpa kila mtu andiko moja au zaidi yaliyo katika “Nyenzo za Ziada” na waombe watafute mistari katika Mathayo 27 ambayo inaonyesha jinsi maandiko yalivyotimizwa. Unaweza kutengeneza chati ambayo inalinganisha unabii na kutimia kwake. Jinsi gani unabii huu unaimarisha imani yetu katika Yesu Kristo?
Mathayo 27:27–49; Marko 15:16–32; Luka 23:11, 35–39; Yohana 19:1–5
Upinzani hauwezi kusitisha kazi ya Mungu.
-
Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kwa uaminifu kukabiliana na upinzani wanapokuwa wakweli kwenye imani yao, ungeweza kuwaalika kusoma mistari inayoelezea mateso ambayo Mwokozi alikabiliana nayo (ona Mathayo 27:27–49; Marko 15:16–32; Luka 23:11, 35–39; Yohana 19:1–5). Tunajifunza nini kutokana na majibu ya Mwokozi ambayo yanaweza kutusaidia kukabiliana na upinzani? Ni mifano gani mingine ya kukabiliana na upinzani inayoweza kutusaidia sisi? (Ona, kwa mfano, Joseph Smith—Historia 1:24–25.)
Mwokozi anatupa matumaini na msamaha.
-
Hata katika dakika yake ya mwisho, Mwokozi aliendelea kutoa matumaini na msamaha. Fikiria jinsi unavyoweza kuwashawishi washiriki wa darasa kufuata mfano Wake. Kwa mfano, ungeweza kuomba nusu ya darasa kusoma Luka 23:34–38 (ikijumuisha mstari wa 34, tanbihic , ambayo inatoa umaizi kutoka kwenye Tafsiri ya Joseph Smith) na nusu nyingine isome Luka 23:39–43. Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kitu wanachojifunza kuhusu Mwokozi kutoka katika mistari yao waliyopangiwa. Je, tunawezaje kufuata mfano wa Mwokozi?
Nyenzo za Ziada
Picha za mateso, maumivu na kufa kwa Yesu.
-
Pilate Washes His Hands (ChurchofJesusChrist.org; Mathayo 27:11–25)
-
Christ with a Crown of Thorns (ChurchofJesusChrist.org; Mathayo 27:26–31)
-
Jesus Carries His Cross (ChurchofJesusChrist.org; Yohana 19:13–18)
-
The Crucifixion (ChurchofJesusChrist.org na Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 57; Luka 23:33–46; Yohana 19:23–37)
-
Burial of Jesus (ChrchofJesusChrist.org na Kitabu cha Sanaa ya Injili, na 58; Yohana 19:38–42)