Agano Jipya 2023
Machi 6–12. Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9: “Hao Thenashara Yesu Aliwatuma”


“Machi 6–12. Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9: ‘Hao Thenashara Yesu Aliwatuma’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Machi 6–12. Mathayo 9–10; Marko 5 ; Luka 9,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili 2023

Yesu anamtawaza Petro

Machi 6–12

Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9

“Hao Thenashara Yesu Aliwatuma”

Unaposoma Mathayo 9–10; Marko 5; Luka 9, tafuta mwongozo wa kiungu kutoka kwa Roho Mtakatifu kuhusu mahitaji ya wale unaowafundisha. Kuandika misukumo yako ya kiroho kunaweza kukusaidia kujiandaa kwa tukio ambalo litakubariki wewe na washiriki wa darasa lako.

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kila mmoja kuandika juu ya kipande cha karatasi ukweli aliojifunza kutokana na maandiko ya wiki hii, ikijumuisha mistari ya maandiko. Baada ya kukusanya karatasi hizo, chagua kadhaa ili kuzisoma kwa darasa. Tunawezaje kutumia kweli hizi kwenye maisha yetu?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 9

Kristo ana uweza wa kutuponya kimwili na kiroho?

  • Mingi ya miujiza ya uponyaji wa Mwokozi pia inafundisha kweli za kiroho. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa hili, unaweza kuligawa darasa katika makundi manne na kulipangia kila kundi moja ya vifungu vifuatavyo: Mathayo 9:2–8; Mathayo 9:18–19, 23–26; Mathayo 9:20–22; na Mathayo 9:27–31 Liombae kila kundi kujifunza muujiza ulioelezwa katika kifungu chao na kisha kufupisha kwa ajili ya darasa zima. Ni kweli gani za kiroho tunaweza kujifunza kutoka kwenye miujiza hii?

mwanamke akigusa vazi la Yesu

Kutumaini katika Bwana, na Liz Lemon Swindle

Mathayo 10

Bwana anawapa watumishi Wake uwezo wa kufanya kazi Yake.

  • Agizo la Mwokozi kwa Mitume Wake linaweza kutusaidia katika wajibu wetu binafsi. Washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa wamepata umaizi katika mada hii kupitia mafunzo yao binafsi; kwa mfano, kuna shughuli kwenye mada hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Waalike wao washiriki kile walichojifunza au wafanye kazi katika vikundi vidogo kukamilisha shughuli hii darasani. Waalike washiriki wa darasa kushiriki uzoefu wakati walipohisi uwezo wa Mwokozi walipokuwa wakitimiza miito yao.

  • Ni kwa jinsi gani kujifunza agizo Kristo alilowapa Mitume Wake katika Mathayo 10 kunawasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa nafasi ya manabii na mitume wa sasa? Inaweza kuwa ya msaada kufananisha agizo la Mwokozi kwa wale Kumi na Wawili na agizo lililotolewa kwa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wa kwanza katika kipindi hiki, linalopatikana katika “Nyenzo za Ziada.” Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi wanavyovutiwa na huduma ya Mitume walio hai. Toa ushuhuda wako juu ya wito mtukufu wa manabii na mitume wanaoishi, na waalike washiriki wa darasa watoe wao.

Mathayo 10:17–20

Tunapokuwa katika huduma ya Bwana, atatupa mwongozo kwa kitu cha kusema.

  • Watu wakati mwingine wanahisi kuchanganyikiwa wanapofundisha au kuzungumza na wengine kuhusu injili. Lakini Bwana aliwaahidi wafuasi kwamba Yeye angewasaidia kujua kitu cha kusema. Tunahitaji kufanya nini ili kupokea msaada Bwana alioahidi kwa ajili yetu? Waalike washiriki wa darasa kusoma Mathayo 10:19–20; Mafundisho na Maagano 84:85; na Mafundisho na Maagano 100:5–8 ili kupata majibu ya swali hili. Ni wakati gani Roho Mtakatifu alikusaidia wewe kujua kitu cha kusema? Unaweza kushiriki uzoefu wako na uwaalike washiriki wa darasa kushiriki uzoefu wao.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Agizo kwa Mitume wa siku za mwisho.

Wakati baadhi ya washiriki wa kwanza wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili katika kipindi hiki walipoitwa, Oliver Cowdery aliwapa agizo sawa na lile Yesu Kristo alilotoa katika Mathayo 10. Alisema:

“Mtatakiwa kukabiliana na hisia za chuki za mataifa yote. … Kwa hiyo, ninawaonya mjenge unyenyekevu mkubwa, kwani najua kiburi cha moyo wa binadamu. Angalieni, ili msije kuinuliwa juu na wajipendekezao kwa ulimwengu. Angalieni ili kupenda kwenu kusivutiwe na vitu vya kidunia. Fanyeni huduma yenu iwe ya kwanza. … [Ni] muhimu kwamba mpokee ushuhuda kutoka Mbinguni kwa ajili yenu wenyewe, ili kwamba muweze kutoa ushuhuda kwenye ukweli. …

“‘… Mnatakiwa kupeleka ujumbe huu kwa wale wanaojifikiria wenyewe kuwa wenye busara. Na hao wanaweza kuwatesa; wanaweza kutafuta uhai wenu. Adui siku zote ametaka uhai wa watumishi wa Mungu. Nyinyi, kwa hiyo, mjiandae wakati wote kufanya dhabihu ya uhai wenu, ikiwa Mungu atauhitaji katika uendelezi na ujenzi wa kusudi Lake. …

“Kisha aliwachukua mmoja mmoja kwa mkono na alisema, ‘Je, kwa azma timilifu ya moyo wako unashiriki katika huduma hii, kuitangaza injili kwa bidii yako yote pamoja na ndugu zako hawa, kulingana na utaratibu na nia ya agizo ulilopokea?’ Kila mmoja wao alijibu kwa kukubali kwa dhati” (katika ““Minutes and Blessings, 21 February 1835,” Minute Book 1, 159–161, 164, josephsmithpapers.org; spelling and punctuation modernized).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Shuhudia juu ya baraka. Unapotoa mialiko ya kutenda, shuhudia kwa mwanafunzi wako kwamba watapokea baraka ambazo Mungu aliziahidi wanapotenda kwa imani juu ya mafundisho Yake. Baraka zisiwe msingi wetu wa motisha kwa utii, bali Baba wa Mbinguni anataka sana kuwabariki watoto Wake wote. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi35.)