Agano Jipya 2023
Machi 13–19. Mathayo 11–12; Luka 11: “Nami Nitawapumzisha”


“Machi 13–19. Mathayo 11– 12; Luka 11: ‘Nami Nitawapumzisha’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2022)

“Machi 13–19. Mathayo 11– 12; Luka 11,” Njoo,Unifuate—Kwa ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Yesu amesimama katikati ya mawingu

Usiogope, na Michael Malm

Machi 13–19

Mathayo 11– 12; Luka 11

“Nami Nitawapumzisha”

Soma Mathayo 11–12 na Luka 11 katikati ya wiki kabla ya kufundisha. Hii itakupa wewe muda wa kutafakari na kupokea ufunuo kuhusu kitu cha kuzingatia uwapo darasani.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kutumia kanuni tunazozipata katika maandiko kwenye maisha yetu ni njia muhimu ya kuonja nguvu ya neno la Mungu. Wahimize washiriki wa darasa kushiriki kitu walichokipata katika kujifunza kwao maandiko wiki hii ambacho wanaweza kukitumia kwenye maisha yao. Ukitolea mfano wa jinsi wewe ulivyotumia maandiko kunaweza kusaidia kuwashawishi washiriki wa darasa kuelezea mifano yao wenyewe.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mathayo 11:28–30

Yesu Kristo atatupatia pumziko tunapomtegemea Yeye.

  • Katika Mathayo 11:28–30, Mwokozi alifundisha kwamba Yeye atatusaidia kubeba mizigo yetu mizito kama tutaukubali mwaliko Wake “Jitieni nira yangu” (mstari wa 29). Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa vyema ahadi hii, ungeweza kuonyesha picha ya nira (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia) na shiriki kweli kama hivi: nira zimesanifiwa ili kusaidia wanyama kubeba mizigo mizito au kusaidia kazi ifanyike, na nira mara kwa mara imetengenezwa kumtosha mnyama husika. Je, maneno haya yanaongeza nini kwenye uelewa wetu wa Mathayo 11:28 –30? Ni mialiko gani tunayoipata katika mistari hii? Je, ni baraka gani tumeahidiwa? Ungeweza pia kushiriki ahadi iliyotolewa na Rais Dallin H. Oaks inayopatikana katika “Nyenzo za Ziada.”

  • Sisi sote tunayo mizigo ambayo inaweza kufanywa kuwa miepesi kupitia nguvu ya Yesu Kristo. Kuhimiza mjadala kuhusu hili, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma na kujadili Mathayo 11:28–30 pamoja na mtu mwingine darasani. Wangeweza kujumuisha maswali kama haya katika majadiliano: Ni mifano gani mingine ya mizigo mtu anayoweza kuwa amebeba? Tunahitajika tufanye nini ili tuweze kuja kwa Kristo? Je, inamaanisha nini kujitia nira ya Kristo sisi wenyewe? Ni kwa jinsi gani wewe ulihisi pale Mwokozi alipoifanya mizigo yako kuwa miepesi ulipomgeukia Yeye? Washiriki wa darasa wangeweza kutafuta utambuzi wa ziada katika ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Walibeba Mzigo Yao kwa Urahisi” (Liahona, Mei 2014, 87–90).

Picha
watu wakiwaangalia wanafunzi wakitembea katika shamba la ngano

Wanafunzi Wanakula Ngano siku ya Sabato, na James Tissot

Mathayo 12:1–13

Sabato ni siku ya kufanya mambo mema.

  • Katika dhamira yao ya kuishika kitakatifu siku ya Sabato, Mafarisayo walitekeleza sheria kali na desturi zao zilizowekwa na binadamu, ambazo hatimaye zilitia giza uelewa wao wa kusudi la kweli la siku ya Sabato. Ili kuanzisha majadiliano kuhusu kwa nini Bwana alitupatia siku ya Sabato, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kurejelea Mathayo 12:1–13 na Tafsiri ya Joseph Smith, Marko 2:26 –27 (katika kiambatanisho cha Biblia). Maelezo haya yanatufundisha nini kuhusu umuhimu wa maandiko? Ni utambuzi gani wa ziada kuhusu Sabato tunaoupata katika Kutoka 31:16–17; Isaya 58:13–14; na Mafundisho na Maagano 59:9–13? Je, ni kwa jinsi gani uhusiano wetu na Mwokozi umebadilika tulipojaribu kushika kitakatifu siku yake?

  • Wakati Mafarisayo walisisitiza sheria nyingi za kila kitu kuhusu Sabato, Mwokozi alifundisha kanuni rahisi: “Ni halali kutenda mema siku ya Sabato” (Mathayo 12:12). Je, ni kanuni gani nyingine inatusaidia sisi kuishika kitakatifu siku ya Sabato (ona maelezo ya Rais Russell M. Nelson katika “Nyenzo za Ziada”). Kwa nini kanuni huleta matokeo mazuri zaidi kuliko mlolongo wa sheria katika kukuza kujitegemea kiroho?

  • Ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Sabato Ni Furaha” (Liahona, Mei 2015, 129–32) na video za ushauri wa Mzee Jeffrey R. Holland “Nyenzo za Ziada” zinaweza kuongeza katika majadiliano kuhusu siku ya Sabato.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Jitie Nira pamoja na Yesu Kristo.

Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Unakuja kwa Kristo ili ufungwe nira pamoja Naye na pamoja na nguvu Zake, ili kwamba usivute mzigo wa maisha peke yako. Unavuta mzigo wa maisha ukiwa umefungwa nira pamoja na Mwokozi na Mkombozi wa ulimwengu, na ghafla matatizo yako, bila kujali ni mazito kiasi gani, yanakuwa mepesi zaidi” (“The Mission and Ministry of the Savior: A Discussion with Elder Russell M. Nelson,” Ensign, June 2005, 18).

“Ni ishara gani ninataka kuitoa kwa Mungu?”

Rais Russell M. Nelson alifundisha: Nilipohitaji kufanya maamuzi ya kujua kama shughuli ilikuwa au haikuwa sahihi kwa ajili ya Sabato, nilijiuliza mwenyewe, ‘Ni ishara gani ninataka kumwonyesha Mungu?’ Swali hilo lilifanya uchaguzi wangu kuhusu siku ya Sabato kuwa dhahiri zaidi” (“The Sabbath Is a Delight,” Liahona, Mei 2015, 130).

Baraka za kutii siku ya Sabato.

Katika mfululizo wa video tatu, Mzee Jeffrey R. Holland anafundisha kuhusu baraka za kutii siku ya Sabato: “Upon My Holy Day—Getting Closer to God,” “Upon My Holy Day—Honoring the Sabbath,” na “Upon My Holy Day—Rest and Renewal” (ChurchofJesusChrist.org).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza Kushiriki. “Kila mtu katika darasa lako ni chanzo kikubwa cha ushuhuda, utambuzi, na uzoefu kutokana na kuishi injili. Waalike kushiriki pamoja na kuinuana” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi5).

Chapisha