Agano Jipya 2023
Juni 5–11. Yohana 14–17: “Kaeni katika Pendo Langu”


“Juni 5–11. Yohana 14–17: ‘Kaeni Katika Pendo Langu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Juni 5–11. Yohana 14–17 “ Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Chakula cha Mwisho

Chakula cha Mwisho, na William Henry Margetson

Juni 5–11

Yohana 14–17

“Kaeni Katika Pendo Langu”

Wakati unapojifunza kwa maombi Yohana 14–17, tafakari jinsi unavyoweza kuonyesha vyema upendo kwa wale unaowafundisha. Roho Mtakatifu ataleta mawazo katika akili yako unapojifunza maandiko, Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia , na muhtasari huu.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Andika nambari 14 mpaka 17 ubaoni, zikiwakilisha sura katika Yohana ambazo washiriki wa darasa walizisoma wiki hii. Waalike washiriki wachache wa darasa kuandika, karibu na kila nambari ya sura, marejeo ya mstari ambao Roho Mtakatifu aliwasaidia kuelewa vizuri au wangependa kujadili kama darasa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Yohana 14:16–27; 15:26; 16:7–15

Roho Mtakatifu hutuwezesha kukamilisha malengo yetu kama wafuasi wa Yesu Kristo.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza majukumu tofauti ya Roho Mtakatifu, fikiria kuwaalika kusoma moja au zaidi ya vifungu vifuatavyo: Yohana 14:16–27; 15:26; na 16:7–15. Wangeweza kuandika ubaoni kitu wanachojifunza kuhusu Roho Mtakatifu kutoka kwenye vifungu hivi. Wangeweza pia kutafuta utambuzi kuhusu Roho Mtakatifu katika maandiko na jumbe zilizoorodheshwa katika “Nyenzo za Ziada.” Je, ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu ametimiza majukumu haya katika maisha yao? Unaweza pia kufikiria juu ya vitu au vielelezo unavyoweza kuvileta darasani ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa baadhi ya majukumu haya.

  • Fikiria kuwaalika washiriki wachache wa darasa kabla ya muda kujifunza mojawapo ya hotuba za mkutano mkuu zilizopendekezwa katika “Nyenzo za Ziada” (au hotuba zingine za mkutano mkuu wanazozijua) kuhusu Roho Mtakatifu. Waruhusu kushiriki kwa muda mfupi kile walichojifunza pamoja na darasa. Je, jumbe hizi zinaongeza nini kwenye kile tulichojifunza kuhusu Roho Mtakatifu kutoka Yohana 14–16?

Picha
Yesu akizungumza na wanafunzi

Karamu ya Mwisho, na Clark Kelley Price

Yohana 15:1–12

Tunapokaa ndani ya Kristo, tutazaa matunda mazuri na kuwa na furaha.

  • Fikiria kuleta mche mdogo darasani (au picha yake) na kuutumia ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuvuta taswira ya mafundisho ya Mwokozi kuhusu mzabibu na matawi yake. Baada ya kusoma Yohana 15:1–12 kama darasa, mnaweza kujadili ina maana gani “kukaa katika [Kristo]” (Yohana 15:4). Washiriki wachache wa darasa wanaweza kushiriki jinsi walivyopata Yohana 15:5–5 kuwa ya kweli. (Ona pia maelezo kutoka kwa Mzee Jeffrey R. Holland katika “Nyenzo za Ziada.”)

Yohana 17

Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ni wameungana kikamilfu.

  • Pengine huwezi kufundisha kweli zote muhimu zinazopatikana katika Yohana 17 katika majadiliano ya darasa moja, bali hapa kuna njia ya kusaidia darasa kuchunguza kweli nyingine kadhaa. Orodhesha ubaoni mawazo kutoka Yohana 17, kama haya:

    • Uhusiano wetu na Yesu Kristo

    • Uhusiano wa Yesu Kristo na Baba Yake

    • Uhusiano wetu na ulimwengu wote

    • Uhusiano wetu sisi kwa sisi kama wafuasi Wake

    Muombe kila mshiriki wa darasa kuchagua mojawapo ya mawazo haya na kusoma Yohana 17, akipekua mistari ambayo inahusiana nayo. Waombe baadhi ya washiriki wa darasa kushiriki kile wanachojifunza.

    Ni jinsi gani uhusiano wetu na Mungu unagusa uhusiano wetu sisi kwa sisi? Ni kwa jinsi gani uhusiano wetu na kila mmoja wetu unavyogusa uhusiano wetu na Mungu?

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Roho Mtakatifu.

Kukaa katika Kristo.

Kumbuka kwamba neno kaa lina maana ya kudumu na kujitolea, Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

“Upambanuzi wa [neno] hili basi ni ‘ishi—bali ishi milele.’ … Njoo, lakini njoo ubakie. Njoo kwa dhamira na uvumilivu. …

“Yesu alisema, ‘Pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya lolote’ [Yohana 15:5]. Ninashuhudia kwamba huo ni ukweli wa Mungu. Kristo ni kila kitu kwetu sisi na tunatakiwa ‘tukae’ katika Yeye kwa kudumu, bila kukubali kushindwa, madhubuti, milele. Ili tunda la injili listawi na kubariki maisha yetu, ni sharti tujishikize Kwake kwa uthabiti, Mwokozi wetu sote, na kwa hili Kanisa Lake, lenye kubeba jina Lake takatifu. Yeye ni mzabibu ambao ni chanzo chetu cha kweli cha nguvu na chanzo pekee cha uzima wa milele. Katika Yeye siyo tu tutavumilia bali pia tutashinda na kushangilia katika kusudi hili takatifu ambalo kamwe halitatufanya tushindwe” (“Abide in Me,” Liahona, Mei 2004, 32).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Mwalike Roho. “Tunaweza kuwa vyombo katika mikono ya Mungu katika kuwasaidia watoto Wake kujifunza kwa Roho Mtakatifu. Kufanya hivyo, tunaalika ushawishi wa Roho katika maisha yetu na kuwahimiza wale tunaowafundisha kufanya hivyo pia. … Muziki mtakatifu, maandiko, maneno ya manabii wa siku za mwisho, madhihirisho ya upendo na ushuhuda, na nyakati za kimya za kutafakari zinaweza kualika uwepo wa Roho” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi10).

Chapisha