Agano Jipya 2023
Juni 12–18. Luka 22; Yohana 18: “Walakini si kama Nitakavyo Mimi, bali kama Utakavyo Wewe”


“Juni 12–18. Luka 22; Yohana 18: ‘Si kama Nitakavyo Mimi Bali Utakavyo Wewe’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Juni 12–18. Luka 22–17; Yohana 18,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Kristo na wafuasi wakiwa Gethsemane

Bustani ya Gethsemane, na Derek Hegsted

Juni 12–18

Luka 1222; Yohana 18

“Si kama Nitakavyo Mimi Bali Utakavyo Wewe”

Fikiria utafanya nini ili kumwalika Roho darasani kwako unapojadili matukio matakatifu katika sura hizi. Kwa maombi tafuta njia za kuwasaidia washiriki wa darasa kuongeza upendo wao kwa Mwokozi na imani yao Kwake.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike washiriki kadhaa wa darasa kushiriki kile wanachohisi walipokuwa wakisoma wiki hii na mistari gani iliwasaidia wao kuhisi hivyo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Luka 10:39–46

Tunakuwa zaidi kama Kristo tunapochagua kuyaweka mapenzi yetu kwa yale ya Baba.

  • Mfano wa Mwokozi wa kujitoa kwa ajili ya mapenzi ya Baba unaweza kuwasaidia washiriki wako wa darasa wakati wanapohitaji kufanya vivyo hivyo. Ili kuanzisha majadiliano, unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki uzoefu wao wakati walipokubali wenyewe kufanya kitu walichojua Mungu aliwataka wafanye. Waombe kueleza jinsi walivyojua kitu ambacho Mungu aliwataka wafanye na jinsi gani walibarikiwa kwa wao kujiweka chini ya mapenzi Yake. Alika darasa lisome Luka 22:39– 46 na kuzungumza kwa nini Mwokozi alikuwa tayari kuyaweka mapenzi Yake chini ya mapenzi ya Baba Yake. Je, tunawezaje kufuata mfano wa Mwokozi?

  • Kwa nyongeza kwa tendo la Mwokozi kujiweka chini ya mapenzi ya Mungu katika Luka 22:42, ni mifano gani mingine ya kujiweka kwake chini tunaipata katika Luka 22 na Yohana 18? Je, Mwokozi alijiwekaje chini ya mapenzi ya Baba Yake maisha Yake yote? Tunatakiwa kufanya nini ili tuweze kuwa kama Yeye? Maelezo kutoka Mzee Neal A. Maxwell katika “Nyenzo za Ziada” yanaweza kuwashawishi washiriki wa darasa kufikiria jinsi wanavyoweza kuyaweka mapenzi yao chini ya yale ya Baba.

Luka 22:39 –46

Yesu Kristo alifanya Upatanisho usio na mwisho kwa ajili yetu.

  • Luka 22:39–46 inaelezea kilichotokea Gethsemane. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa umuhimu wa kibinafsi wa tendo hili takatifu, labda unaweza kuandika ubaoni maswali kama Nini kilitokea Gethsemane? na Kwa nini ni muhimu kwangu? Washiriki wa darasa wangeweza kupata majibu katika Luka 22:39–46; Alma 7:11–13; Mafundisho na Maagano 19:16–19; na video ya “The Savior Suffers in Gethsemane” (ChurchofJesusChrist.org). Ungeweza kupata majibu katika ujumbe wa Rais Tad R. Callister “Upatanisho wa Yesu Kristo” (Liahona, Mei 2019, 85–87).

  • Katika Kitabu cha Mormoni, Yakobo anauita Upatanisho wa Yesu Kristo “upatanisho usio na mwisho” (2 Nefi 9:7). Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa kile hii inamaanisha, unaweza kushiriki mafundisho ya Rais Russell M. Nelson katika “Nyenzo za Ziada” na waombe washiriki wa darasa kuorodhesha njia ambazo nguvu ya dhabihu ya Mwokozi inaweza kufikiriwa kuwa haina kikomo. Wanaweza pia kusoma maandiko yafuatayo na kuongeza kwenye orodha yao: Waebrania 10:10; Alma 34:10–14; Mafundisho na Maagano 76: 24; na Musa 1:33. Tunawezaje kuonyesha shukrani zetu kwa kile Mwokozi amefanya kwa ajili yetu?

Picha
Petro akiangalia mbali kutoka aliko Yesu

Kukana kwa Petro, na Carl Heinrich Bloch

Luka 22:54–62

Tunaweza kuwa waaminifu kwa Yesu Kristo licha ya woga na udhaifu wetu.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuvuta taswira ya matukio katika Luka 22:54–62, unaweza kuonyesha picha, kama vile Kukana kwa Petro (ChurchofJesusChrist.org), au video ya “Jesus Is Tried by Caiaphas, Peter Denies Knowing Him” (ChurchofJesusChrist.org). Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile wanachojifunza kutokana na matukio ya Petro ambayo yanawashawishi wao kuwa waaminifu kwa Yesu Kristo.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kuweka mapenzi yetu chini ya yale ya Baba.

Mzee Neal A. Maxwell alifundisha: “Unapoyaweka mapenzi yako chini ya mapenzi ya Mungu, unampa Yeye kitu pekee ambacho unaweza kwa kweli kumpa Yeye ambacho ni chako halisi kumpa. Usingoje muda mrefu kutafuta madhabahu au kuanza kuweka zawadi ya mapenzi yako juu yake!” (“Remember How Merciful the Lord Hath Been,” Liahona, Mei 2004, 46).

Upatanisho usio na kikomo.

Rais Russell M. Nelson alifundisha:

“Upatanisho wa [Yesu Kristo] hauna kikomo—hauna mwisho. Ulikuwa pia hauna kikomo kwa sababu wanadamu wataokolewa kutoka kwenye kifo kisicho kuwa na mwisho. Ulikuwa hauna mwisho kwa hali ya mateso Yake makali. Ulikuwa hauna mwisho katika wakati, ukikomesha mfano wa kale wa dhabihu ya wanyama. Ulikuwa hauna mwisho katika mawanda—ulikuwa ufanyike mara moja kwa ajili ya wote. Na rehema ya Upatanisho imepanuliwa siyo tu kwa idadi ya watu isiyo na kikomo, bali pia kwa idadi kubwa ya dunia zisizo na kikomo zilizoumbwa na Yeye. Ulikuwa hauna mwisho hata kuzidi kiwango chochote cha upimaji au uelewa wa binadamu.

“Yesu alikuwa ndio mtu pekee aliyeweza kutoa upatanisho huu usio na mwisho, kwa vile alizaliwa na mama mwenye mwili unaokufa na baba mwenye mwili usiokufa. Kwa sababu ya haki hiyo ya kipekee ya kuzaliwa, Yesu alikuwa Kiumbe mkamilifu” (“Atonement,” Ensign, Nov. 1996, 35).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa chombo kinyenyekevu cha Roho. “Lengo lako kama mwalimu siyo kuwasilisha somo lenye kuvutia bali ni kuwasaidia wengine kupokea ushawishi wa Roho Mtakatifu, ambaye ni mwalimu wa kweli” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi10).

Chapisha